Uchaguzi 2020 Baada ya Membe na Maalim Sharif kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, Msajili aibuka atia nia ya kukifutia usajili ACT Wazalendo

Uchaguzi 2020 Baada ya Membe na Maalim Sharif kujiandaa na Uchaguzi Mkuu, Msajili aibuka atia nia ya kukifutia usajili ACT Wazalendo

Wanaoshusha bendera za vyama vya upinzani wanachukuliwa hatua gani?

Mwakyembe alietumia madhabahu ya kanisa kufanya siasa amechukuliwa hatua gani?

Mnachokitafuta mtakipata!!
 
Why wanahaha?

Hili tulilisema toka mwanzo, Magufuli sio muumini wa ushindani wa box la kura. Na wapinzani mlipaswa kuungana kwanza kuhakikisha uchaguzi huu haufanyiki kwani hujuma ni lazima. Lakini ndugu zangu mmeingia kichwa kichwa, bila kuhakikisha hujuma hazipo.
 
Sijawahi kuona kiongozi muoga kama Jiwe!

Kama anajiamini kuwa kafanya kazi nzuri na anakubalika si aje ulingoni ashindane kwa hoja?

Sasa figisu zote hizi za nini!

Kuna kitu wanakifind kwa wazanzibari watakiget
 
Naona msajili wa vyama kama kawaida anatafuta namna ya kuinusuru CCM dhidi ya anguko la kushindwa uchaguzi

Hii serikali inatia kichefuchefu!

TUIACHE SHERIA IFUATE MKONDO WAKE kwa kuzingatia kuwa hakuna aliye juu ya sheria na kwamba Tanzania ndiyo nyumbani. Hakuna kwengine kwa kukimbilia iwapo timbwili la kujitakia likiibuliwa na wanasiasa wachache wachumia matumbo.
 
Hili tulilisema toka mwanzo, Magufuli sio muumini wa ushindani wa box la kura. Na wapinzani mlipaswa kuungana kwanza kuhakikisha uchaguzi huu haufanyiki kwani hujuma ni lazima. Lakini ndugu zangu mmeingia kichwa kichwa, bila kuhakikisha hujuma hazipo.
Hofu yao kuu zaidi ni Zanzibar mkuu.

Si vizuri kuwaachia CCM Zanzibar.

Wapinzani wakishika Zanzibar, itakuwa ni. launching pad ya kuikamata bara barabara!
 
Hii ni barua au gazeti? wenye muda wa kuisoma tunaomba mtufafanulie kuna nini kinaendelea hapa...
 
Hofu yao kuu zaidi ni Zanzibar mkuu.

Si vizuri kuwaachia CCM Zanzibar.

Wapinzani wakishika Zanzibar, itakuwa ni. launching pad ya kuikamata bara barabara!

Nimesema zaidi ya mara moja, bila machafuko hakuna kitakachofanyika. Ushindani wa njia ya kura yenye uhalali sioni ukifanikiwa. Hizo siasa za kistaarabu wanazohubiri ccm ni gia la kuwalaza wapinzani. Nilishauri kutangazwe maandamano nchi nzima, kusisitiza tume huru ya uchaguzi kila mwanzo au mwisho wa mwezi toka mwezi wa March.

Hii ingesaidia kuharamisha huo uchaguzi, na leo hii tungefika tukiwa tayari na joto zuri la uchaguzi, lakini tumekubali kuingia kwenye uchaguzi huku kelele za tume huru hazipo. Hii imetoa mwanya kwa taasisi nyingine kutumika kukomoa wapinzani.
 
Tarehe 14 Julai, siku moja baada ya picha za Bernard Membe kuwa na viongozi wakuu wa ACT Wazalendo kusambaa mitandaoni, msajili wa vyama vya siasa aliwaandikia barua chama kukusudia kukichulia hachua chama cha ACT kwa kile msajili anachokiita ukiukwaji wa sheria ya vyama vya siasa. (Soma viambatanisho kwa taarifa zaidi).

Kwenye barua hiyo Msajili amewahikisha kuwachukulia hatua kali hivi karibuni ili "wawe fundisho kwa vyama vengine".

Kwa mwenendo wa hali ya kisiasa nchini katika UTAWALA (sio uongozi) wa Rais Magufuli, mambo kama haya hayashtui wala kidogo. Ni mwendelezo wa ukandamizaji wa demokrasia ya ushindani na fikra huru.

Uoga wa nini?
Hivi inaleta maana gani, mtu - na chama chako - umekua unafanya siasa peke yako kwa miaka mitano ila bado una hofu ya vyama vengine. Umevifanya vyombo vya habari vya serikali (vinavyolipiwa kodi na kila mtanzania) kama TBC, Daily News na Habari Leo kuwa vyombo vya kukusifu wewe binafsi na chama chako. Ukaona haitoshi ukaingilia uhuru wa vyombo huru, kuvitisha na kuvifungia vengine. Nina rafiki ambae ni mharri katika moja ya magezi maarufu hapa nchini alinisimulia jinsi yule Dr. Abbas anavyowapigiaga simu kuwatisha wakipublish habari za vyama vya upinzani au zile zinazokosoa serikali.

Vyombo vyote vya dola vipo mkononi mwako. Polisi wanafanya kwa matamko yako na wanasiasa wengine na si kwa maadli. Takwimu umeminya, enzi hizo za Kikwete na Mkapa muda kama huu tungeshaona baadhi ya taasisi zikibashiri nani atashinda au kushindwa ila sasa hizi hamna atakaedhubutu kufanya hivo. Kwenye tume ya uchaguzi, Director of elections ni kada wa CCM na inajulikana, ukaona haitoshi ukaamua kupeleka maafisa wa usalama wa taifa kwenye tume. Ukkamtuma mkurugenzi wa tume abadilishe guidelines za uchaguzi kufanya iwe HIARI kuwaalika wasimamizi wa kimataifa wa uchaguzi yaaani international election observers.

Mipango yote hii ila bado kuna uoga, mi nashindwa kuelewa. Yaaani una vifaa vyote vya ushindi ila bado unaogopa? Ninaamini kuna kitu tusichojua. Either, Ni chuki binafsi ya vyama vya upinzani na fikra huru au ana taarifa kuwa ni kweli hapendwi na inabidi atumie nguvu zote alizonazo ili kupata ushindi.

Nini kitatokea ACT kikifutwa au kuzuiwa kufanya uchaguzi?
Kwanza tunafahamu kuwa ACT ndio nguzo kuu ya upinzani Zanzibar kwa sasa. Tunajua Wazanzibari walivyo, wao hawataki mchezo na siasa zao, ukimnyima Maalim fursa ya kugombea, unataka kuvuruga uchaguzi Zanzibar.

Hiyo ni kwa Zanzibar tu, ila tukihuisha taifa kwa ujumla, utaona jinisi kukifuta ACT kutakavyoleta unnecessary distraction ya uchaguzi. Kwanza vyombo vikubwa vya habari vya kimataifa kitarepoti hili tukio (najua hawajali hili), ila watakachojali ni jinsi wadau wa maendeleo wakakavyotoa matamko na kusimamisha misaada.

Tunajua nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, zipo katika hali mbaya ya uchumi kwa sababu ya janga la corona, sidhani kama Magufuli atataka aanze awamu mpya bila kupewa ushirikiano na wadau wa maendeleo, kama ilivotokea uchaguzi wa marudio wa Znzibar 2016, amabapo wadau karibu wote wa maendeleo walimsusia Shein, ikiwmo marekani kufuta msaada wa billion moja nchini.

Kingine, na hii najua Mkuu ndicho anachotaka, kutakua na voter apathy. Hapa namaanisha, watu hawataona haja ya kwenda kupiga kura maana tayari watakua wanamjua mshindi. Hii ni mbaya, maana itaonyesha kabisa demokrasia ya nchi IMEKUFA!!. Pia unajenga chuki kwa wananchi. Siku zote hata ufanye mazuri yapi, binadamu hapendi kuona mtu anaonewa. Ndio maana unaona Afrika Kusini walidahi uhuru wao hata kama wazungu walijenga vitu.

Ni hayo tu!!


ACT 4.jpg
ACT 3.jpg
ACT 2.jpg
ACT 1.jpg
 
Back
Top Bottom