Baada ya Mazishi ya Hayati Magufuli tuambiwe ni kiasi gani cha pesa kilichotumika kwenye shughuli nzima

Baada ya Mazishi ya Hayati Magufuli tuambiwe ni kiasi gani cha pesa kilichotumika kwenye shughuli nzima

Hapa ndipo akili za mwafrika zina tatizo!!yaani mwananchi kutaka kuulizia matumizi ya kodi yake ni kosa? Pesa iliyotumika kwenye shughuri yote ya mazishi ni kodi yetu, na lazima (kama serikali ni ya uwazi gharama ijulikane)kwani haya mambo ya kufanya mambo kwa siri ndio huleta shida, mbona mambo haya kwa wazungu huwa yanakuwa wazi tu??sio kwa nia mbaya lakini inasaidia kuwa wahusika wanajua kabisa kuwa baada ya shughuri matumizi ya pesa hizo yataulizwa.
Mazishi hata hayajafanyika mpo busy na kuuliza matumizi ya Kodi mmeweka sana mbele hela kuliko utu kodi zipo tuu toka enzi za Mitume wao ndio wanaotumia unadhani ukiletewa taarifa tofauti na matumizi utapata wapi sehemu ya kuhoji au mnaandika tuu bila hata kuumiza kichwa.
 
Nazan tusipate shida sana, zle pesa zoote alizokuwa akibana bajeti kwenye matukio mbalombali ya kitaifa ndzo zlizo fanya kazi.
 
Wakikwambia wewe utafaidi nini? Wasipozitumia msibani unadhani utapewa wewe?

Watu wote viongozi walokufaga ushawahi kuuliza gharama walizotumia msibani? Au kisa magufuli?

Hivi ni chuki au ni nini? Kwahiyo ulitaka raisi wa nchi azikwe kienyeji enyeji? Ishiiiiiiiy.
Mkuu tuheshimiane tafadhali, hii ni Pesa yangu ya kodi (kama wewe haulipi that's ur problem) nina haki ya kuhoji na serikali kunijibu tatizo liko wapi?
 
Mazishi hata hayajafanyika mpo busy na kuuliza matumizi ya Kodi mmeweka sana mbele hela kuliko utu kodi zipo tuu toka enzi za Mitume wao ndio wanaotumia unadhani ukiletewa taarifa tofauti na matumizi utapata wapi sehemu ya kuhoji au mnaandika tuu bila hata kuumiza kichwa...
Kwa mawazo haya viongozi wa ki afrika tutazidi kuwalaumu sana! Kwani kwenye ripoti za CAG, lazima itaainishwa tu gharama zote za mazishi labda kama zimetoka kwenye ile vote, eti kodi zipo toka enzi za mitume so what?! Ndio yale yale watu kuhoji deni la taifa waliambiwa hayawahusu!
 
Kwa mawazo haya viongozi wa ki afrika tutazidi kuwalaumu sana!!kwani kwenye ripoti za CAG, lazima itaainishwa tu gharama zote za mazishi labda kama zimetoka kwenye ile vote...., eti kodi zipo toka enzi za mitume so what?!!ndio yale yale watu kuhoji deni la taifa waliambiwa hayawahusu!!!
Unaongea theory kwa kuwa hakuna unachojua CAG anatoa report kutokana na matakwa ya wanasiasa Mzee ludovick Uto na Prof Assad wamefanya kazi na kuipa thamani ofisi zao sio huyu kateuliwa matumizi ya serikali hayaidhinishwi bungeni unazungumzia report ya mkaguzi kweli huko Tanzania ni shida na wewe utalalamika umekosa ajira kwa vitu vipo wazi ila hakuna unachojua.
 
Kwa wale tuliofuatilia mazishi ya mpendwa wetu Marehemu John Joseph Pombe Magufuli tuliona kuna kitu hakipo sawa katika gharama zilizotumika kwenye msiba huu mkubwa kwa taifa. Mazishi haya ambayo kimsingi yaliratibiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kulikosekana uwazi kwenye gharama zilizotumika.

Kwakuwa mpendwa wetu Hayati John Joseph Pombe Magufuli alikuwa muumini wa kupinga ufisadi tunataka uwazi juu ya gharama zilizotumika ili wafuasi wake tuwe uhakika kwamba mpendwa wetu hakuzikwa kifisadi na kumuweka kwenye hali mbaya huko aliko. Mamlaka husika zichukue hatua juu ya jambo hili.
 
Tafuteni kazi za kufanya, mtajikuta mnazeeka mnakufa mnawaachia urithi watoto na wajukuu akaunti za mitandao wenzenu wakiacha akaunti za benki zimenona. Ukishajua gharama za mazishi ya JPM zitakusaidia nini!?.. uliwahi kutangaziwa ilitengwa kiasi gani ili Kama ikizidi useme imezidi?.. hata ukiambiwa ni bilioni 10 au 20 utafanyaje!?.. kuwa bize na maisha yako na waliokuzunguka. Achana na yasiyokuhusu.
 
Kwa wale tuliofuatilia mazishi ya mpendwa wetu Marehemu John Joseph Pombe Magufuli tuliona kuna kitu hakipo sawa katika gharama zilizotumika kwenye msiba huu mkubwa kwa taifa. Mazishi haya ambayo kimsingi yaliratibiwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa kulikosekana uwazi kwenye gharama zilizotumika.

Kwakuwa mpendwa wetu Hayati John Joseph Pombe Magufuli alikuwa muumini wa kupinga ufisadi tunataka uwazi juu ya gharama zilizotumika ili wafuasi wake tuwe uhakika kwamba mpendwa wetu hakuzikwa kifisadi na kumuweka kwenye hali mbaya huko aliko. Mamlaka husika zichukue hatua juu ya jambo hili.

Hakuna haja, maana kufa kufaana
 
Unasikitisha sana brother.

Lakini niseme tu kwamba kama kunawatu 'walipiga' hela iliyotengwa kwa lengo la kufanikisha shughuli flani za mazishi ya hayati JPM dhambi hiyo ipo juu yao.
 
Back
Top Bottom