Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Keshoooo naamka nayo[emoji188][emoji188]
umegusa mulemule kasoro wewe walikuacha na boxer..
huwa zinavuliwa zote
AiseeeNyungu nishafanya sana hii maamuzi ni yako uachwe na boxer au uivue......
Sent using Jamii Forums mobile app
Okay Inaendelea....
Ilichukua muda nikiwa pale njee nikitafakari yale niliyoyaona mule ndani kwenye kile chumba wakati agustino akiendelea kupigiwa ramli.
Basi ndipo agustino akatoka na kunioneshea ishara kuwa nizame kilingeni bila kusita nikaamka pale nikaingia moja kwa moja mule kilingeni nikakaa huku nikiwa ninenyoosha miguu yule mganga akaniambia kuwa weke 5000 ndani ya yale maji nikafanya kama alivyoelekeza.
Baadae akachukua udi akawasha akachukua kibakuli kilikuwa kama na mawe yanafanana na mayai akayashika mkononi akaanza kuyazungusha kwenye kiganja cha mkono halafu mkono mwingine akachukua mkia kama wa mbuzi akaanza kuchovya kwenye dishi la maji ananyunyiza nyunyiza wakati huo akaniambia ninyanyuke chini ni kae kwenye kigoda ambacho kiko mbele yake.
Kisha mfanyakazi wa mganga akaleta njiwa mganga akachukua ile njiwa akavuta kichwa hadi kikatoka kwa kutumia mkono kisha akaanza kuongea maneno ya ajabu sauti yake ikabadilika kabisa ikawa kama ya mzee aliyekabwa na kitu kooni licha ya kuwa na umri kama 40 hivi halafu akaanza kuongea kama wakongo man huku akitafuna meno balaa yani anatafuta unasikia sauti ya meno yakisagika ndani ya mdomo yule kijakazi wake ndio akawa anatafasiri.
Sijawahi kwenda kwa mganga sehemu nyingine ila nadhani wengi wao watakuwa wanapiga ramli kwa njia hii .
Jamaa aliyekuwa anatafasiri ndio akaanza kuniambia dhumuni langu lililo nipeleka pale kuwa nikutafuta pesa na kama nikitoa kafara za damu na kufata masharti lazima lengo langu litatimia tena nitakuwa mtu ambaye ni tajiri sana maana nyota yangu inangaa sana ,baada ya pale na blaa blaa nyingi mganga akarudi katika hali yale.
Baada ya hapo mganga akasema kabla ya kufanya kitu chochote inabidi kwanza tufanyiwe madawa ili kuondoa mikosi yule jamaa yangu agustino akaitwa tukaambiwa tukanunue kuku Jogoo mwekundu kila mmoja, kitambaa Cheusi na chekundu, mkaa, Wembe kama sisi ni wageni tutoe pesa wakanunue wao ili kesho asubuhi tuwahi kazi ianzee kiukweli sikuwa na pesa kila kitu jamaa yangu alinilipia baadae akaturuhusu kuondoka
Pia alitupatia dawa flani hivi yakuogea na kunywa usiku na asubuhi kabla hatujaenda Kwake
Tulivyorudi kwenye lile getto ndio nilikuja kujua kuwa ni kama nyumba ya wagonjwa na matatizo mbali mbali ya wanao enda pale kwa mgangaa tulitafuta kimgaahawa tukaenda kula huku tikipiga story za kujipa moyo kesho yake tukawahi asubuhi na mapema kwa yule mganga ila tulikuta watu kadhaa wameshafika.
Jamaa yangu ndio alikuwa wa kwanza kuingia baada ya watu kadhaa kuhudumiwa baada ya hapo alipelekwa kwenye kale kachumba kadogo kaliko kuwa pembeni asee baada kama ya dakika moja nilisikia anatoa kelele za vilio vya maumivu nikawa najiuliza hivi hiko chumba wanafanywa nini baadae akatolewa ameloa jasho vibaya akapelekwa kwenye lile pagara ambalo halijamalizika .
Zamu yangu ikafika nikaingia kilingeni mganga akasema ili kuondoa mikosi uliyokuwa nayo lazima upigwe nyungu, wengine wanaitwa kufukizwa, nikapewa dawa nikanywa halafu nikachukuliwa kupelekwa kwenye kale kakilinge kengine roho ikaanza kudunda huku nikijiuliza kupigwa nyungu ndio nini.
Nilivyofika jamaa kaniambia toa nguo zote nikabaki na boksa niliona ndani ya kile chumba kuna kahema kadogo sana kamatengenezwa na kitambaa kama cha mwamvuli nikaambiwa ingia humo halafu ukae kwenye kigoda kisha akaniambia ufumbe macho yaani usije ukafungua maana ukifungua tu matatizo utakayoyapata usije kulaumu mtu
Kweli nikafumba macho kwa nguvu zote huku nikiwa nimekaa kwenye kile kigoda kisha nikahisi kama wameingiza sufuria usawa wa miguu yangu kisha nikasikia jamaa ameingiza kitu kama jiwe kwenye lile sufuria nilitaka kufumbua macho lakini kwa vile vitisho niliogopa baada ya hapo niakaanza kusikia kama kunajoto limeongezeka kutoka kwenye lile sufuria
Baada ya sekunde kadhaa nikasikia kama jiwe lingine limewekwa na joto linaongezeka aseee mwili ukaanza kuchemka jasho likaanza kunitoka hadi masikioni ,likawekwa tena jingine nikasikia mvuke umetoka unaanza kunichoma asee maji ya kawa ya moto zaidi mvuke ukawa mwingi nikatamani niinuke pale lakini nikaona niharibu dawa asee sijawahi kuchomwa staili ile tokea na zaliwa
Uvumilivu ulinishinda na jamaa nasikia bado anaongeza nikaanza kupiga kelele nililia kama mtoto mwili ulikuwa umeloa kila sehemu nilitoka jasho sidhani kama nitatoa jasho kama lile hadi naingia kaburini maumivu yalipozidi nikasikia jamaa ametoa kile kihema ndio ikawa hafadhali mwili wote ukabali kutoa maji kama mvua baada ya dakika akaniambia vaa nguo unifate kweli nikafanya hivyo nilisikia nimekuwa mwepesi kama karatasi
Tulizinguka tukaenda kwenye kile kipagara kinavyumba vingi nikaenda kumkuta jamaa mwingine ameshikilia kuku akaichinja damu ikamwagika kwenye dumu lenye maji kama lita ishirini lilikuwa limechanganywa na madawa kadhaa kuku yule nae akatumbukizwa mule jamaa tena kaniambia simama kisha utoe nguo zote nikabaki na boksa.
Alikuwa na ufagio akawa anatumbukiza mule kwenye yale maji yenye dawa akitoa ananichapa nao tena kwa nguvu huku akiongea maneno fulani ambayo nilikuwa siyasikiii aseee nilichapwa mpaka yale maji yote yakaisha akabaki kuku mwenyewe kisha nikaambiwa kaa kwenye majani ya migomba waliokuwa wemetandika kwenye kile chumba nilikaa pale kama masaa matatu....
Sent using Jamii Forums mobile app
Story nzuri inavutia kusoma ina ujumbe mzuri ✔️✔️✔️✔️✔️✔️Sasa baada ya muda kama dakika 15 hivi ya mazingumzo agustino akatoka njee akaniambia wamesha malizana tukapita tukakata miwa halafu tukaondoka njiani agustino akaniambia huyu mzee anapesa yake nyingi lakini ataki kumrudishia amekuwa akimzungusha na malipo kidogo kidogo
Lakini sikutaka kufatilia sana maana nilijua ni madeni tu ya kawaida nilirudi hostel yeye akapitiliza getoni kwake, ilipita kama mwezi jamaa akaja kuniambia anaenda mkoa fulani kumuona ndugu yake baada ya wiki moja atageuza nikasema sawa.
Alikaa kama wiki mbili nakumbuka ilikuwa juma mosi mida kama ya saa 8 hivi mchana akanipigia simu nilikuwa na tecno jeneza kisimu flani hivi kigumu, akaniambia nichomoke hostel na jamaa yangu mmoja alikuwa anaitwa Muddy twende tukampokee amekuja na vitu vingi tumsaidie kupeleka getto wala sikusita nikamwabia muddy agustino amesema tukampokee tuliondoka mpaka centre tukachukua boda hadi stendi baada ya muda kidogo akafika
Alikuwa amekuja na mabegi 4 makubwa sana yaani ni makubwa kweli kweli pamoja na mazaga zaga mengine kwenye mfuko akaniambia nikaite tax nikaenda kufata wakaelewana bei kisha tukamsaidia kupakiza kisha akatuachia 10000 akatuambia tuchukue mizigo iliyobaki tuipakie kila mmoja kwenye boda turudi nayo getto kweli tulifanya hivyo
Tulivyorudi tukamkuta ameshafika getto tukaanza kupiga yale mazaga zaga aliyokujanayo biscuit, pop con,ndizi baada ya hapo akasema kesho tumpeleke town tukiirudi kuna kitu anataka kutueleza maana sisi tumekuwa masela wake watiifu sana
Kweli kesho yake tukachukua usafiri mpaka mjini breki ya kwanza akasema tumpeleke atm kiukweli niliona kama maajabu how comes kijana mdogo anakadi ya bank maana mimi mpaka muda ule nilikuwa naenda bank kulipa ada tu sikuwahi kanyaga bank kwenye ishu yoyote ile. Alitupeleka hotelini tukapiga msosi tukapita pita mjini akatununulia baadhi ya vitu nayeye kanunua kisha tukarudi getto.
Tulivyofika getto ndio jamaa akaanza kufunguka kuhusu biashara anayofanya mazingira ya pale kabla hajaendelea kutupa story ndio akatuambia sogezeni begi moja niwaonyeshe daa akachukua funguo ndogo akafungua kijikufuli flani hivi kuangalia ndani nikasikia marashi ya kufa mtu, juu kulikuwa na taulo kama la kuogea akatoa lile taulo baada ya hapo akatoa kitenge kikubwa kilichokuwa kimefuniika mzigo baadae akamalizia karatasi ya nailoni daa kutoa niliona vitu kama mifagio ya kijani.
Harufu ya bangi ikatoka kali kifala chumba kizima tukabaki kushangaa na jamaa yangu muddy kisha yule agustino akaanza kusema hii ngoma imekauka sana akachukua maji akaanza kuirushia rushia maji huku akituambia hii njia ni safe sana askari hata awe mjanja kiasi gani hawezi kushitukia mchezo akaanza kutuambia yeye ndio supplier wa bangi ule mtaa mzima na anatengeneza faida kubwa kwani anakotokea zinalimwa kama mchicha bei ndogo akija huku anapata faida kubwa sana.
Jamaa aliendelea na ule mchezo kuna wauzaji wengine alikuwa anawapelekea mali kauli kama yule mzee kisha tunaenda kufata pesa baada ya siku kudhaa tulikuwa tukienda kwa yule babu tunakuta ameikata kata ile mifagio imekuwa kama chenga halafu anaitengeneza na rizila inakuwa kama sigara tulikuwa tukifika tunachukua kwanza kama stiki tatu tatu tunavuta stimu zikipanda tunasepa yaani nilijikuta kwenye uvutaji wa bangi bila kujua
Kuna siku alituita akatuambia katika maisha yake amejaribu kila njia ya kupata pesa nyingi lakini dili zake bado hazijakaa sawa ila kuna ndugu yake amemuelekeza kuna mganga mkongomani yuko mahali ukitaka utajiri ni ndani ya siku kadhaa tena hana masharti magumu akatuambia lazima aende ndipo na mimi nikamwambia tufanye likizo na mimi nije niendee nikajaribu bahati...
Sent using Jamii Forums mobile app
Basi kila fundi na ufundi wakeNyungu nishafanya sana hii maamuzi ni yako uachwe na boxer au uivue......
Sent using Jamii Forums mobile app
aisee najua baadhi humu watakuwa wamepitia hayaOkay Inaendelea....