Oooky Inaendelea.............
Niliendelea kukimbia haraka haraka kuelekea ule muembe ulipokuwa baada ya muda kidogo nikaanza kuuona kwa mbali haikuchukua muda nikawa nimefika mahala pale chini ya ule muembe bangi nilizokuwa nimevuta na ule mchaka mchaka ilikuwa imeshapanda kichwani sikuwa na uoga wowote nikawasha ile taa ya sola ,mdogo mdogo nikaanza kusogelea kile kipande cha jiwe.
Nilisogea karibu hadi nikakifikia kisha nikakikanyaga kile kipande cha jiwe halafu nikaanza kumulika na tochi kutafuta kama zile mbegu zimechipua nilitafuta mulika pande zote pale chini sikuona kitu chochote tafuta sana fukua majani bila mafanikio piga tochi pande zote kuzunguka lile jiwe wapi hakuna kitu.
Wakati naendelea kutafuta kupiga tochi kwa mbele nikaona tena kipande kingine cha jiwe chini ya ule muembe kinafanana na kile kile nilicho kuwa nimekikanyaga ndipo nikarudi kuangalia vizuri kwenye mguu wangu nilipokuwa nimekanyaga asee alikurupuka bonge la paka akatimkia kwenye vichaka vilivyokuwa pande zile .
Kumbe muda wote nilidhani nimekanyaga jiwe kumbe ilikuwa ni paka ikabidi nisogee kwenye lile jiwe lingine nikawa naangalia kwa umakini kulizunguka kama mbegu zitakuwa zimeota maana ndio kitu pekee nilichokuwa nimeweka kama alama ya kumbu kumbu.
Baada ya kuangalia kwa umakini ndio nikabahatika kuona zile mbegu zimeota pembeni ya lile jiwe nikaona ndio ile sehemu niliokuwa nimechimba mchanga nakufukia asee kweli niliamini uchawi huendi kwa mentali baharia nimelamba Jokel ,kama ingekuwa kwa wale jamaa wa kubet wangesema nimeshinda jackpot.
Nikatoka pale kwa spidi ya 100km/h mpaka nikafika getto nikamkuta jamaa yangu agustino amepiga usingizi kucheki pale chinj zile damu nilizokuwa nimeziacha hazipo nukamuamsha jamaa tukaanza kupiga story swali la kwanza aliloniuliza akanimbai umeona zimechomoza kwa tabasamu la bashasha nikamwabia ndio aseee akaanza kucheka nikamuuliza niliona humu getto kuna damu zimetapaka hapa chini zimeenda wapi akaniambia hajaziona sikutaka kuendelea kumuuliza ikabidi nivute shuka nijilaze
Wakati nimelala niliwaza pesa zikianza kuingia ninunue vitu vingi magari, nyumba, starehe, mademu ,nifanye anasa zote niliendelea kuwaza hadi usingizi ukanipitia nilikuja kuamka muda umekwenda sana tukaanza kuweka mipango tutatumiaje pesa ambazo tukaanza kuzipata pia ilikuwa imebaki kama wiki moja tu tufungue shule
Siku hiyo ilibidi agustino ampigie simu yule jamaa wa kule shinyanga akamwabia tumefanikisha wote maana mbegu zimetoa majani sasa tunasikilizia tuanze kuvuna tulichokipanda jamaa kwa haraka kabisa akasema tumpigie mganga tumwabie tumefanikisha lile jambo kwa ustadi wa kiwango cha lami.
Tulijaribu kumpigia mganga siku nzima simu inaita tu haipokelewi hadi jioni mida ya saa moja mgamga akampigia agustino basi waliongea mambo mengi kidogo ila mganga akasema yaani kama tumefanikisha kila kitu kimeenda sawa mizimu imesaidia sana kwani imetukubali lazima nayenyewe ipate zawadi kama shukurani ya kutupokea katika ulimwengu wa watu wenye fedha
Mganga akasema zawadi ya mizimu ni hayo mazao mliyoyasumbukia yeye malipo yake anataka fedha na mifugo tumpelekee maana kuanzia leo pesa zitaanza kuhangaika kututafuta tulipo mizimu imevunja nature ya ulimwengu kwamba pesa tutaitafuta kwa jasho badala yake sisi pesa ndio itatumia jasho kututafuta asee agustino alikuwa ameweka loud speaker nilikuwa nimetegesha sikio hakuna siku nimefurahi kama ile kusikia maneno yenyewe kutia moyo kama yale
Basi akaendelea kusema zawadi ya mizimu ni zile mbegu zilizochipua usiku wa saa saba twende tukazichume tukazitupe njia panda na hayo ndio yatakuwa malisho ya mizimu na jinsi watu watakavyokuwa wanaendelea kupita huku na huku kwenye ile njia mchana hadi usiku ndivyo pia pesa zitaendelea kutua kwenye mifuko yetu
Pia akatupa angalizo kuwa hayo ndio maneno ya mwisho kuongea nae kwenye simu kazi yake amesha maliza maelekezo yote ametupatia anachosubiria ni sisi atuone kule kwenye boma lake siku tunaenda kumpatia zawadi zake kama yule jamaa wa kule shinyanga alivyofanya baada ya hapo akakata simu.
Basi tukasema kazi iliyobaki ni ndogo sana kiukweli kutokana na kutembea usiku mara kwa mara nikawa nimesha zoea naona kitu cha kawaida siku hiyo agustino akaniambia twende kule kwa babu tulianza safari tukavuka kijimto tulivyofika hatukumkuta tukasema ngoja tuendelew kumsubiri ili akifika atupatie zile stiki za bangi alizokuwa tayari amezitengeneza sasa baada ya kukaa kwa madakika tukamuona kwa mbali anatokea shambani kumwagilia matikiti alivyofika tukamueleza shida ikabidi atupatie mabaki akamwabia agustino inabidi mzigo mwingine uletwe maana stock yote amemaliza
Tukapiga kweli ganja za maana kujiweka sawa kwenda kumaliza mchezo, ule usiku tulipita mahali tikapiga msosi tukaelekea hadi getto tukanywa zile dawa, nyingine tukaogea tena wakati tunataka kuondoka tukapiga tena bangi kisha kila mmoja akashika njia yake.
Mimi nikaanza kutembea mpaka nikaacha barabara kuu nikaanza kuingia vichakani basi nikaendela kuongeza mwendo huku nimeshikilia tochi yangu lakini sikuwa nimeiwasha basi sijui nini kiliniambia geuka nyuma kwa mbali nikaona mwanamke kama mama mwenye nyumba amesimama ananitazama nikaendelea kutembea kugeuka sikuona kitu chochote tena.
Basi nikaanza kutembea mpaka nikakaribia ule muembe kufika pale chini nikawasha tochi bahati mbaya kutafuta sikuona kitu chochote tafuta sana guys asikwambie mtu pesa ya shetani ni mgumi balaa nilitafuta hadi nikasanda ikabidi niondoke wakati nageuka nyuma naangalia pale niliona jopo la watu wengi wakiwa wamewasha moto mkubwa unaunguza hadi matawi ya ule muembe ikabidi nianze mbio nimekimbia sana kufika getto namkuta agustino amelala pembeni ya kitanda kuna damu kibao halafu nikaanza kumshitua.
Wakati nimemkuta amelala nikajua jamaa atakuwa amesha kamilisha mpango nilijuta kwanini nilichagua kupanda mbegu chini ya ule muembe nilihisi na mkosi nilio usababisha mimi mwenyewe nikaanza kumuita agustino kwa nguvu jamaa bado ameuchapa ikabidi nianze kumvuta anipe habari mambo yake yaliendaje vipi
Nikamtikisa sana wala jamaa anisemeshi wala haongei ndio nikazidi kuchanganyikiwa kuangalia uvunguni nakuta matone ya damu tena freshi nikabaki kujiuliza huyu agustino nini kitakuwa kimempata au niite mama mwenye nyumba aje anisaidie lakini roho inakataa ikabidi nitoke njee nichote maji nideki zile damu na nitoe ile shuka halafu nione kama nitaweza pata msaada kwa watu
Basi baada ya hapo nikachukua kindoo nikatoka njee nikafungua kisima kilikuwa kimezibwa na bati kwa juu nikachota maji wazo la kwanza nikasema ngoja nimwagie labda atazinduka nikachota kikomba kizima kikamwagia wapi daa nikaona hii ishu ninaelekea babaya nikachukua simu nikampigia yule jamaa wa shinyanga simu haipatikani nikasema jamani mimi nitafanya nini nitakimbila wapi...
Sent using
Jamii Forums mobile app