Ni Hatari sana kama tutakua na wapinzani wanaofanya siasa za Kistarabu Kwa Rushwa.
Kumbe Bila Rushwa Mama angetukanwa majukwani!
Wanasiasa ni hatari sana .
Lakini pia watanzania tufahamu fika kuwa hakuna Mwanasiasa Mwenye Tamaa ya Fedha na utajiri ambaye ni mtetezi Wa Wanyonge .Never on earth!!
Atakayewatoa watanzania maskini na kuwapeleka mbele Kwa Sasa ni ama Bashiru Ally, Tundu Lisu, Polepole, John Heche ,Job Ndugai na Dr. Slaa. Hawa watu angalau Hawana Tamaa ya fedha.
Uchaguzi unakaribia Kwa Siasa hizi za Mbowe atairudisha CCM ya wanasiasa wenye mdomo na úlimi unaodanganya Kwa lugha Nzuri na tutaendelea kuibiwa mpaka Atakaporudi Masihi Issah Bin Maryam Mwenye ufalme .
Chadema Kuna kitu hawajifunzi. Utawala ni Wa Mungu . Mungu alimpitisha Magufuli Ili watanzania waamke Kama walivyoamka . Magufuli ameacha roho ya kuhoji na kupigania Mali za umma.
Magufuli ameacha roho ya kukataa miradi Feki . Magufuli ameacha roho ya kukataa ghilba za Wazungu na Mawakala wao. Magufuli ameacha roho ya kutetea wanyonge ambao ni wengi na NDIO wanaoumizwa na umaskini,tozo kubwa,Kodi KUBWA,elimu mbovu, matumizi makubwa ya watawala, wizi, uhalifu , mauaji ya watu kutokana na maisha magumu, ushoga, utekaji Wa Watoto wasio na hatia, Imani za kishirikina , Imani potofu za kuuza mafuta ,mfumuko Wa Bei, ukosefu Wa Ajira n.k. Magufuli alibeba Maono ya Mzee Karume na Nyerere Kwa pamoja ,alikwenda Mbele ZAIDI katika kukupigania Taifa hili wakati huu ambapo Kuna pengo kubwa sana kati ya maskini na matajiri KWENYE nchi yenye utajiri mkubwa Wa asili ulioletwa na Mwenyezi Mungu.Roho aliyokuwa ameibeba Magufuli ndiyo roho ya uhuru Wa nchi hii. Hakuna MTU atakayeiua HIYO roho. HIYO ndiyo roho inayolinda uhuru,Rasilimali na utu Wa Watanzania .
Mbowe asijidanganye Kwa Siasa zake Hata pakiwa na Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi Chadema ikifanana na CCM kamwe hawawezi kushinda .
Magufuli ndiye aliyeleta Siasa za Tofauti NDANI ya CCM na ndiye aliyewaamsha wanyonge kuwakataa wapigaji .
Mbowe akiwa amelewa Kama Jana ashauriwe asipande majukwaani kwani anakiua chama . MTU mwenye Busara ya kutosha huwezi kupanda jukwaani KWENYE Ardhi ya Wasukuma ukaanza kudhalilisha na kumponda Kiongozi Mkubwa aliyewaletea Heshima kubwa NDANI na Nje ya nchi . Wasukuma wengi walionufaika na utawala Wa awamu ya Tano katika miradi ya kimkakati lakini pia kisiasa na kiuchumi . Daraja kubwa KULE Busisi ni Alama kubwa ya Shujaa Wa kisukuma JPM . Leo Mbowe alivyo Wa ajabu anashindwa kutumia busara na kujiepusha na hasira na ghadhabu za watu Wa Ukanda Wa Ziwa ambao wanamkubuka Magufuli Kwa mema Mengi kuliko mabaya machache ya kuzuia mikutano ya Hadhara na uchaguzi.
Kuna mambo Mengi sana yangekwama Kwa muda mrefu Bila Magufuli kuletwa hapa Duniani .Kuna mambo Mengi sana yamefanyika Kwa sababu ya msimamo Wa Magufuli.
Mbowe Acha Siasa za kihuni watanzania wanataka será mbadala na SIO kejeli