Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Oky Inaendelea....

Wakati bado tunaendelea kusubiri likizo ifike twende kwa mganga kuna siku nilitoka shuleni kwenda getto kwake kupumzika lakini hakuwepo nilitoa ufunguo juu ya mlango nikafungua nikaingia ndani.

Kwa jinsi nilivyokuwa nimechoka nikasema ngoja nilale kidogo kisha niangalie ustaarabu wa msosi cha kushangaza ile nimepanda kitandani nikasikia kitu kama maji maji ya baridi kuangalia vizuri nikaona damu zimetapaka kitandani japo sio nyingi kivile.

Ikabidi nifunge mlango niondoke baadae sana jamaa alikuja mpaka shuleni lakini sikutaka kumuuliza zile damu zilitokana na nini maana aalikuwa anaonekana hana tatizo lolote wala sikumwambia kuwa nilienda getto lakini nilibaki na maswali mengi kichwani nikijiuliza jamaa atakuwa alifanya nini pale.

Baada ya likizo kufika nilimwambia muddy kuwa tubaki pale kwa jamaa twende wote kujaribu maisha kwa mganga kwani kulingana na story za agustino alizokuwa akipewa na jamaa yake kuwa mgaanga katajirisha watu kibao.

Lakini muddy alikuwa kama anasita maana yeye alikuwa anatuzidi miaka mingi kama 9 hivi sema kwenye cheti alikuwa kapunguza akatuambia yeye anafamilia soo anatakiwa aendee nyumbani kusaidia matatizo kadhaa next round tutampeleka na yeye. Kile kitendo kilinivunja moyo lakini niliamua kubaki pale maana kwa zile story za pesa nilikuwa sina ujanja

Basi agustino baada kama ya siku mbili akaniambia tuanze safari jamaa atakae tupokea na kutupeleka anatusubiri tayari wameshaongea basi safari ikaanza kuelekea shinyanga ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika tulitumia kama masaa 8 kufika shinyanga mjini jamaa alitupokea akatupeleka kwake kusema ukweli jamaa alijuwa na uwezo lakini sii wakutisha sana watoto wa mjini wanasema pesa ya kula

Usiku baada ya kupiga msosi wa nguvu alikuja hadi kwenye chumba alichotupatia kulala akaanza kutupa story jinsi alivyokuwa kapuku mpaka sasa anamiliki coaster kadhaa, go dowm za mpunga, nyumba , gari ya kutembelea, akatuambia kama mkifata masharti vizuri ya mganga lazima mambo yetu yataa kaa vizuri kama yeye . baada ya hapo akatuambia kesho asubuh anatupeleka kila kitu tutaambiwa na yule mkongomani.

Huyo mganga alikuwa anakaa njee kidogo ya shinyanga maeneo kama sijasahau panaitwa isaka kama unaelekea kahama tulichukua masaa kadhaa tukawa tumefika jamaa alipaki gari kwa mbali kidogo akatupeleka kwa jamaa fulani akatuambia hapa ndio mtakaa hadi mmaliziwe shughuli yenu tulikabidhiwa chumba kiko kwa njee tukaweka mizigo

Kisha tukaanza kutembea kuelekea kwa yule mganga tulitumia dakika chache hadi kufika hapo kwa mganga alikuwa na uwanja mkubwa sana alikuwa amejenga nyumba ndogo anakaa na familia yake . Katikati ya uwanja alikuwa amejenga vijumba vidogo viwili vya majani njee ameweka mabenchi ya kutosha, mbele ya uwanja alikuwa na pagala kubwa halijamalizika.

Tulifika jamaa akapitiliza hadi kwa mkee wa mganga wakasalimiana kwa furaha na bashasha akamueleza nimewaleta vijana wangu kisha yeye akaondoka sisi tukaambiwa tukapange foleni kwenye benchi maana tulikuta watu wengi kiasi . Wakati tumekaa pale tulianza kusikia vitu vyaa ajabu ajabu maana kuna kijumba kimoja mtu alikuwa akiingizwa kati ya vile viwili analia na anapiga kelele za kufa mtu

Wengine walikuwa wanakuja na mbuzi,mkaa,kuku, ,mara wengine wanatoka kuoga kwenye lile pagara mara sauti za ajabu zinatoka kwenye kile kijumba kama majini nikabaki napigwa tu butwaa tulikaaa pale hadi muda wetu wakuingia ukafika baada ya mmama mmoja kutoka tukaitwa na msaidizi tuingie mule kilingeni.

Kwanza tulivyoingia tu unakaa huku umenyoosha miguu kwenye mkeka Peku mbele kidogo kulikuwa na kigoda kidogo mganga alikuwa amekaa chini nyuma yake kulikuwa na ngozi kubwa ya mnyama kama chui imetundikwa ukutani, alikuwa na kibakuli kimejaa mawe fulani hivi kama mayai meupe yanamadoa doa meusi, kulikuwa na kioo kikubwa sehemu yote ilikuwa imefunikwa na kaniki nyeusi, kulikuwa pia na kidishi cha maji ya kunawia alikuwa anavikopo vya madawa kama 500 pembeni yake.

Basi baada ya kutuchukua maelezo kidogo akasema lazima atupige ramli kwanza ili kujua nyota zetu na swala la ramli kila mmoja atoe 5000 maana kwa wale wataalam wa maswala ya uganga wanajua ramli haipigwi bure wala kwa mkopo pia ramli inatakiwa kila mmoja apigiwe kivyake soo ikabidi mmoja atoke njee abaki mmoja.

Basi mimi ikabidi nitoke nimuache jamaa ndani ....








Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duu naomba unitag ukitupia
Muddy kajitokeza kaiendeleza sasa jamaa kakata tamaa kabisa.Akina Muddy huwa si watu wema aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
Stori yakinafki

Sent using Jamii Forums mobile app
hiz story za ntaendelea zimesheheni sana hapa jf

mikito mikito kashaharibu jf

Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseeeee leta Leta mkuuu
Njia yenyewe tayari ina giza, iweje uone uone/ upate mali kwa njia hiyo?
Imeshaisha story Mkuu [emoji23][emoji23]
Heee ndio imeisha?

Sent using Jamii Forums mobile app
mzee baba tunasubil Fanya uanze Kuandia bac
Sijui wanajionaje hawa
ngoja tumsubil akuje na mwendelezo ila sijui kama hata tunywesha chai ya rangi
Na jinsi walivyo-run Cartel yao


Sent from my iPhone using JamiiForums
Endeleza hii kitu wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikendelea unistue aseee
nasubiri mwendelezo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama umeshapata mtaji haina haja ya kumwaga damu
Huyo mkongo anapatikana wapi
Story kali na ni nzuri sana tunaisubiria tujue jinsi gan ulikuwa drag dealer na kukimbizana na cops
Subscribed.!!
Haya mvuta bange ndio imeisha au
Tayari wakuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji2215][emoji2215][emoji2215]

Sent from my SM-A105G using Tapatalk
 
Back
Top Bottom