Baada ya Ndoa kuvunjika, sheria inasemaje kuhusu matunzo ya mtoto? Ni hiari au ni lazima Wazazi kutunza watoto?

Baada ya Ndoa kuvunjika, sheria inasemaje kuhusu matunzo ya mtoto? Ni hiari au ni lazima Wazazi kutunza watoto?

Kuna sehemu nimesoma, mwanasheria mmoja kutoka kwa Majirani zetu, Kenya, Anasema kwamba, kwa mujibu wa sheria, kama ulimuoa single mother, ukaanza kuishi naye na ukaanza kum-support yeye na mwanaye kwa mahitaji yote, ikitokea changamoto, mkaamua kuachana basi yule mama ana haki ya kukuburuza mahakamani endapo utasitisha kutoa huduma na matunzo kwa yule your Non-biological kid(mtoto wa kufikia) uliyemkuta naye.

Hii imekaaje wataalam, mbona wanaume hatuna pa kukimbilia, kila kona sisi ni wa kubebeshwa mizigo kama punda!

Kwa mujibu wa sheria au mujibu wa sheria za Kenya. Sheria za kwetu zinasemaje???
 
Hapo najiuliza,ilitokea pia mwanamke alinikuta na watoto,tukawa tunawahudumia kwa pamoja,baada ya kuachana,na yeye ataendelea kuwajibika nao?
Ikate Kote Kote na hiyo ndio maana halisi ya Sheria hizi za upande mmoja tuu ni utaratibu tu na wala si Sheria
 
Mkuu Kwani Kuna shida gani kulea mtoto wa kidume mwenzio? Unaambiwa ukipenda Boga penda na ua lake.
 
Kuna sehemu nimesoma, mwanasheria mmoja kutoka kwa Majirani zetu, Kenya, Anasema kwamba, kwa mujibu wa sheria, kama ulimuoa single mother, ukaanza kuishi naye na ukaanza kum-support yeye na mwanaye kwa mahitaji yote, ikitokea changamoto, mkaamua kuachana basi yule mama ana haki ya kukuburuza mahakamani endapo utasitisha kutoa huduma na matunzo kwa yule your Non-biological kid(mtoto wa kufikia) uliyemkuta naye.

Hii imekaaje wataalam, mbona wanaume hatuna pa kukimbilia, kila kona sisi ni wa kubebeshwa mizigo kama punda!
nimecheka mno😁 hivyo ukioa single maza maana umebeba na dhamana ya mwanae milele?
 
Mkuu Care Giver

Mosi, Mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa ana Haki zote za msingi za kurithi mali ya Baba yake. Kabla ya mwaka 2011 watoto wa nje ya ndoa hawakuwa na Haki ya kurithi mali za baba yao.

Lakini sheria ya mtoto mwaka 2019 mtoto wa nje ya NDOA ana haki zote za kurithi mali ya mzazi wake. Miaka ya nyuma kesi zilikuwa zikiamuliwa kwa kufata sheria za kimila kwamba watoto wa nje ya ndoa hawana haki ya kurithi mali.

1. Katiba ambayo inasema watu wote ni sawa.
2.sheria ya mtoto kifungu cha 5 ambacho kinakataza kubagua watoto
3.sheria ya mtoto kifungu cha 10 ambacho kinampa Haki ya ku-enjoy mali ya mzazi wake.
4.mikataba ya kimataifa kuhusu Haki za watoto ambazo Tanzania imeridhia.

Kiuhalisia katika sheria hakuna kitu kinaitwa “mtoto Haramu” sababu mtoto hapangi azaliwe wapi au asizaliwe wapi.
vipi mirathi ikiendeshwa kwa sheria/ kanuni za kiisram!
Ambapo mtoto wa nje hatambuliki ,,,ni haramu!
 
Back
Top Bottom