Baada ya miaka 39, Taifa Stars yafuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 baada ya uicharaza Uganda goli 3-0, Uwanja wa Taifa-Dar

Hongera JB. Hongera Steve nyenyere. Hongera Wema Spatu. Hongera DAB. Hongera Pm . Hongera jpm. Hongereeni wachuzaji wetu. Hongereeni waTz na waUg. Hongera mie
Itifaki imezinguliwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Timu za kufuzu zimeongezwa, group tulilopangwa ni jepesi. Mimi nawapongeza CAF, na wala si mtu mwingine
Group halikuwa jepisi wewe labda hufuatiliagi mpira Cape Verde unawajua vizuri wewe na Uganda je? Hawa wote sio size yetu labda Kesotho hvyo usiwe mgumu kupongeza. Kilichokuwa kinatuangusha sisi ni rushwa kila sehemu sasa wala rushwa wamedhibitiwa na JPM matunda tunayaona.
 
Kumbaf kabisa jitu kama wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maslahi feki yamefeli. Atukuzwe Mungu aliyetuvusha. Shukrani kwa Taifa Stars, Coach na benchi la ufundi kwa juhudi zenu.

Hatimaye AFCON
 
Ushindi wa goli 3 kwa 0 ilioupata timu ya taifa stars leo dhidi ya Uganda na hivyo kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Nchi za African@ AFCON zitakazochezwa Misri mwezi June mwaka huu ni uthibitisho mwingine kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mh Paul Makonda ni hadhina kwa taifa kwenye upangaji na usimamizi wa masuala ya kitaifa.

kwa faida ya wengi ni kwamba Mh Makonda alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya kuiwezesha taifa stars kufuzu AFCON 2019 ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa na jukumu la kushirikiana na Uongozi wa timu kubuni mbinu na mikakati ya kiufundi ndani na nje ya uwanja, bila shaka kwa matokeo yaliyopatikana inahitaji kiburi na husuda na wivu kupinga kwamba hajafanikiwa.

Jukumu lingine kubwa lilikuwa ni kuhamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu ili kuwapa nguvu na hamasa wachezaji ya kupambana na kushinda. Katika hili la kuhamisha watu kujitokeza tumpe Kongole Makonda kwa niaba ya kamati aliweza kuwaunganisha watu maarufu kutoka tasnia za muziki, filamu, wanamitindo, wanasiasa na kuwaomba kutumia vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuhamisha wananchi na matokeo yake yameonekana uwanja ulijaa yaani zaidi ya watu 60,000 walikuwepo taifa.

Kwa kurejea baadhi ya mambo mengine mengi ambayo mhe Makonda amewahi kufanya;-

## kufanikisha kama kusaidia Walimu katika Mkoa wa Dar es salaam kupanda daladala bure,

## kufanikisha upatikanaji wa bima za afya @ toto kadi kwa mamia ya watoto ambao wametelekezwa na wazaz.

## kuwapatia viatu bandia walemavu, kuchangia matibabu ya wagonjwa mbalimbali nje ya Nchi.

## kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi zinazohusu ardhi na kuwasaidia wakina mama hasa wajane waliodhurumiwa Nyumba na mashamba.

## kupanua huduma za kijamii kama vile ujenzi wa hospital Temeke, shule za sekondari na Msingi hivyo kuwawezesha wananchi na wanafunzi wengi kupata huduma.

Makonda ni binadamu pamoja na mafanikio hayo Lukuki aliyofanya katika kipindi kifupi ambacho amekuwa mkuu wa Mkoa yaweza kuwa kuna mapungufu ya hapa na pale amefanya lakini hayaondoi ukweli kwamba amejitanabaisha kuwa ni asset kwa taifa letu.
 
1. Ni mara yangu ya kwanza kuiangalia timu ya taifa uwanjani kwa mkapa

2. Nimetoka mikoani huko interior kuja kushuhudia tukio hili muhimu

3. Pamoja na kelele za jezi ya "msalaba" lakini mimi niliinunua nilipigwa 30,000/= si haba nilikuwa nazo acha nao wavune leo

4. Hamasa ya watazamaji ilikuwa kubwa sana lakini burudani ni za kishamba wanaleta vidada vinakata viuno tena mbali na jukwaa kuu, yule dada wa danadana katikati ya uwanja hakuja hata karibu na wageni kuwaburudisha

5. General ukiuangalia uwanja kijumla rangi nyekundu na nyeupe kama za simba zilionekana kwa maana nyingine hizi jezi za msalaba na zilile nyingine zilimezwa

6. Wazungu huteua rangi moja ambayo huizaa mashabiki wote ambazo wakiva wote huweza kumtisha mpinzani.

7. TFF hawapangilii na wala sikuona duka lao pale uwanjani lenye jezi authorized hata kama laki tungenunua sisi wa mikoani tofauti na sasa wamewaacha wamachinga na wachina wanajibunia makorokocho yao ndio wanaita jezi za taifa na zikishasambaa wanapiga kelele za kwao zipo wapi na duka gani??

8. Tukitaka uzalendo lazima na hata kwenye sare tufanane sio wengine meupe wengine blue, wengine kijani wengine nyekundu vurugu mechi.

9. waganda walikuwa wachache lakini ukiwaangalia nguo na bendera zao wate wanafanana nadhani tuanze kubadilika tupitishe rangi moja official ambayo itatumiwa na watu wote
 
hongera jpm kwa kutufungia lile goli la tatu kama la tyson kombe la dunia

current location@ ilala pub[emoji847][emoji854][emoji854][emoji854][emoji481][emoji481]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niwape hongera sana wachezaji wa timu ya Taifa na wananchi wote kwa ujumla kwa kuwapa moyo vijana wetu na hatimaye tumeuona ushindi

Hamasa iliyojengwa ilikuwa kubwa sana. Kuanzia vyombo vya habari, viongozi wa serikali, wa kisiasa na hata wa dini wote kwa pamoja wali wapa hamasa vijana wetu kuufikia ushindi wa leo

Kilichofanyika uwanjani kinadhihirisha kwamba kumbe watanzania si kwamba hatuwezi, ila huwa tunakosa kitu kidogo sana ambacho ni hamasa katika kile tukifanyacho

Ukiangalia kuanzia mechi ya juzi kati ya Simba na wale wakongo na hii ya leo utagundua kumbe tukitiwa moyo tunaweza kufika mbali

Katika tasnia ya ualimu, walimu wanasisitizwa kuwapa moyo na ku wahamasisha wanafunzi kujaribu na kufanya kwa kujiamini katika masomo yao bila kuwakatisha tamaa wala kuwacheka pale wanapokosea

Taifa Stars kushinda leo goli tatu kwangu mimi naona wamewapa somo kwa vitendo wale wote waliohusika kufanikisha hamasa iliyokuwepo kwamba wasisubiri mwishoni tu kuja kutia hamasa.

Na pia hili ni somo kwa viongozi wetu kwamba watu wao wakipewa motisha, wakihamasishwa kwa lugha nzuri ya upendo na ya ushindi vitu vitafanyika vizuri tu!

Binadamu hufanya kitu kizuri pale anapokuwa huru na anapopewa motivation hufanya vizuri zaidi!

Tuache lugha za vitisho kwa wafanyakazi wetu wa chini, tuache mikwara kwa tunaowaongoza badala yake tutumie lugha ya ki ungwana, lugha inayohamasisha mafanikio... hakika tutatoka hapa tulipo.

AFCON, NI ZAMU YETU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…