Ushindi wa goli 3 kwa 0 ilioupata timu ya taifa stars leo dhidi ya Uganda na hivyo kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Nchi za African@ AFCON zitakazochezwa Misri mwezi June mwaka huu ni uthibitisho mwingine kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mh Paul Makonda ni hadhina kwa taifa kwenye upangaji na usimamizi wa masuala ya kitaifa.
kwa faida ya wengi ni kwamba Mh Makonda alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya kuiwezesha taifa stars kufuzu AFCON 2019 ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa na jukumu la kushirikiana na Uongozi wa timu kubuni mbinu na mikakati ya kiufundi ndani na nje ya uwanja, bila shaka kwa matokeo yaliyopatikana inahitaji kiburi na husuda na wivu kupinga kwamba hajafanikiwa.
Jukumu lingine kubwa lilikuwa ni kuhamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu ili kuwapa nguvu na hamasa wachezaji ya kupambana na kushinda. Katika hili la kuhamisha watu kujitokeza tumpe Kongole Makonda kwa niaba ya kamati aliweza kuwaunganisha watu maarufu kutoka tasnia za muziki, filamu, wanamitindo, wanasiasa na kuwaomba kutumia vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuhamisha wananchi na matokeo yake yameonekana uwanja ulijaa yaani zaidi ya watu 60,000 walikuwepo taifa.
Kwa kurejea baadhi ya mambo mengine mengi ambayo mhe Makonda amewahi kufanya;-
## kufanikisha kama kusaidia Walimu katika Mkoa wa Dar es salaam kupanda daladala bure,
## kufanikisha upatikanaji wa bima za afya @ toto kadi kwa mamia ya watoto ambao wametelekezwa na wazaz.
## kuwapatia viatu bandia walemavu, kuchangia matibabu ya wagonjwa mbalimbali nje ya Nchi.
## kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi zinazohusu ardhi na kuwasaidia wakina mama hasa wajane waliodhurumiwa Nyumba na mashamba.
## kupanua huduma za kijamii kama vile ujenzi wa hospital Temeke, shule za sekondari na Msingi hivyo kuwawezesha wananchi na wanafunzi wengi kupata huduma.
Makonda ni binadamu pamoja na mafanikio hayo Lukuki aliyofanya katika kipindi kifupi ambacho amekuwa mkuu wa Mkoa yaweza kuwa kuna mapungufu ya hapa na pale amefanya lakini hayaondoi ukweli kwamba amejitanabaisha kuwa ni asset kwa taifa letu.