Lazima ajue maana yeye ndie alikuwa bingwa wa hizo mishe kwa hayati na mtoa Siri mkuu wa serikali Ila asubirie karma iko njiani atakosa wa kumlalamikia tena
Viongozi hawawazi shinda za wananchi lakin wanawaza uchunguzi wa 2025 ni aibu sana ,vijijin hakuna umeme ,maji ,hospital na madawa,watoto wanaenda peku mashulen ,wafanya Kazi mishahara haiongezek
Ki-Katiba Spika Kama anatokana na wabunge atapoteza nafasi ya uspika Kama hana sifa za kuwa mbunge. Sifa ya kuwa mbunge ni kuwa mwanachama wa Chama cha siasa! Rais ndiyo Mwenyekiti wa CCM kwa hiyo Chama kikimvua uanachama tu amekosa uspika na ubunge na hata Mafao halipwi.
Ila Ndugai ni mburula na wenzie akina Bashiru wamemtanguliza yeye naye kaingia kingi.
Hii conflict Kati ya executive na Bunge itufungue macho kwa hitaji la katiba mpya. Speaker kuzodolewa namna ile ni kuonesha ya kwamba Bunge letu halina nguvu. Katiba mpya inahitajika kuweka checks and balances. Tatizo ukisema katiba mpya watu wanafikiria CHADEMA basi, lakini madhara Kama haya hawayaoni.
Nakumbuka fulani aliwahi kutoa kauli ya kupumzika siasa 2025, alichofanya "mwenye nchi" leo ni kuonesha yeye binafsi anavyoiwaza 2025 na ameshanogewa na cheo, ndio maana alikuwa wa kwanza kuwaambia wanawake wenzake 2025 ni zamu yao.
Mengi ya maneno aliyotoa kumjibu mwenzake leo ni mihemko tu na kuchamba kama zilivyo tabia za wanawake wengi, lakini hana hoja yoyote ya msingi.
Kwa hii kauli yake ya leo inawezekana akaamsha vita ya chini chini ambayo hatajua ukubwa wake na miongoni mwa adui zake watakuwa hao wanaompigia vigelegele leo.
Hakuna atakayeamsha vita ndani ya ccm. Kumbuka wengi ni mafisadi na wana makando kando mengi. Ni rahisi kushughulikiwa ukiinua kichwa tu. Wapinzani ndio wanaweza. Kauli ya Nduhai imeshasemwa na wapinzani kila mara lakini hawakufanywa kitu maana hawana cha kupoteza.
Kwanza kabisa mi naamini Mh. Job Ndugai hakumaanisha kudharau mamlaka ya Rais, ila alichukulia ni kauli ya kawaida kama ambavyo unajua watanzania.
Ila Mh. Rais inaonekana hajiamini kabisa kutokana na makundi yaliyopo ndani ya CCM na hii ilichangiwa na huyo mnoko aliyemuambia adui yake ni shati la kijani (mtu huyu alijua madhaifu ya Mama akaona amfarakanishe kabisa na wana CCM ili wao ikija 2025 wapate pakutokea).
Jambo lingine lililopo mbele ni uwezekano wa Mama kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye (hii inawezekana kabisa kwa sababu mpaka sasa Mama ni dhahiri kifo cha Dkt Magufuli yeye ni kama alikipanga kitokee awe Rais (hii inatokana na kauli zake za kudra za mwenyezi mungu na uchu wa urais alionao).
Uchu wake wa urais umemjengea maadui wengi sana ndani ya CCM na kwa sasa wanamuangalia kama adui yao namba moja kiasi kwamba wabunge wengi wataunga mkono hoja ya kutokuwa na imani na rais.
Na Ndugai hawezi kuachia ngazi labda wamuue kwa sababu hana cha kupoteza.
Na huu ugomvi mama kautafuta mwenyewe kwa kuamini vitu ambavyo si vya kweli kwa sababu moyoni mwake kabisa Ndugai naamini hakumaanisha kudharau mamlaka ya rais na viongozi wote waandamizi wanamheshimu mama ila yeye mama inaonekana ni mtu wa kujishuku shuku, na hiyo inaweza pelekea kuungwa mkono Ndugai bungeni na hatimaye kumpigia kura ya kutokuwa na imani Mama.
Mama asipokuwa makini, hatoweza kutimiza miaka yake 5, atapigiwa kura ya kutokuwa na imani na urais wake ukaishia hapo na tena wanaweza hata kumfungulia mashitaka na anaweza kusota ndani kwa sababu yeye kaonekana kushangilia kifo cha mtangulizi wake na uchu wa urais (kwa sababu aelewe aliyekufa ni mtu mmoja-Dkt Magufuli na ile machinery ya urais ipo inamcheki vizuri mienendo yake).
Ni hayati baba wa taifa aliyetuwekea utaratibu kuwa UTII KWA MWENYEKITI NI LAZIMA...IWE HADHARANI AMA KIFICHONI......
Hizo ndizo itikadi zetu tunazoziimba katika madarasa ya ITIKADI.....
CCM imefika hapa kwa sababu ya kanuni hiyo KUU....
Wanabodi,
Hili ni bandiko la ma GT, hivyo hatutataji majina na naomba usitaje jina lolote!.
Hatua ya kwanza ni sikiliza kauli hii
Hivi hata baada ya kauli kama hii, kama wewe ni mtu mzima na akili zako timamu, bado unasubiri nini to do the right thing, the needful?.
Swali ni jee tumshauri mtu wetu, a do the needful, au akomae nao, till they do him away?.
Mimi nimemsikiliza Mama, kiukweli hajamtendea haki mtu wetu!, zile kauli kuhusu tozo, mikopo na deni la Taifa ni kauli za kizalendo na wala sio homa 2025, kwasababu kiukweli kabisa mtu wetu, hajawahi hata kuwazia 2025 kwasababu ndani ya CCM kuna a silent code ya kupokezana fulani kati ya Wakatoliki na wale jamaa zetu!.
Kwa vile alianza Mkatoliki, Juliasi akaja Jamaa zetu, Hasani, akaja Mkatoliki Benyamini Wiliamu, akaja jamaa zetu Mrisho, akafuta Yohane Yosefu, hivyo 2025 ilikuwa ni zamu ya wale jamaa zetu na Mungu ndio akawatangulizia, hivyo kusema kauli ile ya kizalendo ni homa ya 2025, huku ni kumsingizia bure tuu huyu mtu wetu!.
Kwa vile the boss is always right, ikitokea ume differ na boss wako, to the point ya bosi wako to question your intellect "mtu mzima mwenye akili timamu", the best way is to Quitt, the sooner, the better.
Namalizia kwa swali hili la msingi, baada ya maneno haya ya Rais Samia, kama mtu wetu ni timamu, he shoud do the right thing, "the needful", jee tumshauri to do the right thing, "The Neeful?", before its too late, au akomae nao, mpaka kieleweje, if it is to do him away, akomae till they do him away?. The game is on again, it is not over yet until it's over.
Wanabodi, Japo siku zote Nabii huwa hakubaliki nyumbani, hili nalijua na litabezwa, na nimeisha lisemea humu TZ Tulipo Sipo!. Nabii Hakubaliki Nyumbani, JF Tuna Manabii wa Kweli, Tuwatumie Walisaidie Taifa!. - JamiiForums Hii ni thread ya maono ya unabii, na sio utabiri na sio trends reading...
Tizama mtu wetu alifanya kosa la kuomba msamaha technical error. Lakini kwa vile mtu wetu nae anao muhimili wake basi autumie vizuri awashawishi wabunge wapige kura ya no confidence na serikali, bunge livunjwe uchaguzi uitishwe atakaepata apate na atakaekosa akose. Huko CCM mwanachama yoyote aruhusiwe kugombea hiyo kofia ya mfalme
Huku arbabu mwenyekiti wa CCM kule Kanda ya ziwa mh.mzee KM akisimama imara mno kutetea jahazi....nyimbo zikahanikizwa "TUNA IMANI NA DESH DESH OYAA OYAA OYAAA"🎼🎼
Wajumbe "wake" waliokuwa ni zaidi ya 70% ya akidi ya wajumbe wote hawakumsaidia "mwamba" kutokuzama🤣
NGUVU YA MWENYEKITI IKAONEKANA NA PANGA LIKAFYEKA SHINGO YA MTU.....
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.