Baada ya Mbowe kugeuka na kuwa kama kina Shibuda, John Cheyo na Mrema ni upi mustakbali wa siasa za upinzani Tanzania?

70% ya watanzania hawajui kiingereza lakini utakuta na wao wapo kwenye mjadala wa kusema MAGUFULI hajui Kingereza.
Na yeye magufuli alikuwa ni mmoja kwenye hiyo 70% ya wasiojua kiingereza. Lazima tusene kwa vile alidai ana PhD. Unapataje PhD na English unaongea kama vile bata antembea huku anakunya. Eti "The people was daying in ze rake"
 
Mkuu utapoteza muda wako, huyo jamaa hajui tumetoka wapi tupo wapi na tunakwenda katika nyanja za kisasa na kimaendeleo ya kiuchumi.
 
Mkuu wewe ndio hukujua walichokuwa wanafanya kwa sababu furaha yako kubwa sana. Wenzio walikuwa wamezama katika MAOMBI mazito ambayo yamekufichua wewe kutoka huko kwenye mema ya Nchi, ni kama vile kiroboto kwenye ngozi ya ng"ombe,
Maombi tena! Yale yale ya kuondoa corona na maombi.
Mambo ya imani ni ngumu sana kujadili hapa maana ni masuala ya kiimani.
 
Mkuu yaani Mama kama atatuletea ile Katiba ya mapendekezo ya Mzee Warioba, mimi na ukoo wangu wote wenye jumla ya watu zaidi ya 100 tutampa kura zetu.
 
Jitafakari utanzania wako. Naona wewe unapenda siasa za mikwaruzano, matusi na kila aina ya vurugu kuliko siasa za kukosoana kistaarabu na kusahihishana. Kuna uwezekano wewe siyo Mtanzania mzalendo.
 
Jina lako hapo linaonyesha usharishari. Ushari katika siasa hapa Tanzania hauna nafasi. Anza kwa kubadilisha na hilo jina lako.
 
Awali nilikuweka katika kundi la member wale genius lakini nimezijutia fikra zangu za awali. Sijasoma na kumaliza hoja Yako maana ni wastage of time kwani Haina mashiko na ni upotoshaji.
Mwaka 2016 Hadi 2021 nchi hii ilipita katika kipindi kigumu sana pengine kuliko huko Somalia au DRC na ndio maana hata katika zile tafiti za mataifa yasiyo na furaha duniani Tanzania ilikuwa katika nafasi za juu kabisa pamoja na kuwa nchi haikuwa na vita.
Watu wameuwawa, wameteswa,wamefilisiwa, wamefinguliwa kesi za uongo na ndugu zetu wengi wamepotea kama mbuzi anavyopotea zizini na hatujui lakufanya au kusema.
Hali hiyo ili kuirekebisha Kwa serikali isifanye hayo Ina njia mbili kuu nazo ni;
1. KUINGIA VITANI ILI KUIONDOA SERIKALI
2. KUTENGENEZA MARIDHIANO NA MUAFAKA ILI MKUBALIANE KIUTU.

Hatua hiyo ya pili ndio Mbowe na Samia waliongoza vyama vyao kuweza kukubaliana na Sasa hatua zinachukuliwa Kwa mafanikio makubwa.

Hivi mnaopinga ujasiri huu wa vyama hivi mnataka kutuambia mnapenda hiyo njia nyingine yaani VITA? hivi mnavijua vita au mnavisikia? Mmewahi kutembelea nchi ambazo ziko VITANI mkaona maisha ya kina mama na watoto wanavyo ishi. VITANI sio jambo la ajabu familia Yako kuvamiwa na mkeo na mabinti zako kubakwa Kwa zamu ukishuhudia jee mwapenda hayo? Kupoteana na ndugu zako sio story huko jee na Hilo?
Hapa kwetu hata kuandamana bei ya vyakula ikipanda hatuwezi twaweza kumuondoa nduli kama Magu?
Tuipiganie Katiba mpya iliyo Bora na Tume huru ya uchaguzi ili ifike tunaishi na kufanya mambo kama Ghana au nchi za ulaya yaani Leo chama hiki kinapata madaraka kihalali kesho kikiharibu kinapigwa chino kinaingia kingine bila ngumi wala panga.
Mandela na De Klerk walipewa tuzo ya NOBEL Kwa haya wanayofanya Samia na Mbowe, nasi Kuna siku tutawapa tuzo ya kuu kuliko zote wakifanikisha.
 
Maombi tena! Yale yale ya kuondoa corona na maombi.
Mambo ya imani ni ngumu sana kujadili hapa maana ni masuala ya kiimani.
Maombi ni muhimili mwingine katika maisha ya mwanadamu. Leo wewe ukiteuliwa (kwa elimu yako ya Siasa za TZ)DC utaapishwa na wewe utaomba (....... Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie) hayo mayo ni maombi Mkuu
 
Wewe huu muda unaopoteza huku si ukalime?
 
Tangu nianze kufuatilia michango yako humu, sijawahi kuona ukimbeza Mbowe wala Chadema.

Hatua hii ya usiri uliopo katika maridhiano unakunyima amani mkuu?
 
Kama unaleta mambo ya kipenda roho hula nyama mbichi, huwezi kuona siasa za "kuunga mkono juhudi" zinazoendeshwa kwa ujanja mkubwa tofauti na ilivyokuwa kipindi cha mwendazake.
 
Ni bora wapige Dili tu kwa sababu Watanzania ukiwaambia tokeni mabarabarani tudai haki zetu hutomuona hata mtu mmoja barabarani !! Mange Kimambi analijua hilo !!
 
Kama unaleta mambo ya kipenda roho hula nyama mbichi, huwezi kuona siasa za "kuunga mkono juhudi" zinazoendeshwa kwa ujanja mkubwa tofauti na ilivyokuwa kipindi cha mwendazake.
OK Sasa njia Gani Bora, tuingie VITANI tuwatoe CCM?
 
Tangu nianze kufuatilia michango yako humu, sijawahi kuona ukimbeza Mbowe wala Chadema.

Hatua hii ya usiri uliopo katika maridhiano unakunyima amani mkuu?

Sina haja ya kumbeza maana natambua mchango wake kwa CDM, ila kwa sasa hastahili kuendelea kuwa mwenyekiti wa CDM. CDM naikubali niibeze ili ,nikufurahishe ww?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…