Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!

Sitashangaa kusikia next President ni msukuma tena!!.
Maadam kwenye uchaguzi wa rais wa Tanzania, hatuchagui kabila ya mtu, bali tunamchagua mtu mwenye sifa na vigezo, ikitokea mwaka 2020, mtu mwenye sifa na vigezo ni Msukuma, tutamchagua!. Hatutamchagua kwa Usukumani wake, bali kwa sifa na vigezo vyake.

Hili Mwalimu Nyerere amelifafanua vizuri sana, kama "mtu hana sifa, hatutamchagua kwasababu ni kabila langu", au mtu ana sifa zote, hatukataa kumchagua kwasababu ya kabila lake!", kumchagua mtu kwasababu ya kabila lake ni ubaguzi, na kumkataa mtu kwasababu ya kabila lake pia ni ubaguzi!, ikitokea kwa sasa wenye sifa ya urais ni Wasukuma tuu, let it be!.
P
 
HILI JAMBO WAPEWE WANANCHI KAMA WENZETU RUSSIA WALIVYOFANYA NA LIKAFANYIKA VEMA

Putin aridhia uwezekano wa kumuongezea muhula madarakani​

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameunga mkono pendekezo la mabadiliko ya katiba, ambayo yatamwezesha kubakia madarakani kama rais baada ya muhula wake wa sasa kumalizika mwaka 2024.
Mabadiliko hayo yatawezekana ikiwa yataungwa mkono na raia wa Urusi katika kura ya maoni juu ya marekebisho ya katiba, na kisha Mahakama ya Katiba iridhie kwamba kwa kupanga upya kikomo cha mihula ya urais, katiba haitakuwa imekiukwa.

''Kwa pamoja, bila kujali mambo mengine, tumeweza kufanya mengi katika kuiimarisha nchi yetu'' amesema Putin mbele ya wabunge, na kuongeza kuwa ''Nina uhakika kuwa tunaweza kufanya mengine zaidi hadi mwaka 2024, na baada ya hapo, tutaona kitakachotokea.''

Uwezekano wa kuongoza hadi mwaka 2036 au milele?

Ikiwa mabadiliko hayo yatafanikiwa, Putin anaweza kubakia madarakani hadi mwaka 2036. Kauli yake imekuja siku moja tu, baada ya kukanusha dhana ya urais wa maisha, mtindo wa enzi za Umoja wa Kisovieti.
 
Maadam kwenye uchaguzi wa rais wa Tanzania, hatuchagui kabila ya mtu, bali tunamchagua mtu mwenye sifa na vigezo, ikitokea mwaka 2020, mtu mwenye sifa na vigezo ni Msukuma, tutamchagua!. Hatutamchagua kwa Usukumani wake, bali kwa sifa na vigezo vyake.

Hili Mwalimu Nyerere amelifafanua vizuri sana, kama "mtu hana sifa, hatutamchagua kwasababu ni kabila langu", au mtu ana sifa zote, hatukataa kumchagua kwasababu ya kabila lake!", kumchagua mtu kwasababu ya kabila lake ni ubaguzi, na kumkataa mtu kwasababu ya kabila lake pia ni ubaguzi!, ikitokea kwa sasa wenye sifa ya urais ni Wasukuma tuu, let it be!.
P
Pasco bana
Siasa mingi sana veve.
mzee wa kung'ata na kupuliza...😀😀😛😛
 
Huna hekima wewe. Makonda hata ukuu wa wilaya hana uwezo. Uwezo wake wa asili kupambanua issues ni mdogo sana. Inaweza kuwa hatari. Unajua hata magu kinachomsaidia 'anabebwa-bebwa'?
 
Kama teuzi tu amekosa ndo uraisi atapata.
Majira yake yalishapitwa,si tishio tena raia Wana amani. Hana amri, hana madaraka, ni sawa na raia tu wa kawaida ambae mnaweza mkadindiana tu. Amri pekee aliyonayo labda kumuamrisha mkewe tu
 
Wanabodi,
Kabla Magufuli hajawa rais wetu, sisi wengine wenu tulijua tangu mwaka 2014 na tukasema humu!.Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli

Miongoni mwa sifa zilizomuibua Magufuli ni sifa inayoitwa "uthubutu" unreasonably ambayo wengine huita ni udikiteta. Yaani kuachana na mambo ya kufuata sheria, taratibu na kanuni, ndiyo yametufikisha hapa, hawa viongozi wenye "uthubutu" hawahitaji kujua sheria, taratibu na kanuni, zinataka nini, bali hufanya lile linalowezekana,

Ndio maana tukasema humu, japo Magufuli kweli ni dikiteta, Tanzania mahali ilipofika ilimhitaji mtu kama Magufuli na Mwenyeenzi Mungu akaisikia sala yetu, akatupatia Magufuli!.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Tukija kwa Makonda, muda mfupi baada ya kuteuliwa DC wa Kinondoni, akaonyesha uwezo, hivyo kama ilivyokuwa kwa Magufuli, mwaka 2014 tulisema ni Magufuli, na mwaka 2015 kweli akawa yeye. Vivyo hivyo kwa Makonda akiwa DC, akina sisi tukasema hivi Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam
Na kweli haukupita muda akawa!.

Hivyo kwa hii kazi nzuri yote anayoifanya Magufuli, atakapoondoka ile 2025, kama hatamuachia nchi mtu mwenye kufuata nyayo zake, hii kazi nzuri yote ya Magufuli itakuwa ni kazi bure! . Hivyo nimeshauri Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Kwa vile katiba sio Msahafu, 2025 tuibadili katiba Magufuli aendelee indefinitely kama Mugabe, mpaka atakapo choka kabisa na kuwa hawezi tena kwa incapacitation, au tumsubirie Mungu, au Tanzania sasa na sisi tuanze mtindo wa spotting na headhunting na kumfantia grooming huyo headhunted.

Kwa maoni yangu Makonda atatufaa sana kumpokea Magufuli, maana kiukweli huyu Jamaa atatufaa sana kwa sababu ana uthubutu mkubwa zaidi kuliko hata Magufuli. Makonda akimpokea kiukweli kabisa Tanzania itanyooka.

Magufuli pamoja na mazuri yake, naye kama binadamu pia ana madhaifu na mapungufu yake, Vivyo hivyo Makonda pia sio malaika naye ana mapungufu yake, moja ya mapungufu makubwa ya Makonda ni inferiority complex inayopelekea ku practice superiority complex na kujikuta ana over do bila kujijua.

Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.

Mfano ni jinsi anavyojikomba komba kwa rais Magufuli mpaka kupindukia, karibu kila jambo lazima amtaje rais Magufuli tena kwa majina yake yote manne na sifa zake zote nne "Rais Wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli" (si mnajua watu wa Kanda yetu kwa kupenda masifa). Makonda lazima afike mahali aonyeshe anaweza kusimama on his own na sio kila wakati kutegemea apron strings za rais Magufuli.

Hivyo 2025 rais Magufuli asipoongeza muda, Makonda atatufaa sana. Kwa vile Makonda ni Mlolomije, kwa kuanzia 2020 akalichukue lile jimbo la yule chapombe, na atashinda kwa kishindo na kupewa moja ya important portfolio zenye impact, ili 2025 ampokee Magufuli.

Kitendo cha mtu wa Kanda ya Ziwa kushika urais kama alivyo rais Magufuli, ni dalili ya Tanzania kutenda haki ya wengi wape, yaani wenye haki na uhalali wa kutawala nchi ni wale walio wengi!. Hivyo baada ya rais Magufuli aje rais Makonda, na baada ya hapo tuendelee kule kule mpaka na makabila mengine wawe ni walio wengi ndipo nao wastahiki! .

Makonda konyesha uwezo wa uthubutu, jee mnalionaje hili la kwanini asiwe Makonda kumpokea Magufuli?.

Kwa kwa wale mashabiki wa upinzani mtanisamehe bure, kwenye urais upinzani ni bado sana.

Paskali.
Update,
Kumbe wanaoesema baada ya Magufuli, Makonda atatufaa, siko peke yangu,
Msikilize kiongozi huyu wa dini, msikilize mpaka mwisho

Viongozi wakuu wa dini, wanaletwa na MWENYEWE YEYE, hivyo baada ya kuisikia kauli kama hiyo ya kiongozi wako wa dini, wewe kama ni muumini safi na wa kweli, ni kuikubali, hiyo ni sauti ya Mungu ikinena kupitia vinywa vya Manabii, wewe ni nani upinge?.
P
Ama mayala,wewe ni hinga kubwa la mfano wake
 
Kama teuzi tu amekosa ndo uraisi atapata.
Majira yake yalishapitwa,si tishio tena raia Wana amani. Hana amri, hana madaraka, ni sawa na raia tu wa kawaida ambae mnaweza mkadindiana tu. Amri pekee aliyonayo labda kumuamrisha mkewe tu
Unamkumbuka yule katibu wa chama cha madereva wa malori tanzania aliyekufa kifo kilichozua utata? Basi uwe na adabu
 
Yaani Pascal siku hizi sijui umekuwaje!yaani hata kama ni njaa sio hivyo!post zako za sasa zinakosa credibilities!unaonyesha biased ya wazi na kulamba miguu!wewe ni mtu mzima!hembu tulia unajichoresha sana!
 
Hivi alishajibu tuhuma kuhusu Matata🤣🤣🤣
 
Ili aje kua rais muda huu ilitakiwa awe kwenye wizara haswa ya mambo ya nje na ingependeza kama ubunge wake ungekua wa kupigiwa kura na wananchi.

Ingeonyesha anaaminiwa na wananchu na pia hiyo post ingemsogelesha karibu na maswala mtambuka na watu mbalimbali.

Shida ingekua hiko kizuizi cha marekani.
 
Kwa hapa nyumbani kwa wale wanaopendekeza nani awe nani sijawahi kuona wakimtoa mtu ambaye ana mawaa yeyote.

Fuatilia marais wote waliowahi kuongoza; iwe Nyerere, Mwinyi, Mkapa ama kikwete, Wana background nzuri Kijamii na kielimu, hakuna ambaye kasoma shule nyepesinyepesi , ukitoa nyerere wote wamekuwa Mawaziri kabla ya kushika Urais, hivyo rekodi nzuri ya utendaji serikalini katika nafasi za juu, imebakia kua moja wapo ya sifa kwa Rais Mtarajiwa. Hivyo ukitaka kuangalia nani anafaa hiyo nafasi usisahau kuangalia na hilo pia.
 
Hv DAB akiopoa uprezidaa ktk watu watakaoneemeka si pamoja ma ww
 
Makonda ana kipi special kiasi cha kumuona anafaa?
anza na mwaka wake mmoja wa ukuu wa mkoa ni innovation idea gan iliyowasaidia wananchi zaidi ya siasa za muda mfupi?

Huyu ni muuaji; alihusika moja kwa moja na jaribio la kutaka kumuua Lissu! Mmesahau jinsi alivyomteka Roma Mkatoliki halafu leo mnaaza kuleta uchafu wenu hapa; kwani mnadhani watu wa nchi hii ni matahira? Kama mnampenda sana mkatieni hekari za shamba akalime si mnahimiza Vijana wajiajili!!!
Mlivyokuwa wasahaulifu hata hamkumbuki kuwa Bashite ni persona non grata kule marekani [ Yaani amepigwa spana hawezi kanyaga ardhi aliko ROMA Mkatoliki hivi sasa] Maisha Yake yote!!!
 
Back
Top Bottom