Baada ya Mbowe kugeuka na kuwa kama kina Shibuda, John Cheyo na Mrema ni upi mustakbali wa siasa za upinzani Tanzania?

Naona Tindo akili zako zinaanza kurudi sikutegemea kama utaandika hiki nikadhani labda account yako imekuwa hacked
 
Kama huwezi kuyaona maendeleo kwa kuwa wewe ni KIPOFU, hatuna msaada na wewe
Kwa hii miaka 60 unajisifu kwa maendeleo gani yenye kuendana na huo umri? Kama sasa wewe unaona kuna maendeleo najiuliza tafsiri ya kutokuwa na maendeleo kwa upande wako ni ipi?
 
Ina maana kuwa kweli huoni tofauti kati ya agenda ya kina Shibuda na hii ya Mbowe....!!?
 
Swali la msingi sana.Aeleze alivyotaka CDM ingefanya siasa za aina ipi?Je,wapigane ngumi?Waue watu?Wafanye ugaidi?Wapindue serikali?Watukane asubuhi ya leo hadi keshoye kwa mtiririko?Au ana chama chake mbadala akilete kifanye atakacho?
Mrema na lipumba walipofanya hivyo mbona mliwatukana?
 
Chadema hawajawahi kuandamana kwa maslahi ya wananchi ndio hakupata sapoti kubwa ya watu Chadema inaandamana kwa mlengo wa maslahi ya chama chao ngoja nikuulize umekuona Chadema imeandamana kwasababu ya vitu kupanda bei? Missile of the Nation Hili swali kwanini Chadema hawapendagi kulijibu
 
Mrema na lipumba walipokuwa wakifanya hayo mbona mliwatukana?
 
Upinzani siyo kupinga kila kitu hata kiwe cha maana na kutukana.
 
Sio rahisi hivyo!!Nyie wafuasi wa MEKO tunajua hiki kinachoendelea kinawauma sana!!mlitaka ziendelee zile siasa za kishenzi tu!!kwani mlikuwa mnafaidika nazo!!wewe una uchungu na CDM kuliko mbowe??
Huyo unayemponda ni Chadema mwenzako Tena ana kadi kabisa ya hicho chama hii ndio shida yakufikiri kila anayeponda maridhiano ni shabiki wa Magu
 
NI lini chadema wamerusiwa kuandamana hapa Tanzania
 
Mkuu unajitoa ufahamu ukumbuki kampeni ya UKUTA?
Ilifanikiwa kwani???? mbona haikufanikiwa
Niambie ni lini chadema wamerusiwa kuandamana nchi hii ya Tanzania, majaribio yote ya maandamano yalikuwa yanazuiwa na polisi

Ni uongo wa wazi kusema chadema walishawah kuandamana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…