Cdm haikuwa na tatizo la wapiga kura, usitake kumpa sifa asizostahili. Watu tulijiandikisha kwa hasira tukijua Lowasa angekuwa mgombea wa ccm, ila viongozi wa Cdm wakampa Lowassa nafasi baada ya kupigwa chini huko ccm. Kama Lowassa ndio alileta kura 6m+ akiwa na miezi miwili, sema alileta viti vingapi vya ubunge na udiwani akiwa na miaka miwili? Au hata alifungua matawi mangapi ya cdm?
Hizo kura 6m angezipeleka TLP tungekuelewa. Ni kweli safari hii cdm wanaweza wasipate hata jimbo moja, ila sio kwakuwa haina wapiga kura, bali ni kwakuwa Magufuli kwa kutumia madaraka yake vibaya, ataagizwa watoa rushwa wa ccm kutangazwa washindi na tume isiyo huru ya uchaguzi.