Uchaguzi 2020 Baada ya Membe na Maalim Sharif kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, Msajili aibuka atia nia ya kukifutia usajili ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Baada ya Membe na Maalim Sharif kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, Msajili aibuka atia nia ya kukifutia usajili ACT Wazalendo

Siamini hiyo michezo ya msajili, hizo ni mbinu zile zile alizosema Mzee Tupatupa jana, wanajaribu kukikuza hicho chama kionekane threat, hakuna lolote hapo.

Membe hawezi kuwa threat kwa CCM hata siku moja, Lissu is.
ABSOLUTELY.
 
Magufuli anaogopa nini?Mbona sioni wa kumshinda unless wapinzani waungane.
 
Why wanahaha?
Hofu yao kubwa ni kwa Maalim Seif huko Zanzibar na ujio wa Membe ni kama tu kutia acid kwenye kidonda.

Kwa urefu wa hii barua,eleweni wamekusudia kuwapa adhabu, na bila shaka kuwafutia au kusitisha usajili wa chama chenu; hivyo, ikibidi muanzee kujiandaa kwenda Mahakamani na kama sheria inaruhusu.

Ikiwezekana,fungueni kesi kuzuia uchaguzi mkuu usifanyike mpake shauri lenu (iwapo mtafutiwa au kusitishiwa usajili na nyie kwenda mahakamani) liishe au vinginevyo muungane na CHADEMA kwenye uchaguzi ingawa hata CHADEMA nao hawako salama kwani lolotte laweze kuwakumba na wao kabla ya tarehe ya kufanyika uchaguzi.
 
Kwangu mm naona Ccm wana akili sana. ACT lazima kipate msuko suko ili kuhalalisha kuwa BM ni threat lakini ukweli ni kwamba kinachouliwa ni Chadema. Akili kubwa. Haya tuanze kupambana na ccm dhidi ya ACT.
 
Naona msajili wa vyama kama kawaida anatafuta namna ya kuinusuru CCM dhidi ya anguko la kushindwa uchaguzi

Hii serikali inatia kichefuchefu!
Na tusubiri tutaona mengi. Wananchi ndio watakaoamua. Ccm yaweza dhani inajijenga lakini ndio inazidi kuzama katika kaburi lake... je wanadhani bado wanapambana na vyama vya upinzani?

Hivi hawakujifunza katika uchaguzi wa serikali za mitaa? Ninachokiona ni kuwa CCM inataka kuua na kutia watu ulemavu wa kudumu baada ya kuona umaskini na ujinga havitoshi!
 
Na nyie mmepoa Sana! Huu uvumilivu tumeshakuwa Kama wajinga na wapumbavu!

Figisu zote hizi bado tu tunainamisha vichwa Kama makondoo! Tunataka mtuongoze,mkae front tuandamane Tz nzima! Huu upuuzi wa ubakwaji wa demokrasia mpaka lini?

Hili bomu wanajiandalia wenyewe litawalipukia.

Bomu la kwanza Tundu Lissu anakuja for strategic plans

Bomu la pili uchaguzi kama hautakuwa fare utawalipukia note my words

Bomu la tatu hili la act nalo naona msajili anamshika osama ndevu kitakachotokea sijui yangu macho.

CCM wawe makini sana this time. Watu wamechoka sana
 
Back
Top Bottom