Baada ya Mazishi ya Hayati Magufuli tuambiwe ni kiasi gani cha pesa kilichotumika kwenye shughuli nzima

Kwa jinsi hii shughuli ya msiba inavyoendeshwa inaonyesha wazi kuna mabilioni ya fedha yanapotea kwa kutumia mgongo wa kumzika kiheshima Rais Magufuli.

Kuna wengine bila shaka wanatumia fursa hii kupiga pesa, pesa ambazo kwa namna moja au nyingine zingesaidia mambo mengi mno MF madawa hospitalini, upanuzi wa barabara, mikopo kwa wanafunzi, mishahara nk.

Mh rais Magufuli enzi za uhai wake miongoni mwa vitu ambavyo alikuwa havipendi ni matumizi yasiyo ya lazima ya pesa ndio maana alikuwa mstari wa mbele kwenye kubana matumizi.

Hivyo basi si mbaya tukajua ni kiasi gani cha pesa kilichotumika kwenye mazishi yake.

Pia tukijua ni kiasi gani cha pesa kilichotumika kwenye kugharamia hiyo peace maker kwa siku kwa kipindi chote alichokuwa madarakani kama rais.
Mkuu we jikalie kimya tu, hii ndio Nchi masikini pekee ambayo inatumia mabilioni ya hela kumzururisha Mtu (Rais) alietangulia mbele ya haki wakiamini hakustahili kufa kipindi hiki,

Tena mtu ambae alipinga kwa dhati matumizi makubwa ya pesa kwa shughuli ambazo hazina ulazima sana.tule ugali tukalale.
 
IMG-20210326-WA0057.jpg
 
Yani hata zingetumika zote mtu huyu alistahili Kumbuka pesa unazoziongelea yeye ndie alokuwa mstari wa mbele kuwakaba mabeberu hadi hizo fedha ndio tukajua kumbe hatukuwa maskini.Mwanga wa milele Bwana amuangazie
 
Yaani inatakiwa mtoke kwenye hayo maisha msiba wowote ukiwa unaendelea ninyi mnafikiria hela na nguo alizoacha marehemu...
Hapa ndipo akili za mwafrika zina tatizo!!yaani mwananchi kutaka kuulizia matumizi ya kodi yake ni kosa??pesa iliyotumika kwenye shughuri yote ya mazishi ni kodi yetu, na lazima (kama serikali ni ya uwazi gharama ijulikane)kwani haya mambo ya kufanya mambo kwa siri ndio huleta shida, mbona mambo haya kwa wazungu huwa yanakuwa wazi tu??sio kwa nia mbaya lakini inasaidia kuwa wahusika wanajua kabisa kuwa baada ya shughuri matumizi ya pesa hizo yataulizwa.
 
Yani hata zingetumika zote mtu huyu alistahili Kumbuka pesa unazoziongelea yeye ndie alokuwa mstari wa mbele kuwakaba mabeberu hadi hizo fedha ndio tukajua kumbe hatukuwa maskini.Mwanga wa milele Bwana amuangazie
Miaka mitano tu umekopa kwa hao mabeberu trilioni 35!!!!daaa hatari sana!!suala la kujitegemea tungeweza kufika lakini sio kwa mala moja hivyo!!!kama tulivyokuwa tukiaminishwa, kuwa kila mradi tunaojenga ni kwa pesa yetu, sasa hayo matrilioni vipi tena?!!kuendesha serikali kwa kificho ficho, yaani ilifikia hata serikali kukopa ni kwa siri!!haitaki wananchi kujua?!!
 
Hapa ndipo akili za mwafrika zina tatizo!!yaani mwananchi kutaka kuulizia matumizi ya kodi yake ni kosa??pesa iliyotumika kwenye shughuri yote ya mazishi ni kodi yetu, na lazima (kama serikali ni ya uwazi gharama ijulikane)kwani haya mambo ya kufanya mambo kwa siri ndio huleta shida, mbona mambo haya kwa wazungu huwa yanakuwa wazi tu??sio kwa nia mbaya lakini inasaidia kuwa wahusika wanajua kabisa kuwa baada ya shughuri matumizi ya pesa hizo yataulizwa.
Sasa hapa atakujibu nani?
Kwanini usiende kuuliza kwenye mamlaka husika maana hata sisi hatujui
Kuuuliza uliza kama hivi ni dalili za umaskini
 
Hata kama hakuna wanaobwia pesa kwa mgongo wa msiba...

Hakuna sababu ya kutumia mabilioni ya Shilingi kufanya msiba. KUNA WATU wa ajabu sana. Wanaojua hata marehemu asingepemda matumizi makubwa namna hiyo. Eti wao wanatumia kwa kuwa hayupo.

Kwa haraka haraka utagundua, watu wabadhilifu wafuja mali ni wengi sana. Watu wasiofikiria mbali ni wengi
 
Sasa hapa atakujibu nani?
Kwanini usiende kuuliza kwenye mamlaka husika maana hata sisi hatujui
Kuuuliza uliza kama hivi ni dalili za umaskini
Sorry!!hivi unaelewa maana ya forum?tuanzie kwanza hapo!!
 
Haina haja ya kuzuga na hilo swali kila mtu anajua ..
Hapa hujauliza ila unapiga porojo na udaku
Haya niambie umejibiwa tayari bajeti ni kiasi gani imetumika?
 
Wewe ukipata mdiba kwako pesa hazitumiki?
Hebu kuweni mnasoma na kuelewa kabla ya kudandia hoja!!inshu hapa sio kuwa pesa haijatumika, pesa imetumika na ni nyingi, lakini kama wananchi wanatakiwa kuambiwa ni kiasi gani, kwa ni pesa zao!!(serikali zenye uwazi lakini)
 
Hiyo ndio tofauti ya Msiba wa Hayati na hao Marehemu wenu. Msiba wa Hayati hakuna budget wala michango
 
Kwa jinsi hii shughuli ya msiba inavyoendeshwa inaonyesha wazi kuna mabilioni ya fedha yanapotea kwa kutumia mgongo wa kumzika kiheshima Rais Magufuli.

Kuna wengine bila shaka wanatumia fursa hii kupiga pesa, pesa ambazo kwa namna moja au nyingine zingesaidia mambo mengi mno MF madawa hospitalini, upanuzi wa barabara, mikopo kwa wanafunzi, mishahara nk.

Mh rais Magufuli enzi za uhai wake miongoni mwa vitu ambavyo alikuwa havipendi ni matumizi yasiyo ya lazima ya pesa ndio maana alikuwa mstari wa mbele kwenye kubana matumizi.

Hivyo basi si mbaya tukajua ni kiasi gani cha pesa kilichotumika kwenye mazishi yake.
Uambiwe wew kama nani.kapuku
 
Back
Top Bottom