Baada ya Nape Nnauye, Makatibu Uenezi wa CCM Taifa waliofata walipwaya sana

Baada ya Nape Nnauye, Makatibu Uenezi wa CCM Taifa waliofata walipwaya sana

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Hii ndio sababu ya Chama cha Mapinduzi ccm kutapatapa.

Kiukweli ni kuwa ccm haina tena kitu cha kuwadanganya wananchi cha kusema inaeneza.

Siasa za hadaa na ahadi za uongo zimekuwa ni zile zile kwa miongo kadhaa.
Baada ya Nape Nauye na sera yake ya kujivua gamba ambayo kiasi fulani ilileta matokea kwenye utendaji wa serikali hakuna Katibu Mwenezi Mwingine aliyeleta Tangible results.

Hii inatokana na kuwa Makatibu wenezi waliofata waliamini kazi yao ni kuonge ongea tu na kufoka foka bila vitendo.

Matokeo yake Uongozi wa Juu wa Chama na Serikali hauoni Kazi hasa zinazofanywa na hao walioteuliwa.

Wakati mwengine wakiamini labda wamekoswa kuteua, wanatengua na kuteua tena.

Hata hivyo hali imezidi kuwa mbaya maana kila Twuzi wanajikuta wamekosea zaidi.

Kumwengua Paul Makonda na Kumleta Amos Makala linaweza kuwa tatizo kubwa zaidi kuliko alilokuwa nalo Paul Makonda.

Mungu ameondoa Mikono yake juu ya ccm. Inasubiri anguko tu.

Mtawatumbua Makatibu Enezi woote lakini mnawaonea tu. Nyakati zimefika zisomeni.

Zile itikadi za hadaa, propaganda wananchi wanazielewa hawadanganyiki tena.
 
Hawakupwaya kipindi cha nape vyama vya upinzani vilikua na nguvu na ccm ilikua ikijifanyia mageuzi ndani ya kichama wote wamefanya kazi sawa!
Walipwaya sana. Na ndio maana chama kinatapa tapa....mara Abdul Shaka, mara Sofia Mjema mara Polepole. Ndani ya Muda mfupi
 
Mwisho wa siku tunataka kuona Matokeo.....hayo makundi kwetu wananchi hayana tija
Kazi ndio hiyo ndani ya miaka 60 chama kinaendelea kuimarika na kufanya mageuzi mengi imetunga sera na ilani nzuri zinawakosha wananchi na kupata kura nyingi zinazoendelea kusimika dola kila uchaguzi!
 
Ukweli usemwe Nape aliimudu sana ile nafasi ya Uenezi, aliweka mlima ambao imekuwa vigumu kufikiwa na kila anayekuja kuchukua hiyo nafasi baada yake.
 
Hawakupwaya kipindi cha nape vyama vya upinzani vilikua na nguvu na ccm ilikua ikijifanyia mageuzi ndani ya kichama wote wamefanya kazi sawa!
Kwahiyo hivi sasa hata chamatwawala hakina jipya kwakuwa kimelala fofofo,huku kikijidanga wapo wabunge ishirini wakuteuliwa wanao waamsha chama twawala😅
 
Kazi ndio hiyo ndani ya miaka 60 chama kinaendelea kuimarika na kufanya mageuzi mengi imetunga sera na ilani nzuri zinawakosha wananchi na kupata kura nyingi zinazoendelea kusimika dola kila uchaguzi!
Labda sera ya kupora uchaguzi, bunduki na masanduku kwenye vyumba vya kupiga kura.
 
Kwahiyo hivi sasa hata chamatwawala hakina jipya kwakuwa kimelala fofofo,huku kikijidanga wapo wabunge ishirini wakuteuliwa wanao waamsha chama twawala😅
Hahaha
 
Jamii forum kuna watu ni cream grade one ya hii website iq zao ,akili zao , uzi zao , mawazo yao

Afu kuna grade ya kati hawa hawa atleast iq zao wana piga nyuzi kali pia

Kuna makapi ya jamii forum kama huyu mwandishi huwa wanaanzisha uzi hata kama huna manufaaa mara nyigi uzi unakuwa mfupi kama status ya whatsapp
afu full pumba ....makapi ya jamii forum siku hizi yapo mengi sana

Hivi kweli nape huyu nape ndo aliwazidi wengine ......kawaida sana huyu jamaa zaidi labda sifa za kijinga
 
Mkuu umemsema mwenzako halafu wewe ndio umeonekana kituko.
 
Nape kaweka rekodi isiyovunjwa. Ndio maana tangu aondoke wanabadilisha badilisha kila siku. Mara Polepole wakamtoa, Shaka wakamtoa, Njema wakamtoa na Makonda wakamtoa. Viatu ni vipana sana
 
Back
Top Bottom