Mkuu unajitahidi katika uchambuzi, lakini moja ya mapungufu yako:
1) ama kuwa na mapenzi ya kupitiliza kwa upinzani.
2) Kutotaka kubadilishana uelewa na kuto taka kuchambua kwa undani kila tukio zito ili kupata mjumuiko ambao utatengeneza muono sahihi wa kesho kisiasa. Siasa ni pamoja na kujua kuchuja propaganda ili kutenganisha la kweli na la uwongo. Bahati mbaya unatakiwa mara nyingi uwe na elimu ya kutosha kuweza kutumia formula ya uchambuzi ya HYPOTHESIS ANALISIS NA SYNTHESIS ANALISIS kwa uweledi na ufasaha.
Bahati mbaya katika hili la upungufu na mapenzi kupitiliza tupo wengi mnoo tena pande zote mbili wasiopenda mabadiliko na wapenda mabadiliko, inapelekea kupunguza utamu wa michango na kupunguza thamani ya JF.
Sina tatizo na maoni yako, ila umekuja na hoja ambayo inabebwa na mahaba niue zaidi. Ni kweli nina mapungufu, ila sio hayo uliyoyaweka wewe. Umekuja na mchango kuwa Lowassa ndio alileta kura cdm uchaguzi wa 2015. Wakati ninajua fika 2015 cdm ndio ilikuwa chama cha kisiasa kilichopandisha hamasa zaidi ya kisiasa, na wapiga kura kuliko chama chochote. Kazi hiyo cdm iliifanya toka 2010 baada ya uchaguzi, mpaka 2015. Lowasa alikuwa kama mfungaji aliyebaka na goli wazi, kisha afunge kwa Madaha, halafu unataka awe nyota wa mchezo, kisa kafunga goli pekee la ushindi?
Kudhibitisha uko na hoja ya kupika, nimekuambia kama yeye ndio alileta kura 6m+ akiwa ni miezi miwili, taja alileta viti vingapi akiwa na miaka miwili. Au taja idadi ya matawi aliyofungua ndani ya hiyo miaka miwili, naona unazunguka tu.
Tuje kwenye hili la uchaguzi wa 2020. Magufuli kama Magufuli sio muumini wa box la kura, na ameshinda mara chache mno kwa njia ya box la kura, tena hata huko alifanya figisu zote. Wakati akifanya hayo alikuwa ni waziri tu, je leo hii ni rais, kwa katiba hii mbovu unategemea aheshimu box la kura?
Tuje kwenye mifano halisi wa kitakachotokea kwenye uchaguzi huu. Nitajie toka Magufuli ameingia madarakani ni lini kumewahi kufanyika uchaguzi wa kweli? Kwa macho yangu nimeona ukatili, ushenzi na uhayawani wa wazi ili ccm watangazwe washindi kwenye chaguzi za marudio. Yote haya yamefanyika kwa utaratibu wa jeshi la polisi na tume ya uchaguzi. Nimeona wasimamizi wa uchaguzi wakifunga ofisi zao ili kukwepa kupokea fomu za wapinzani, hatimaye mgombea wa ccm apite bila kupingwa. Ukifuatilia mbinu hizi, zote ndio alizokuwa akitumia Magufuli huko nyuma kupata ubunge.
Hayo hapo juu nimeyataja kwa uchache, lakini funga kazi ya tabia za Magufuli kwenye chaguzi za nchi hii, ilikuwa ni kwenye uchaguzi wa SM. Wote tuliona uchaguzi uliokosa heshima na ushenzi wa kiwango cha juu kutokea ndani ya chaguzi za nchi hii. Sina chochote cha kuongea maana matokeo yalikuwaje, na ushindi wa ccm ulipatikaneje kila mtu anajua. Kinachosaidia mpaka sasa kwa hali hii kutokea ni ukondoo wa watanzania. Jaribu kufuatilia mwenendo wa uchaguzi wa October, kote huko tayari kimeandaliwa mazingira ya kufanikisha uchaguzi wa hujuma na ushenzi wote unaoufahamu wewe. Ndio maana asasi zote zinazofahamika kwa kusema ukweli zimezuiwa kuangalia uchaguzi, na taasisi zote na waangalizi wa kimataifa wanaoweza kusema kweli wamezuiwa! Hivyo uchaguzi wa 2020 utakuwa ni wa tabia binafsi za Magufuli dhidi ya upinzani. Kama kweli unasimama kwenye ukweli, basi huo ndio ukweli.