Waheshimiwa! Kwa hii story niliyoandika nimegundua kitu kimoja cha ajabu sana, imagine like 70% hawajaongea kuhusu matukio ya hiyo familia na tabia zao za ajabu ila wanashangaa kutoa 15M ??!!!
Kiukweli nimepambana sana na bado napambana, ilifikia hatua nikataka kuuza gari, na biashara nilifunga nikaanza from scratch! Lakini kwenye maisha yangu yote sijawahi kuwa na uoga wa kushtushwa na 7figures.
Mtu anasema huna uwezo wa kutoa 15M, mwingine kama story ni ya kweli basi 0 moja imeongezwa 😄... sasa hebu jiulize kitu kimoja, kama tokea umezaliwa hadi sahivi (naamini wengi ni 30s) unakosa imani kabisa mtu akiandika 15M, ramani yako (roadmap) ipoje aise? Au ndo tunaishi kwa mazoea tu kwamba ukila, ukinywa ndo baasi hayo ndo maisha? Hakuna savings, hakuna malengo, hakuna dharura? 15M si pesa rahisi kupata wala kutoa, lakini it means hata ukiipata ila ukaja kuipoteza kwenye hasara za biashara inaweza kukuzika!
Ukiendelea kushtushwa na hizo pesa hutozipata mazee, sio kwamba ninazo hata! ila sometimes act kama unazo at least ikujengee ujasiri, maana sasa kama unaisoma 15M na bado unashangaa japo ni maandishi tu na upo over 30 si hatari hiyo?! Acheni hizo mambo bhana tupambane 😄😄😄