Inaendelea........
Nilikaa pele kwenye majani ya migomba kama masaa 3 hivi hadi jua likaanza kuwa kali maana lile jumba lilikuwa liko wazii kwa juu.
Nilikaa pale nikaangalia juu nikawa naona jua linavyo nipiga huku nikiendelea kutoa manyoya ya kuku ambayo yalikuwa yameganda sehemu mbali mbali za kwenye mwili wangu nikaanza kujiuliza hivi kweli ndio nimeamua kupitia njia hii?
Sikuwaza sana wala sikujutia kutokana na maisha ambayo nilikuwa nimepitia hapo nyuma, maisha ya kuomba omba kwa watu na kufanya vibarua vya ajabu ajabu. Ada yenyewe ya masomo nilikuwa mpaka nikapige magoti kwa afisa elimu kama mtoto yatima ndio itolewe .
Wakati bado naendelea kuwaza nikasikia sauti ya yule kibaraka wa mganga ananiambia vaa nguo unifuate basi baada ya hapo nikapelekwa hadi kilingeni nikamkuta mganga akaniambia kaa kwenye kigoda kisha akaniambia vua shati na suruali upandishe hadi magotini.
Baada ya hapo akachukua kibakuli kilikuwa na unga mweusi pia akachukua wembe akaupasua akaanza kunichanja, Alianza kunipiga chanjo mbili mbili kila sehemu kuanzia utosini, kifuasi, nyuma ya shingo, kwenye viwiko vya mkono, kwenye magoti, panapo unganisha mkono na kiganja, pia mwisho wa miguu kwenye maungio ya mguu na kikanyagio.
Alipomaliza akaanza kunipaka ule unga mweusi alipomaliza akaniambia niondoke na nisije nikaoga mpaka kesho yake nirudi kupata maelekezo mengine niliondoka hadi pale tulipopewa chumba nikamkuta jamaa yangu amesha fika na amefanyiwa kama mimi niliyofanyiwa.
Basi tulilala hivyo hivyo kesho yake asubuhi tukawahi kwa mganga baada ya kwenda tuliingia pamoja na agustino kisha tukapatiwa dawa ya kwenda kuogea halafu mganga akatuambia tumebakiza mambo machache tu tukamikishe yaliyotupeleka pale.
Akatuambia siki ile ile tunatakiwa kwenda kati kati ya barabara yaani njia panda majira ya saa saba usiku tufanyiwe dawa halafu itakuwa imebaki hatua moja ili tuweze kuondoka basi tuliondoka tukaenda tukaoga tukapumzika ili ikifika mida mida ya usiku tuanze kwenda kwa yule mganga.
Baada ya muda kufika tulienda kwa mganga akatukabidhi kijakazi wake alitoa zile kaniki nyeusi ambazo tulikuwa tumekwisha zinunua akatuambia tuvae kisha tukaanza safari haikuwa mbali sana kama mita 250 tukawa tumefika.
Baade tulikaa kati kati ya bara bara akatuchanja utosini akafanya madawa yake pale halafu akatoa kijembe kidogo sana unaweza kukishika na mkono mmoja tu akachimba udongo kisha akatuambia kila mmoja achote mchanga tukaweka kwenye mfuko kila mtu tofauti halafu kwenye lile shimo akatoa dawa flani akafukia mule.
Baada ya hapo tukaondoka tukarudi hadi kwa mganga ,tulikuta mganga anashughulikia mama mwingine na watu kadhaa walikuepo sisi yule jamaa akatuambia tuondoke halafu kesho asubuhi turudi tena
Kesho yake asubuhi tukaenda mganga akatuambia imebaki hatua moja pia mizimu na mababu lazima ipate zawadi ambayo ni damu ili ipate furaha itutekelezee jambo letu vizuri tukasema hakuna tatizo tuko tayari basi mganga akatuambia lazima mlipie gharama shillingi 50000 kwa wale vijakazi yeye malipo yake tutarudisha mambo yakiwa sawa basi jamaa yangu bila kusita akatoa pesa yote pale pale.
Kisha wakasema leo usiku ndio tunaenda kumaliza kila kitu tutoe na pesa wakanunue nazi na udi kwa ajili ya kazi yetu baada ya hapo wakatuambia tuondoke turudi usiku maana kazi itaanzaa saa sita usiku.
Basi tulikuwa na furaha tukijua kuwa tunaenda kumaliza kila kitu ili turudi tuendelee hata kupiga msuli maana nakumbuka jamaa alikuwa kwenye begi amabeba mastering history awe anapitia pitia lakini hakuwahi igusa hadi tunatoka pale kwa mganga
Basi usiki kwenye mida ya saa 5 tukajisogeza pale tulikuta jamaa wameandaa vitu kadhaa wamaweka kwenye gunia basi tukaanza safari nilikuwa nadhani tunaelekea njia panda laahaula baada ya kutembea sana kama kilo mita moja tukajikuta tuko eneo la makaburi daa nikaanza kuogoba basi tulivyofika jamaa wakatuambia tubadili nguo yaani zile kaniki nikikumbuka nacheka sana tulikuwa kama bongo movie kisha jamaa akatoa kile kijembe akachimba mbele ya kaburi moja .
Akaniambia chota mchanga na mkono wa kulia basi nikachota nikauweka kwenye kile kimfuko cha kule njia panda halafu akaniambai nilale juu ya lile kaburi pia na jamaa yangu akaambiwa afanye hivyo hivyo basi wakawasha udi kuzungula lile kaburi.
Daa wakangomani ni hatari asikwambie mtu nilisikia wanaanza kuongea lugha nisiyo ielewa wakawa kama wanakemea mapepo yaani zaidi ya walokole wanavyokemea kisha walikuwa na kikamba kama kombeo cha kupasulia nazi wanaingiza nazi ndani yake wakati huo mimi nimelala chali halafu wanapasua nazi juu ya kaburi usiki unasika kama baruti
Kwa kuhesabu haraka haraka walipasua kila mmoja nazi kama saba kisha tukaondoka wakatuambia tuondoke bila kuongea kitu chochote tukafika hadi kwa mganga wakatuambia tuondoke tusiongee jambo lolote hadi kesho asubuhi turudi pale tupewe maelekezo ya mwisho.
Kweli tuliondoka hatukuongea neno lolote kila mmoja alijikausha hakuna ambaye hata alikohoa, asubuhi na mapema tukafika pale kwa mganga tukakuta mabaharia wengine wako pale wanaonge tu habari za madini baadae tuliitwa maana Sisi tulikuwa ni kama tumesha maliza basi.
Mganga sikuio ni kama alikuwa na furaha sana tulionge story za kawaida kisha akatuambia naona kabisa mnaenda kutimiza malengo yenu dawa zote na kila kitu kimeenda sawa sasa ni hivi akatoa ule mchanga ulikuwa katika kila kimfuko akanipatia mimi na agustino pia kisha akatoa mbegu za maharage akanipatia mimi mbili na agustino mbili akazifunga kwenyw karatasi nyeusi .
Kisha akatuambia hizi mbegu mtaondoka nazo kila mmoja kwa wakati wake atanunua jogoo mwekundu halafu mida ya saa saba usiku utaenda upandikize kwa kutumia huu mchanga maji usimwagilizie itakuwa ni damu ya yule kuku kisha utahesabu siku saba utaenda kuangalia kama imeota angalizo nalo wapa usionekane na mtu yoyote yule.
Pia akatuambia baada ya siku saba ukikuta hazija ota usijisumbue kurudi kwangu maana mambo yako yatakuwa yamesha haribika mizimu itakuwa imekukataa sito weza saidia kitu chochote.......
Sent using
Jamii Forums mobile app