Baada ya Malalamiko ya wananchi, Serikali yasitisha bei mpya za vifurushi

Samia safiiiiii...mama la mama safiiiii??

Nilijua tu, waziri wa teknolojia wa saivi ni wa hovyo kuwahi kutokea ...na sijui kwanini mama la mama amemuacha, ila nina imani na mama hii product ya kipuuzi ataitupilia mbali
Na wewe unatakiwa utumie akili, wewe unadhani huyo rais alikua hajui kwamba bando linaongezeka? Alafu eti unakaa unamsifia daaah sijui ujinga utatuisha lini!!

Kwa kifupi ujue waziri hawezi kufanya maamuzi bila rais na makamu wake kujua!! Na mpaka waziri anafanya maamuzi jua ana baraka zote kutoka kwa rais. Acha kusifia upuuzi.
 
Wanatuchezea akili washaona watanzania hatujui kuhoji, washushe na bei kbs.
Batch of idiots
Mimi nasema Mkurugenzi Mkuu wa TCRA lazima ang'oke huyo. Hawa ndo vimelea vya Jiwe vimebakia vinasumbua watu kama huyo DG wa TPA...!!!
 
Tokea Mwinyi ajiuzulu Uwaziri uliwahi kusikia Waziri mwingine kama sio kutumbuliwa
Huyo mzee Mwinyi aliacha legacy ambayo siyo rahisi kuifuta.....!!!
Legacy hiyo bado inaendelea kumbeba hata mwanae Hussein!!!
 
Pumbavu wewe ! Huelewi unachokisema, wakati mama anaingia tayari huyo ndungugile sijui alikua amesha implement mabadiliko ya bando na pengine marehemu alikua ameshakubali, sasa mama ameingia na yamesitishwa wewe kwa akili zako za kiduwanzi huoni ni jambo la kupongezwa ?
 
Na wewe tuondolee udwanzi wako.
Hivi unajua kitu kinaitwa BARAZA LA MAWAZIRI(Cabinet of Ministers)?
Unataka kutuambia Mama Samia na Bwana Mpango hawakuwepo kwene Cabinet wakti Ndugulile akiwasilisha huo upuuzi wake toka TCRA na Makampuni yao na wakapewa blessings na Serikali?? Shame on you.
 
Kweli mkuu,, bora hata angekuwa na hizo akili za kizamani, usikute hana akili hata 1!
 
Japo sijasoma nisingekubali huu utopolo Ndugulile amefanya.
 
Wakati magu anakubali mama samia si alikua VP? Kuna kitu rais atafanya VP wake asijue?
 
Serikali Yasitisha Bei Mpya Za Vifurushi Vya Internet

Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA), imesitisha kwa muda matumizi ya bei mpya ya vifurushi vya data ili kutoa nafasi kwa watoa huduma kupanga upya bei za vifurushi kwa ufanisi na kufanya uchambuzi wa kina kwa ajili ya kulinda maslahi ya watumiaji.

Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni muda mfupi baada ya kampuni za mawasiliano ya simu kutoa maboresho ya vifurushi ambavyo vimeanza kutumika Aprili 2, 2021, ikiwa ni sehemu ya matakwa ya kanuni ndogo za vifurushi.

Baada ya vifurushi vipya kutolewa, baadhi ya wananchi kupitia mitandao ya kijamii wamelalamikia kile walichoeleza kuwa ni kupanda kwa gharama za vifurushi, tofauti na matarajio yao kuwa gharama zingepungua.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…