Uchaguzi 2020 Baada ya Nyalandu kuongoza kura za awali kwa 100%, Je ni dalili za Nyalandu kupeperusha bendera ya CHADEMA? Je, Lissu atarudi kweli J3?

Naona unamshambulia mchangiaji kwa kutoa mawazo yake binafsi.
 

Kunywa chochote utakacho hapo sinza, niPM nakuja kulipa.
 
Huelewi kitu unaongelea ushabiki, Lissu asipopitishwa kugombea uraisi na CDM utafanyaje?, Watu wapo kimaslahi zaidi nyie mnaleta ushabiki wa Simba na Yanga.
Jibu simple sana ,,tutampigia kura Magufuli na wabunge wa ACT
 
Mimi nimemfungukia na kumwambia ukweli yaani mtu anakuwa chanzo cha kuleta taharuki ndani ya chama.

Amsapoti huyo Zitto wake na Membe wake tuone kama watafanikiwa maana tulikuwa tuna wapa sapoti kwa kuamini kuwa nao ni wapinzani wenzetu.
Misile ametuangusha sana
 
Kawakataza nani? Pigeni mnakotaka na sisi tutampigia kura mh Lissu na wabunge na madiwani wa cdm na hatimaye kuifurusha ccm kutoka magogoni.
Jibu simple sana ,,tutampigia kura Magufuli na wabunge wa ACT
 
Wewe utaongea unacho jisikia kutokea huko kwenu Burundi.

Tuwachie sisi watanzania tufanye kazi zetu kwa manufaa ya nchi yetu.
Nyalandu katenga bilioni 5 kwa ajili ya kampeni, unategemea Mbowe amuache amchukue Lisu anaetegemea michango ya buku buku kutoka kwa akina mmawia na tindo?
 
MKuu muda utasema kweli, wewe utapiga kelele tuu. Ni vizuri tusubiri matokeo ya uchaguzi 2020.
 
Kosa kubwa Sana na litakaloiua cdm na kuondoa uaminifu kwa wanachama ni kutompa Lissu nafasi,Lisu anauchungu na watz wanaokandamizwa na mifumo dhalimu,amekuwa akiwatetea hata kabla ajapigwa risasi.
Kwa Sasa cdm bila lisu itafutika Kama Cuf bila maalimu
 
MKuu muda utasema kweli, wewe utapiga kelele tuu. Ni vizuri tusubiri matokeo ya uchaguzi 2020.

Tusubiri matokeo yapi, wakati matokeo yote yatatokana na utashi wa Magufuli? Kungekuwa na ushindani kwa maana ya ushindani, tungesema tusubiri matokeo. Kwa mfano, hebu nipe matokeo ya kilichotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kama sio hayo ninayo kuambia kuwa ni maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi?
 

Mkuu unajitahidi katika uchambuzi, lakini moja ya mapungufu yako:

1) ama kuwa na mapenzi ya kupitiliza kwa upinzani.
2) Kutotaka kubadilishana uelewa na kuto taka kuchambua kwa undani kila tukio zito ili kupata mjumuiko ambao utatengeneza muono sahihi wa kesho kisiasa. Siasa ni pamoja na kujua kuchuja propaganda ili kutenganisha la kweli na la uwongo. Bahati mbaya unatakiwa mara nyingi uwe na elimu ya kutosha kuweza kutumia formula ya uchambuzi ya HYPOTHESIS ANALYSIS NA SYNTHESIS ANALYSIS kwa uweledi na ufasaha.

Bahati mbaya katika hili la upungufu na mapenzi kupitiliza tupo wengi mnoo tena pande zote mbili wasiopenda mabadiliko na wapenda mabadiliko, inapelekea kupunguza utamu wa michango na kupunguza thamani ya JF.
 
Tangu lini Manyumbu mmejitambua? Nyie mko kutii maagizo ya DJ mbowe na yeye ndo anaamua nani agombee. Aliamua agombee Lowassa 2015 na ikawa hivyo, mwaka huu akiamua asimame Nyalandu au akiamua kumuunga mkono Membe manyumbu lazima mfuate na mumsifu huyo mtakae elekezwa. CHADEMA NI MBOWE
 

Sina tatizo na maoni yako, ila umekuja na hoja ambayo inabebwa na mahaba niue zaidi. Ni kweli nina mapungufu, ila sio hayo uliyoyaweka wewe. Umekuja na mchango kuwa Lowassa ndio alileta kura cdm uchaguzi wa 2015. Wakati ninajua fika 2015 cdm ndio ilikuwa chama cha kisiasa kilichopandisha hamasa zaidi ya kisiasa, na wapiga kura kuliko chama chochote. Kazi hiyo cdm iliifanya toka 2010 baada ya uchaguzi, mpaka 2015. Lowasa alikuwa kama mfungaji aliyebaka na goli wazi, kisha afunge kwa Madaha, halafu unataka awe nyota wa mchezo, kisa kafunga goli pekee la ushindi?

Kudhibitisha uko na hoja ya kupika, nimekuambia kama yeye ndio alileta kura 6m+ akiwa ni miezi miwili, taja alileta viti vingapi akiwa na miaka miwili. Au taja idadi ya matawi aliyofungua ndani ya hiyo miaka miwili, naona unazunguka tu.

Tuje kwenye hili la uchaguzi wa 2020. Magufuli kama Magufuli sio muumini wa box la kura, na ameshinda mara chache mno kwa njia ya box la kura, tena hata huko alifanya figisu zote. Wakati akifanya hayo alikuwa ni waziri tu, je leo hii ni rais, kwa katiba hii mbovu unategemea aheshimu box la kura?

Tuje kwenye mifano halisi wa kitakachotokea kwenye uchaguzi huu. Nitajie toka Magufuli ameingia madarakani ni lini kumewahi kufanyika uchaguzi wa kweli? Kwa macho yangu nimeona ukatili, ushenzi na uhayawani wa wazi ili ccm watangazwe washindi kwenye chaguzi za marudio. Yote haya yamefanyika kwa utaratibu wa jeshi la polisi na tume ya uchaguzi. Nimeona wasimamizi wa uchaguzi wakifunga ofisi zao ili kukwepa kupokea fomu za wapinzani, hatimaye mgombea wa ccm apite bila kupingwa. Ukifuatilia mbinu hizi, zote ndio alizokuwa akitumia Magufuli huko nyuma kupata ubunge.

Hayo hapo juu nimeyataja kwa uchache, lakini funga kazi ya tabia za Magufuli kwenye chaguzi za nchi hii, ilikuwa ni kwenye uchaguzi wa SM. Wote tuliona uchaguzi uliokosa heshima na ushenzi wa kiwango cha juu kutokea ndani ya chaguzi za nchi hii. Sina chochote cha kuongea maana matokeo yalikuwaje, na ushindi wa ccm ulipatikaneje kila mtu anajua. Kinachosaidia mpaka sasa kwa hali hii kutokea ni ukondoo wa watanzania. Jaribu kufuatilia mwenendo wa uchaguzi wa October, kote huko tayari kimeandaliwa mazingira ya kufanikisha uchaguzi wa hujuma na ushenzi wote unaoufahamu wewe. Ndio maana asasi zote zinazofahamika kwa kusema ukweli zimezuiwa kuangalia uchaguzi, na taasisi zote na waangalizi wa kimataifa wanaoweza kusema kweli wamezuiwa! Hivyo uchaguzi wa 2020 utakuwa ni wa tabia binafsi za Magufuli dhidi ya upinzani. Kama kweli unasimama kwenye ukweli, basi huo ndio ukweli.
 

Uko sahihi sana kwa usemalo, ni kweli Mbowe alifanikiwa kumuweka Lowassa na watu walitii. Na hata sasa atamuweka anayemtaka, ila sio kila siku ni Ijumaa. Safari hii akikosea shabaha, ndio atajua sisi wapiga kura ndio wenye maamuzi ya kura. Tusiandikie mate, maana umekuja kwa mihemko kama mwanamke aliyemfumania mumewe na house girl.
 
Kiongozi huwa naheshimu michango yako, na naamini wewe sio mmoja wa walioamini Lowassa ataleta mabadiliko yoyote na haupo kwenye kundi la waliokuwa wakizungusha mikono. Amini nakwambia upeo wa watanzania wengi upo chini. Wanafata upepo tu, hata Mbowe ampitishe Nyalandu Kisha aungane na Membe kumsimamisha awe mgombea bado kuna nyomi kubwa litashangilia tu. Kuamini maneno yangu linganisha michango yako humu JF tu na wapuuzi wengine wasiotumia LOGIC michango yao ni mipasho tu. Mfano, sehemu zote humu ulipoulizwa humu JF Lissu asipopitishwa utafanyaje?, Jibu lako limekuwa uongozi wa CDM ndo utawajua vizuri. Wenzako wasiotumia akili wakiulizwa wanaanza matusi na kejeli, na kusisitiza tayari Lissu kashapitishwa. Meaning hawana plan B. Wakati mkifia chama na kuonyesha hisia zenu, kwa Mbowe na waliomzunguka ni picha tofauti. Wanaangalia maslahi zaidi. Jumatano jioni sio mbali,tutajua mbivu na mbichi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…