Baada ya njia za giza kugonga mwamba kwenye kusaka utajiri, nimeamua kufanya hivi

Usisahau kutuletea hiyo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oooky Inaendelea......

Jamaa Agustino yeye ikabidi aendeleze gemu maana alisema elimu yaya sasa hivi haamini kama inaweza mtoa anataka a base kwenye maswala ya biashara tulikuwa tukikaa mahali akianza kupanga plani zake asee unaona kabisa huyu jamaa haichukui muda atakuwa tajiri

Akaniambia huko kwao sema operations za maaskri zimekuwa nyingi lakini anataka achukue shamba hata ekari kumi sehemu za pembeni apande mahindi kati kati apande bangi yale mahindi yawe kama cover

Maana alisema kwenda kukusanya bangi inachukua muda na sehemu nyingine kama hufaamiki hawakuuzi so anataka kuingia yeye mwenyewe front line

Siku zikazidi kukata bado anaendea kuuza na katika maeneo yale japo ni kijijini ila shughuli ya kiuchumu iliokuwepo ilikuwa inachochea ulevi sana, ukahaba soo mzigo ulikuwa unatoka

Kunasiku jamaa hakutokea shule maana alikuwa kaniambia kunamtu kamtumia mzigo daa kumbe askari wa barabarani wamezidisha doria mzigo haukufikishwa hata kule kwao mkuu wa wilaya alikuwa anazunguka kila kona kuteketeza mashamba na kukamata watu kuhusiana na bangi

Basi ikabidi atulie kidogo baada ya muda kupita kunajaaa ambae ni ndugu yake pia niliwahi kumkuta getto kwa agustino alimpigia simu akamwabia kuna njia imepatikana ni nzuri sana yaani hiyo maaskri hawawezi kujua kama unasafirisha jamaa aliwauliza hiyo njia ni ipi?

Jamaa akamwabia unachukua mifagio ya bangi hapa ambao hawafaamu vizuri bangi ikiwa inachumwa inawekwa mpaka inakauka inakuwa kama ile mifagio tuliokuwa tunachuma maporini tunaenda kufagilia shuleni

Soo jamaa akamwabia unachukua fagio unalipiga maji kwa kunyunyizia ili lisidondoshe yale matawi halafu unatafuta ubao mzuri na panga kali mithili ya wembe unaanza kuikata kata vupande vidogo vidogo kicha unachukua yale madumu makubwa ya njano lita 20 unaanza kujaza zile chenga kisha unachukua karatasi unafunga kwa juu plas mfuniko ngoma inatembea

Wakati ule tuliona mvumbuz wa ile njia ni bora sana agustino alikuwa anasema hata angekutananae angempa zawadi

Kweli ile njia ilianza kuzaa matunda jamaa akawa anaenda anachukua mzigo anapakia kwenye madumu kisha anaweka juu kule kwenye kelia ya gari akifika anaita boda anafunga kisha anatembea

Kunasiku tulikuwa tunampekea babu mzigo tukakutana na kikosi cha majama wa pale pale washamba tu wakaanza kututolea vitisho kulikuwa kunammoja ameenda age kama 30+ akaanza kusema ninawaonya fanyeni yalio waleta muondoke zenu mkiendelea nitawafanya kitu kibaya mimi nimezaliwa hapa

Basi baada ya vile vitisho hatukujibu kitu tukaondoka hadi kwa yule babu, huyu babu hakuwa mzee ila alijuwa anamatatizo fulani ya mwili halafu alikuwa anaishi kwenye kijumba kidogo sana mwenyewe. Ilibidi agustino amwabie story ya wale jamaa lakini babu akatupa moyo akasema yule jamaa hana lolote now wateja wamemuama alikuwa anachanganyia watu bangi na majani tofauti ili apate faida sana

Basi kipindi hiko nilikuwa sina stress sana na maisha maana darasani nilikuwa nimeanza kurudi rudi vizuri na yule jamaa yangu muddy alikuwa anatupiga msasa sana hata yeye hatukumueleza yale mazaga zaga yaliyotukuta kule kwa mganga

Basi siku zikaenda bado tunaendelea kupiga mishe zile zile mpaka tukamaliza kidato cha tano ilibidi mimi nisepe kurudi home kweli nilimkuta mama anaendelea vizuri agustino yeye alibaki kule kuendelea kukusanya pesa zake kwa wale jamaa

Baada ya kufungua shule nikakaa siku kadhaa jamaa akanitumia message nakuja na mzigo njoo unisaidie kupokea nikaenda hadi standi alikuwa na madumu kama 5 nikapakia 2 yeye akapakia yalio baki. Tulipofika getto akasema wakati uliondika kunajamaa amemwabia ana sehemu anataka kumkodishia afuge samaki pia kule kwao amesha kodi mashamba ya kuzugia kilimo cha mahindi ndani aweke bangi

Kiukweli jamaa agustino licha ya kuwa alikuwa anadili na biashara haramu lakini alikuwa ni mtu mwenye maono ya kufika mbali alinisapoti sana kwenye maswali ya kifedha hadi nikasahau yale maisha ya kuunga unga

Baada ya siku kadhaa kupita tulikuwa darasani muda wa vipindi lakini jamaa aliniambia naondoka naenda kupokea mzigo standi nimetumiwa maana getto alikuwa amemaliza kila kitu kiukweli lile eneo lilikuwa na walevi wengi tena bangi ilikuwa inatoka vibaya lakini agustino alikuwa anatokea wilaya tofauti ambayo ndio kilimo cha hilo zao limeshamili

Basi aliondoka akatuacha pale darasani yalipita masaa kadhaa nikasema ngoja nimtafute jamaa atakuwa kasha rudi getto likini simu yake haikupatikana, nilimpigia yule jamaa yake akapiga kwenye lile gari wakasema jamaa alifika akapakia mzigo kwenye boda akasepa baada ya hapo yeye hajui chochote

Nikasema ngoja nianze safari kutoka pale hostel niende kwenye getto lake nione kama atakuwepo nilifika pale subiri sana tena kwa njee maana alikuwa ameondoka na ufunguo subiri sana mtu hatokei piga simu hadi nikaanza kuwa na wasiwasi nini kitakuwa kimemkuta agustino?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23] wanajesh ndio hawajui uchawi heeee!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rise and fall of agustino mandumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Endelea mkuu


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
troublemaker Carleen Davet 😊
 
Duuh!! yan nasoma huku napiga maombi story isiishe.Dah!!andika nyingine tumtafute mwanetu Agustino
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…