Pre GE2025 Baada ya Mbowe kutetea uenyekiti wake, masikini Tundu Lissu, kwishney! Je, atabaki ama atatimka? Lissu Cool down, usiitishe Press kumjibu Mbowe!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
mkuu Pascal Mayalla natangaza maslah kuwa mimi ni mfuatiliaji mzur wa maandiko yako na ninabarikiwa sana kwa uchambuzi wako na hakika kwa habari za uchambuzi wa kisiasa nimekuweka nafasi ya juu zaidi huku JF tangu enzi za kutuwekea bandiko lililokuwa linabashiri uwezekano wa mgombea na mshindi wa uraisi namba 10 na hakika ikawa. si hilo tu na mengine mengi yanatoa mwongozo na hatimae inakuwa sawa. na hilo; kutoka kwako na wachambuzi wengi wengi lukuki wa humu jf yanaifanya jf kuwa mhimili muhimu sana kwangu kuuamini kuliko chanzo chochote.

ikumbukwe tetesi za nani ataibuka mshindi katika chama hiki zilianza humu na pia ikaandaliwa kura ya maoni ya awali kabisa. watu wakakejeli ni ushabiki wa mtandaoni. mimi niliamini matokeo ya humu ndiyo yameshamaliza uchaguzi mengine ni kuweka mhuri tu.

tatizo kidogo la 'Nsumba Ntale' Pascal ni; kuna nyakati unajisahau unajikweza kudhani fikra zako ndizo ziko juu ya wengine na unajiweka kwenye nafasi ya kutodhaniwa una nafasi ya kufanya makosa kama ilivyo sifa ya binadamu. hili pia kwangu sio tatizo maana u mwepesi wa kujikosoa na kukiri hadharani kuwa ulikengeuka ktk jambo fulani na hauachi kutoa pongezi kwa mhusika aliyethibitisha bila chembe ya shaka kuwa amekukosoa kwa haki (to prove wrong) na hili limenifanya nikukubali na kukupenda zaidi.

nakukumbusha tena nje na mada ya uchaguzi, rudi nyuma enzi za utabiri wa marehemu sheikh Yahya Hussein (wewe ukikuwepo physically siku anatamka juu ya uwezekano wa kutawala jinsi ya 'ke') fuatilia tena records hasa waandishi mlipoanza kubisha na kutia shaka kabla na baada ya utawala wa mwanamke. kuna jambo lilisemwa.
 
o
Asante sana kwa yote, naomba links ya utabiri huo wa Sheikh Yahya.
P
 
Hili lilikanushwa na jamii check.
P
 
Unajisikiaje sasa?
 
Kwa upande wangu mimi ni no comment kwani kiwango cha unafiki nchini kinatisha! Natumaini tu kwamba matokeo ya huu uchaguzi, yatawafungua macho vipofu wa kisiasa wasiojua kuwa hawajui waliotamalaki nchini.
 
Mkuu Pascal Mayalla naomba kusikia maoni yako baada matokeo haya,
 
CCM mtajinyea mwaka huu
Chuma ndio hicho kimeshika hatamu

Tundu Lissu atawaua Kwa presha
Na bado
Ndio kwanza ametangazwa..
 
Nakiri hapa I was wrong!, nili mu under estimates TAL!.
Sasa nimekubali!
One down, two to go!.
October 2025 ule mbuyu unakwenda chini!.
Usikute Lissu ni mpango wa Mungu kwa Tanzania post '25.
Mwacheni Mungu aitwe Mungu!.
Hongera Sana Tundu Lissu!.
P
Nimekuwa nikichungulia nyuzi uziandikazi nikitaraji labda kuna kitu utaandika kuhusiana na hili lakini wapi. Sasa najua wewe ni kati ya mliobadilishiwa password msione mpango unaoendelea baada ya mwelekeo kubadilishwa, mmeachwa muendelee na ule mpango wa mazoea.
Kama imewezekana kwa gaidi kutoka jela na moja kwa moja akaelekea Ikulu, basi zama za upinzani hawana uwezo wa kuongoza ni ama zimepita au ilikuwa ni story tu.
Angalia vizuri, kuna mahala wenzako wameku sideline, na hii si habari njema, haujachelewa.
Ila kuanzia sasa, uwe makini sana na sauti yoyote ile "from within".
 
Brother tunaenda kwenye siasa za ushindani ccm tunaenda kupoteza wabunge %kubwa sana... hii safi
 
Nakiri hapa I was wrong!, nili mu under estimates TAL!.
Sasa nimekubali!
One down, two to go!.
October 2025 ule mbuyu unakwenda chini!.
Usikute Lissu ni mpango wa Mungu kwa Tanzania post '25.
Mwacheni Mungu aitwe Mungu!.
Hongera Sana Tundu Lissu!.
Inawapa tabu sana CCM,
na mbaya zaidi hili jambo limetokea CCM ikiwa na 100% kuwa Mbowe atashinda na hivyo business itakuwa as usual kwenye 2025 General Election, Kwa kweli jambo hili linawapasua kichwa kwamba how they could change the game na washawatangaza wagombea wa genreal Election 2025!
 
Nadhani sasa utaamini kuwa umezeeka, ule utabiri wako kuhusu ni yeye, aliyechaguliwa sijui na yeye hakuna kitu, na huu wa Lisu nao hakuna kitu.
 
Mzeee mzima husomi hata alama za nyakati huna hata hekima bure kabisa Chawa ww
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…