Kwenye maisha mambo ni mengi, umenikumbusha aisee. Nikiwa chuo kuna dada tulikuwa karibu sana kwenye magroup ya kudiscuss hadi marafiki zangu wakawa wanasema kwamba yule dada ameonesha upendo zaidi lakini mimi sikuwa na muda wala sielewi. Kwa kweli tulikuwa marafiki hadi tunamaliza chuo then tukapoteana kabisa. Baada ya miaka nane nikaona namba ngeni kumbe ni yeye. Tukaongea sana na akauliza kama nimeoa nikajibu ndio lakini yeye akasema alizaa tu na mtu wa dini nyingine na hakuna ndoa. Akasema hivi " nilijitahidi kuwa karibu sana lakini hata hukuona kitu labda hukuwa fungu langu" hii kauli ikafanya nikumbuke maneno ya marafiki zangu na nilijisikia vibaya. Baada ya hapo hatukuwahi kuwasiliana tena na miaka mingi imepita.