Baada ya Mbowe kuiponda awamu ya 5, maoni ya wananchi ambao ni wapiga kura kwenye Instagram page ya JF yanashtua

Baada ya Mbowe kuiponda awamu ya 5, maoni ya wananchi ambao ni wapiga kura kwenye Instagram page ya JF yanashtua

UZI WA SUKUMA GANG HUU🤣🤣🤣🤣 Sukuma gang kuleni mlichokipanda na muwe wavumilivu tu kwani hakuna namna. Haya ni matokeo ya mliyoyapanda wenyewe tena kwa furaha kubwa huku mkipongezana
 
Bhagosha walinufaika sana nan awamu Ile! Hawakuona madhila yaliyowapata wengineLazima wampondeMbowe.

Ameeleza ukweli na wala hajakosea. Nashangaa Wana cDm wanamponda!
Huu ni muda wa kumponda asiyekuwepo kwa sasa? Kiufupi wamechemka!
 
Hakuna watu wenye akili instagram,

watu walohudhuria mkutano mwanza ni kielelezo kuwa mbowe ni mwamba na Magufuli alikuwa wa hovyo, watu hawakumshobokea zaid ya chawa wake
ACHENI kujipa matumaini ya kijinga.

Ni kukosa akili Kwenda kumponda Magufuli KWENYE himaya yake wakati ameshafariki na ameacha Alama kubwa kuliko mikutano ya Hadhara.

Kila MTU anaona kuwa NI GENGE LA AKINA MAROPE NA WAPIGAJI WENGINE WALIOKUA WANASHIRIKIANA NA Mbowe kumtukana Magufuli Kwa ajili ya kuziba mianya Yao ya Wizi madili .

Hakuna Mtanzania asiyejua KAZI kubwa aliyoifanya Magufuli.
Mbowe Jana amekosea sana watanzania hawahitaji Wanasiasa legelege.
Nchi hii inaibiwa Kwa Kasi ya ajabu. Viongozi hawakai maofisini Wala hawana huruma Tena na mali za umma. Kila Mkuu Wa Idara anataka kutajirika haraka haraka mana hakuna MTU Wa kumzuia. Nchi Gani inakua hivyo?
Kumbuka hakuna Katiba inayowabana wezi na itakapoundwa haitashughulika na yaliyopota . Watu wataiba sana na wataleta Katiba ya kulinda maslahi Yao. Mwenye Mali ndiye atakayetunga Sheria na Katiba. Nchi hii tumeepihwa na kitu kizito.
Miradi mingi kwa maelfu inafanyikia KWENYE makongamano. Watu wanapiga mabilioni Kwa kuanzisha mradi Wa mamilioni.
Chadema ilipata wanachama wengi kwa msimamo Wa Dr. Slaa Wa kupambana na Mafisadi Bila woga na hakujali maisha yake yalipokua hatarini.

Bora aje Tundu Lisu Mbowe amepoteza dirá kabisa. Hana uchungu na umaskini Wa Watanzania wenzake unaosababishwa na CCM ya wapigaji.
Mbowe Hana Tofauti na wale wanaopewa pesa KUFANYA vitendo vya kigaidi Bila kujali madhara Kwa WENGINE.
 
Kuna utofauti wowote wale wa awamu ya tano KUUNGA MKONO JUHUDI na huyu chapombe?

Mwenyekiti kufanya kazi za Sofia Mjema kuongelea CCM na serikali yake.

Tofauti ni yeye kuhamia rasmi CCM. Ila kwa sasa yeye na chama chake pamoja na ACT wazalendo wanaifanyia kazi nzuri sana awamu ya sita (CCM) na siyo wananchi.
 
Ni Hatari sana kama tutakua na wapinzani wanaofanya siasa za Kistarabu Kwa Rushwa.
Kumbe Bila Rushwa Mama angetukanwa majukwani!

Wanasiasa ni hatari sana .

Lakini pia watanzania tufahamu fika kuwa hakuna Mwanasiasa Mwenye Tamaa ya Fedha na utajiri ambaye ni mtetezi Wa Wanyonge .Never on earth!!

Atakayewatoa watanzania maskini na kuwapeleka mbele Kwa Sasa ni ama Bashiru Ally, Tundu Lisu, Polepole, John Heche ,Job Ndugai na Dr. Slaa. Hawa watu angalau Hawana Tamaa ya fedha.

Uchaguzi unakaribia Kwa Siasa hizi za Mbowe atairudisha CCM ya wanasiasa wenye mdomo na úlimi unaodanganya Kwa lugha Nzuri na tutaendelea kuibiwa mpaka Atakaporudi Masihi Issah Bin Maryam Mwenye ufalme .

Chadema Kuna kitu hawajifunzi. Utawala ni Wa Mungu . Mungu alimpitisha Magufuli Ili watanzania waamke Kama walivyoamka . Magufuli ameacha roho ya kuhoji na kupigania Mali za umma.
Magufuli ameacha roho ya kukataa miradi Feki . Magufuli ameacha roho ya kukataa ghilba za Wazungu na Mawakala wao. Magufuli ameacha roho ya kutetea wanyonge ambao ni wengi na NDIO wanaoumizwa na umaskini,tozo kubwa,Kodi KUBWA,elimu mbovu, matumizi makubwa ya watawala, wizi, uhalifu , mauaji ya watu kutokana na maisha magumu, ushoga, utekaji Wa Watoto wasio na hatia, Imani za kishirikina , Imani potofu za kuuza mafuta ,mfumuko Wa Bei, ukosefu Wa Ajira n.k. Magufuli alibeba Maono ya Mzee Karume na Nyerere Kwa pamoja ,alikwenda Mbele ZAIDI katika kukupigania Taifa hili wakati huu ambapo Kuna pengo kubwa sana kati ya maskini na matajiri KWENYE nchi yenye utajiri mkubwa Wa asili ulioletwa na Mwenyezi Mungu.Roho aliyokuwa ameibeba Magufuli ndiyo roho ya uhuru Wa nchi hii. Hakuna MTU atakayeiua HIYO roho. HIYO ndiyo roho inayolinda uhuru,Rasilimali na utu Wa Watanzania .

Mbowe asijidanganye Kwa Siasa zake Hata pakiwa na Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi Chadema ikifanana na CCM kamwe hawawezi kushinda .
Magufuli ndiye aliyeleta Siasa za Tofauti NDANI ya CCM na ndiye aliyewaamsha wanyonge kuwakataa wapigaji .
Mbowe akiwa amelewa Kama Jana ashauriwe asipande majukwaani kwani anakiua chama . MTU mwenye Busara ya kutosha huwezi kupanda jukwaani KWENYE Ardhi ya Wasukuma ukaanza kudhalilisha na kumponda Kiongozi Mkubwa aliyewaletea Heshima kubwa NDANI na Nje ya nchi . Wasukuma wengi walionufaika na utawala Wa awamu ya Tano katika miradi ya kimkakati lakini pia kisiasa na kiuchumi . Daraja kubwa KULE Busisi ni Alama kubwa ya Shujaa Wa kisukuma JPM . Leo Mbowe alivyo Wa ajabu anashindwa kutumia busara na kujiepusha na hasira na ghadhabu za watu Wa Ukanda Wa Ziwa ambao wanamkubuka Magufuli Kwa mema Mengi kuliko mabaya machache ya kuzuia mikutano ya Hadhara na uchaguzi.

Kuna mambo Mengi sana yangekwama Kwa muda mrefu Bila Magufuli kuletwa hapa Duniani .Kuna mambo Mengi sana yamefanyika Kwa sababu ya msimamo Wa Magufuli.

Mbowe Acha Siasa za kihuni watanzania wanataka será mbadala na SIO kejeli

Umetokea jela (miezi minane ndani).

Siku hiyo hiyo kituo cha Kwanza ikulu. Toka siku hiyo ni kutetea awamu ya sita. Mtu aliyekufunga kwa miezi minane. Mbowe hana muda wa kuongelea matatizo ya Wananchi.

Naona watu wenye uwezo wa kutetea maslahi ya Watanzania labda ni John Heche, Dr Slaa, Dr Bashiru Ally, Lukuvi, Mpina definitely Polepole.
 
ACHENI kujipa matumaini ya kijinga.

Ni kukosa akili Kwenda kumponda Magufuli KWENYE himaya yake wakati ameshafariki na ameacha Alama kubwa kuliko mikutano ya Hadhara.

Kila MTU anaona kuwa NI GENGE LA AKINA MAROPE NA WAPIGAJI WENGINE WALIOKUA WANASHIRIKIANA NA Mbowe kumtukana Magufuli Kwa ajili ya kuziba mianya Yao ya Wizi madili .

Hakuna Mtanzania asiyejua KAZI kubwa aliyoifanya Magufuli.
Mbowe Jana amekosea sana watanzania hawahitaji Wanasiasa legelege.
Nchi hii inaibiwa Kwa Kasi ya ajabu. Viongozi hawakai maofisini Wala hawana huruma Tena na mali za umma. Kila Mkuu Wa Idara anataka kutajirika haraka haraka mana hakuna MTU Wa kumzuia. Nchi Gani inakua hivyo?
Kumbuka hakuna Katiba inayowabana wezi na itakapoundwa haitashughulika na yaliyopota . Watu wataiba sana na wataleta Katiba ya kulinda maslahi Yao. Mwenye Mali ndiye atakayetunga Sheria na Katiba. Nchi hii tumeepihwa na kitu kizito.
Miradi mingi kwa maelfu inafanyikia KWENYE makongamano. Watu wanapiga mabilioni Kwa kuanzisha mradi Wa mamilioni.
Chadema ilipata wanachama wengi kwa msimamo Wa Dr. Slaa Wa kupambana na Mafisadi Bila woga na hakujali maisha yake yalipokua hatarini.

Bora aje Tundu Lisu Mbowe amepoteza dirá kabisa. Hana uchungu na umaskini Wa Watanzania wenzake unaosababishwa na CCM ya wapigaji.
Mbowe Hana Tofauti na wale wanaopewa pesa KUFANYA vitendo vya kigaidi Bila kujali madhara Kwa WENGINE.

Lissu angeweza kuwa mwanasiasa mzuri angeondoa haya mapungufu.

Tatizo lake he is too emotional, Hana staha kwenye kauli zake na ana kejeli, dharau nyingi sana. No really presidential material ni mwanaharakati.

Pia anawababaikia sana wazungu badala ya kuangalia maslahi ya Tanzania Kwanza kwenye kila kitu.
 
Mama Samia ni genious kawapa mafuta wapinzani ili wajikaange wenyewe
Mama hana roho ya kishetani kama lile jiwe. Mama ni muhumini wa haki na na ninauhakika atakapo ondoka, atatuachia watz kitu kikubwa sana KATIBA MPYA NA BORA KWA KILA MTZ. kitu ambacho kitafanya akumbukwe/atajwe kwa upendo mkubwa milele na milele
 
Hana haki yeyote Yeye anagawa asali kwa wengine anaohofika watampinga! Hana lolote wewe mwenyewe unajua hilo ila kwa vile unapenda kubwabwaja sawa!
 
Hana haki yeyote Yeye anagawa asali kwa wengine anaohofika watampinga! Hana lolote wewe mwenyewe unajua hilo ila kwa vile unapenda kubwabwaja sawa!
Jiwe hakuwa anagawa asali? Ninachojua mama anagawa asali kwa nia njema

Jiwe lilikuwa linagawa asali kwa wauwaji/wasiojulikana
 
Jiwe hakuwa anagawa asali? Ninachojua mama anagawa asali kwa nia njema

Jiwe lilikuwa linagawa asali kwa wauaji/wasiojulikana
Wewe jua tu huyo mwenyekiti wako Makengeza kashalamba asali! Hakuna hoja za wananchi ni kulalamika tu Magufuli Magufuli!
Wananchi wanatarajia kusikia anazungumzia kero badala yake kavya mikvant mpuuzi yule!
 
Pole sana sukuma gang.
 
Mama hana roho ya kishetani kama lile jiwe. Mama ni muhumini wa haki na na ninauhakika atakapo ondoka, atatuachia watz kitu kikubwa sana KATIBA MPYA NA BORA KWA KILA MTZ. kitu ambacho kitafanya akumbukwe/atajwe kwa upendo mkubwa milele na milele
Mimi ninafikiri tumeweka saana imani kwenye katiba mpya. Katiba mpya ilishindikana mara ya kwanza kwa sababu ya kuchakaliwa na CCM. Ile iliyochakachaliwa ilikuwa mbovu kuliko iliyopo sasa. Sasa, sijui ni kitu gani kinawafanya watuu waamini sana kwenye katiba mpya itakayopitishwa na CCM. Rasimu ya katiba ya Warioba ilitupiliwa mbali, na ikaja rasimu mbovu kuliko zote. Rasimu inapitishwa na makada wa CCM, sasa unafikiri watajiwekea kitanzi?

Mbowe badala ya kutaka kuiondoa CCM kwenye madaraka anang'ang'ania kumtukana marehemu. Tangu lini katika mila za kiafrika marehemu akatukanwa. Hata kama marehemu alikuwa jambazi, utasikia watu wanampa au wanazitaji zile sifa zake nzuri. Mzuri hakosi kasoro, na mbaya hakosi angalao kizuri kimoja. Mbowe kumng'ang'ania marehemu anaonyesha ni mtu wa visasi. Lakini ajue, na yeye pia anahusika na vifo ndani ya CHADEMA, kwa hiyo asjione msafi. Watu wa Tarime bado wanamlilia shujaa wao Chacha Wangwe, aliyeuawa na Mbowe pale tu alipoonyesha nia ya kugombea uenyekiti wa CHADEMA.

Mama Samia kisha mfix Mbowe kwa mbinu zilezile za Magufuli. Magufuli aliuua upinzani kwa kunyofoa au kuwarubuni wabunge wao kwa fedha. Na sasa Mbowe karubuniwa kiani kwa pesa na kupewa masharti ya kutosema chochote kibaya kuhusu serkali ya CCM. Kapewa kibarua cha kumtukana marehemu huku Samia akijuwa dhahiri kuwa kumtukana marehemu ni kujipiga risasi mguuni.
 
Mpaka ulewe chakari ili kumponda inaonekana hata yeye haamini anayoyasema.

Tanzania ina matatizo kibao kama mfumuko wa bei, ajira, katiba mpya, Loliondo inauzwa, wanyama wa maliaasili wanasafirishwa, rushwa, tozo, Kodi, mazingira mabovu ya biashara. Yeye mbowe yote haya hayamhusu.

Kazi yake kwa sasa baada ya kulamba asali ni kuwa chawa rasmi wa Samia na kupambana na awamu ya tano.

Analipiwa kila kitu hadi trip za marekani.

Itisha nawe mkutano uyaseme hayo
 
Back
Top Bottom