Baada ya miaka 39, Taifa Stars yafuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 baada ya uicharaza Uganda goli 3-0, Uwanja wa Taifa-Dar

Baada ya miaka 39, Taifa Stars yafuzu kucheza michuano ya AFCON 2019 baada ya uicharaza Uganda goli 3-0, Uwanja wa Taifa-Dar

Ushindi wa goli 3 kwa 0 ilioupata timu ya taifa stars leo dhidi ya Uganda na hivyo kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Nchi za African@ AFCON zitakazochezwa Misri mwezi June mwaka huu ni uthibitisho mwingine kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam mh Paul Makonda ni hadhina kwa taifa kwenye upangaji na usimamizi wa masuala ya kitaifa.

kwa faida ya wengi ni kwamba Mh Makonda alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya kuiwezesha taifa stars kufuzu AFCON 2019 ambapo pamoja na mambo mengine ilikuwa na jukumu la kushirikiana na Uongozi wa timu kubuni mbinu na mikakati ya kiufundi ndani na nje ya uwanja, bila shaka kwa matokeo yaliyopatikana inahitaji kiburi na husuda na wivu kupinga kwamba hajafanikiwa.

Jukumu lingine kubwa lilikuwa ni kuhamasisha Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu ili kuwapa nguvu na hamasa wachezaji ya kupambana na kushinda. Katika hili la kuhamisha watu kujitokeza tumpe Kongole Makonda kwa niaba ya kamati aliweza kuwaunganisha watu maarufu kutoka tasnia za muziki, filamu, wanamitindo, wanasiasa na kuwaomba kutumia vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuhamisha wananchi na matokeo yake yameonekana uwanja ulijaa yaani zaidi ya watu 60,000 walikuwepo taifa.

Kwa kurejea baadhi ya mambo mengine mengi ambayo mhe Makonda amewahi kufanya;-

## kufanikisha kama kusaidia Walimu katika Mkoa wa Dar es salaam kupanda daladala bure,

## kufanikisha upatikanaji wa bima za afya @ toto kadi kwa mamia ya watoto ambao wametelekezwa na wazaz.

## kuwapatia viatu bandia walemavu, kuchangia matibabu ya wagonjwa mbalimbali nje ya Nchi.

## kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi zinazohusu ardhi na kuwasaidia wakina mama hasa wajane waliodhurumiwa Nyumba na mashamba.

## kupanua huduma za kijamii kama vile ujenzi wa hospital Temeke, shule za sekondari na Msingi hivyo kuwawezesha wananchi na wanafunzi wengi kupata huduma.

Makonda ni binadamu pamoja na mafanikio hayo Lukuki aliyofanya katika kipindi kifupi ambacho amekuwa mkuu wa Mkoa yaweza kuwa kuna mapungufu ya hapa na pale amefanya lakini hayaondoi ukweli kwamba amejitanabaisha kuwa ni asset kwa taifa letu.
Kwenye mpira nagoma na nafanya kiburi kabisa!
Watanzania kwa mpira wala hatuhitaji wanasiasa au watu wasioujua mpira kutuhamasisha!
Yaani mm Shilole Wema sepetu wanihamasishe kushangilia timu yangu ya Taifa?watu ambao hata mashindano yenyewe hawayajui?watu ambao wao wenyewe wanaulizana kuwa mashindano haya si ndio wanayoshindana Simba?
Nakataa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ungepewa wewe jukumu lile la kuhamasisha ungeshindwa?

Funzo kwa maccm Magufuli akiwa muungwana Taifa linaweza kusimama pamoja kama jana, aache kuwagawa Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nyinyi mlijigawa kitambo sana ndio maana kabla ya mechi dua zilikua ni Tanzania ifungwe. So uliowaona jana uwanjani na waliokuwemo humu ni watanzania ambao mda wote huwa wanawapuuza. Huwa nasema Tanzania ni kubwa zaid ya jf,usijifungie humu ukaja na propaganda zako eti taifa limegawanyika. Majibu umeyaona jana na 2020 somo ni hilihili

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Hiyo ni coincidence tu.
1-Kwa Taifa Stars ushindi wetu umetokana kwanza waganda wamesha-qualify hivyo hawakuwa na haja ya ushindi, pili hata kama tungemfunga Uganda magoli 10 na Lesotho angeshinda ingekuwa ushindi wetu ni wa bure tu.
2-Kuhusu Simba SC wa kupewa credit ni Mo Dewji ambaye anaigharamia club na kuhakikisha timu inafanya vizuri.
3-Hassan Mwakinyo kama alivyosema mweyewe ame-struggle kivyake mpaka amefika alipofika.
Tuache kutumia siasa katika michezo, usitake kuwafanya wanamichezo wote ni wanachama wa CCM, unaweza kufanya perfomance yao kuteremka.
Tumeona tu kamati ya uhamasishaji ya Taifa Stars ikiongozwa na baadhi watu wa CCM kuna watanzania walikuwa wakiiombea timu yetu ifungwe.
Kama tunavyosema tusichanganye dini na siasa, hivyo hivyo tusichanganye michezo na siasa.
Huoni jinsi Magufuli alivyopambana a rushwa kwenye michezo?

Akina Malinzi wako wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kamsikilize Chief Coach wa Uganda..alisema wachezaji wake hawakuwa motivated baada ya kuwa walishaqualified.. Bashite hatabaki kuwa Zero..
hakuna mtu asiependa ushindi na kuweka ka historia cha kutokufungwa mech hata moja sema jana tuliwazidi kila kitu kuanzia uwanjani nje ya uwanja hadi uwanjani wachezaji na hayo ni maneno tu ya kocha na je wangetufunga angesema hvyo?
 
Nijuavyo mimi
1. Msuva 21'
2. Nyoni 51'
3. Agrey Morris 57'

Wakati vijana hawa wakiyafanya haya, Mungu alikuwa upande wetu Uganda hawakuchezesha full squad na kule Cape Verde FT 0-0

Kama kuna mwingine alifunga goli zaidi ya hawa basi tunapoenda Egypt tusimsahau.
 
kwani 1.5trilioni zimepotea kipindi cha rais gani?
Hizo 1.5T umetumia ripoti ya zito au CAG?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
CAF wameongeza timu za kushirik AFCON ndo mana tumepita wengi, mbona huyo mtu wako alivyopiga bit ndo tukaenda kufungwa, punguzen kulamba ndala za watawala

Sent using Jamii Forums mobile app
Defence mechanism

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Mkiwa na kiongozi mkuu ambaye hataki siasa anataka kazi tu ,mambo yote hubadilika kutoka juu mpaka chini ,tofauti na tulivyokuwa tunaaminishwa na baadhi ya wasomi hasa chadema kwamba rais hata akiwa mwizi ,mvivu mzururaji mambo yataenda tu kisa eti urais ni taasisi?

Asante Taifa stars, Simba na bondia Mwakinyo

Asante kasi ya Rais Magufuli.

Sent using Jamii Forums mobile app
usishau na ushindi huu....

 
Back
Top Bottom