BREAKING NEWS: UMOJA WA WATU WALIOATHIRIKA NA MAGONJWA YA AKILI (UWAWAMA) wamemchangia Mh. Edward Lowassa shillingi Laki nane na kumsihi kuchukua fomu ya kugombea uraisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Akizungumza walipokwenda kumtembelea nyumbani kwake mjini Dodoma wanachama hao wakiongozwa na Mwenyekiti wao Ndugu Taabani Maajabu walimueleza kuwa wamesukumwa kumuomba Mh. Lowassa kugombea kutokana na umahiri wake katika kusimamia uboreshwaji wa sekta ya afya wakati akiwa waziri Mkuu wa kwanza wa Awamu ya nne. Waathirika hao wamemuelezea waziri Mkuu huyo mstaafu aliyekuwa karibu na wagonjwa wengi nchini na hasa waathirika wa magonjwa ya akili kuwa mtu shupavu na mbisho aliyewapigania sana kuanzisha mifuko yao ya maendeleo alipokuwa waziri mkuu. Kwa kutambua uwezo wake waathirika hao wa magonjwa ya akili wamemuomba Mh. Lowassa asisite kuchukua fomu na wao watakuwa nyuma yake kuhakikisha wanampigania mpaka kufikia mwisho wa safari mpya ya matumaini.