Kifaurongo
JF-Expert Member
- Jan 18, 2010
- 4,221
- 2,359
Mwambieni Nyarandu, pamoja na kupata 100%, hawa ndio WAJUMBE wa baraza kuu. 😂😂😂????
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwambieni Nyarandu, pamoja na kupata 100%, hawa ndio WAJUMBE wa baraza kuu. 😂😂😂????
Hata selikali iliyopo inapenda na ku ukubali, muulize makonda na sakata lake kutokomeza ushoga, je selikali ilifanyaje? Utapata jibu acha kubwabwaja, jikite kwenye hoja.Mnapenda ushoga?
Mkuu hizo ni kura za awali, japo matamanio yako ni Lissu kutokurudi. Kwanza ufahamu Lissu harudi kwa ajili ya kugombea urais maana sio mkimbizi wa kisiasa, bali anarudi baada ya matibabu. Isitoshe mkutano wa mwisho bado, na hata cdm wakikosea wakampitisha Nyalandu, basi watakuwa wamejikaanga wenyewe. Sisi wapiga kura wengi wa upinzani hatuna imani na mwanaccm yoyote, bali tuna imani na Lissu.
Kwahiyo hao wajumbe wawe makini na maamuzi yao, maana sisi wapiga kura wa upinzani tunajitambua, na hatukoa tayari kurudia kosa la Lowassa.
Hakuna wa kumshinda Nyalandu hapo Ufipa!
Hata selikali iliyopo inapenda na ku ukubali, muulize makonda na sakata lake kutokomeza ushoga, je selikali ilifanyaje? Utapata jibu acha kubwabwaja, jikite kwenye hoja.
Karma ya 2015 itaendelea kutafuna kizazi na kizazi Cha CDM .Mkuu hizo ni kura za awali, japo matamanio yako ni Lissu kutokurudi. Kwanza ufahamu Lissu harudi kwa ajili ya kugombea urais maana sio mkimbizi wa kisiasa, bali anarudi baada ya matibabu. Isitoshe mkutano wa mwisho bado, na hata cdm wakikosea wakampitisha Nyalandu, basi watakuwa wamejikaanga wenyewe. Sisi wapiga kura wengi wa upinzani hatuna imani na mwanaccm yoyote, bali tuna imani na Lissu.
Kwahiyo hao wajumbe wawe makini na maamuzi yao, maana sisi wapiga kura wa upinzani tunajitambua, na hatukoa tayari kurudia kosa la Lowassa.
Acheni demokrasia ichukue mkondo.Dua la kuku hilo .Hakuna Mungu aweza mlaani mtu kwa kutumia uhuru wake wa demokrasia ya kupiga kura!!Mjumbe yeyote wa chadema atakaye mpigia kura Nyarandu apitishwe kugombea urais kwa ticket ya CDM huyo mjumbe na alaaniwe milele yote
Acheni demokrasia ichukue mkondo.Dua la kuku hilo .Hakuna Mungu aweza mlaani mtu kwa kutumia uhuru wake wa demokrasia ya kupiga kura!!
Ni ajabu sana kamati kuu ya CHADEMA inaamini kuwa Nyalandu ni bora kuliko Lissu
Sasa kama kamati kuu yenyewe haiamini kuwa Lissu hastahili kuwa namba moja kwenye urais, kwa nini sisi wananchi tuamini kuwa yeye anafaa kuwa Rais?
Hizi kura za kamati kuu zimetuma meseji kwa wananchi na kwa Wanachadema wote kuwa Uongozi wa Chadema hauamini kuwa Lissu hafai kuwa rais licha ya kuwa ameonekana kuwa ni mwenye kutajwa tajwa zaidi na wananchi.
Nani anateswa na kichaa!!?Mi Lumumba Lisu anawatesa sanaa
Mkuu J5 sio mbali ndo utajua namaanisha ..sitaki ujue mm ni nani lkn chukua hii...Lissu ndo mgombea kwa 99.9%
Kama kuna mtu ataendelea kubishana na wewe mkuu tindo baada ya maelezo haya mazuri ya hoja,huyo atakuwa na tatizo ubongoni mwake.Sina tatizo na maoni yako, ila umekuja na hoja ambayo inabebwa na mahaba niue zaidi. Ni kweli nina mapungufu, ila sio hayo uliyoyaweka wewe. Umekuja na mchango kuwa Lowassa ndio alileta kura cdm uchaguzi wa 2015. Wakati ninajua fika 2015 cdm ndio ilikuwa chama cha kisiasa kilichopandisha hamasa zaidi ya kisiasa, na wapiga kura kuliko chama chochote. Kazi hiyo cdm iliifanya toka 2010 baada ya uchaguzi, mpaka 2015. Lowasa alikuwa kama mfungaji aliyebaka na goli wazi, kisha afunge kwa Madaha, halafu unataka awe nyota wa mchezo, kisa kafunga goli pekee la ushindi?
Kudhibitisha uko na hoja ya kupika, nimekuambia kama yeye ndio alileta kura 6m+ akiwa ni miezi miwili, taja alileta viti vingapi akiwa na miaka miwili. Au taja idadi ya matawi aliyofungua ndani ya hiyo miaka miwili, naona unazunguka tu.
Tuje kwenye hili la uchaguzi wa 2020. Magufuli kama Magufuli sio muumini wa box la kura, na ameshinda mara chache mno kwa njia ya box la kura, tena hata huko alifanya figisu zote. Wakati akifanya hayo alikuwa ni waziri tu, je leo hii ni rais, kwa katiba hii mbovu unategemea aheshimu box la kura?
Tuje kwenye mifano halisi wa kitakachotokea kwenye uchaguzi huu. Nitajie toka Magufuli ameingia madarakani ni lini kumewahi kufanyika uchaguzi wa kweli? Kwa macho yangu nimeona ukatili, ushenzi na uhayawani wa wazi ili ccm watangazwe washindi kwenye chaguzi za marudio. Yote haya yamefanyika kwa utaratibu wa jeshi la polisi na tume ya uchaguzi. Nimeona wasimamizi wa uchaguzi wakifunga ofisi zao ili kukwepa kupokea fomu za wapinzani, hatimaye mgombea wa ccm apite bila kupingwa. Ukifuatilia mbinu hizi, zote ndio alizokuwa akitumia Magufuli huko nyuma kupata ubunge.
Hayo hapo juu nimeyataja kwa uchache, lakini funga kazi ya tabia za Magufuli kwenye chaguzi za nchi hii, ilikuwa ni kwenye uchaguzi wa SM. Wote tuliona uchaguzi uliokosa heshima na ushenzi wa kiwango cha juu kutokea ndani ya chaguzi za nchi hii. Sina chochote cha kuongea maana matokeo yalikuwaje, na ushindi wa ccm ulipatikaneje kila mtu anajua. Kinachosaidia mpaka sasa kwa hali hii kutokea ni ukondoo wa watanzania. Jaribu kufuatilia mwenendo wa uchaguzi wa October, kote huko tayari kimeandaliwa mazingira ya kufanikisha uchaguzi wa hujuma na ushenzi wote unaoufahamu wewe. Ndio maana asasi zote zinazofahamika kwa kusema ukweli zimezuiwa kuangalia uchaguzi, na taasisi zote na waangalizi wa kimataifa wanaoweza kusema kweli wamezuiwa! Hivyo uchaguzi wa 2020 utakuwa ni wa tabia binafsi za Magufuli dhidi ya upinzani. Kama kweli unasimama kwenye ukweli, basi huo ndio ukweli.
Unazungumzia elimu kwa maana ya kuelimika au elimu kwa muktadha wa vyeti!?Mkuu sijui unalifahamu hili:
"Adui yako wa kisiasa akimpatia unatakiwa umpige sana achakaye kiasi ambacho hata atakapo pata nafasi ya kurudisha ngumi zake, basi ngumi hizo ziwe hazina madhara kwako".
Na hii ndio uhalisia wa mapigo ya siasa ambayo Chadema anapambana nayo..
"Wakati unamshambulia adui yako wa kisiasa, hakikisha Magenerali wengine wako imara na wakishambulia na kutoa kipigo maeneo yote ambayo anaweza kupata usaidizi, au kukimbia kabla hajapigwa sana na kuchakazwa".
Sasa Mkuu uendeshaji vita ya kisiasa wa Chadema ni wa kitoto mpaka muda huu na sababu kubwa ni kuto kuwa makini katika kuteuwa Magenerali ambao wamebobea katika nyanja za vita. Angalia Uongozi wa juu kabisa wa Chadema unakufahamisha kuwa vita wanayoweza ni vita ya nguvu na sio uwezo wa kubobea wa akili.
Nakuuliza na napenda uwe mkarimu kwa hili , unijibu jinsi akili yako inavyo kutuma na kwa hili nitajuwa tunabadilishana ufahamu wa pamoja na nani kwa kiwango gani?.
Ukipewa au Dr Magufuli au Mbowe, Nani atakuwa mwenyekiti wako?
Ukipewa Dr Bashiru amd Mnyika nani kati ya hao utapenda katibu mkuu wako?
Ukipewa Dr. Rodrick Mpogolo au Benson Kigaila nani utapenda awe Naibu katibu Mkuu wako ?
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Chadema Salum Mwalim na CCM Dr Abdalah Juma?
Pole pole au Makene ?
Utachagua nani katika hizo nafasi zao kuzingatia weledi na ufahamu.
Unapokuwa na chama ambacho viongozi wenye Elimu ya kutosha na uwezo mpana wa kufikiria, unatengeneza Magenerali ambao kila mmoja ana uwezo wa kupigana vita kwa kiwango cha juu kabisa.
Ogopa Chama ambacho, Mwenyekiti Elimu ya Kuunga, Katibu Mkuu pia, Naibu manaibu makatibu wakuu hivyo hivyo, (Uongozi wa juu kabisa hata mwenye Degree hata iwe moja hakuna kwa dunia ya leo) Iwe bara au Visiwani. lazima kuna matatizo labda kwa leo uniambie Upevu wa Elimu sio lazima.
Huwezi kuwa na safu ya juu kabisa ya uongozi ambayo Elimu hakuna na ndio unawapa tochi ya kumulikia watu wawafuate , lazima wafuasi watakuwa na matatizo mkichwa.
90% ya waliorudi ccm ni wale waliotoka ccm. Sio kwamba walifukuzwa, bali walikosa nafasi huko ccm, wakaona wajitoe kuja cdm. Nyalandu hana record nzuri ya utendaji toka ccm, hivyo akiwa mgombea wa Cdm huku dola ikijua madhambi yake, ni rahisi kumbana mpaka asalimu amri kama Lowassa na Sumaye. Narudia tena, ni nadra sana mwanaccm yoyote, tena aliye na record yenye makandokando kuacha uanaccm wake, ccm ikiwa madarakani, regardless kaondokaje ccm.
Hilo la Lissu kuwekewa vikwazo kutokana na kesi za kubambikiwa tunalifahamu vizuri sana. Lakini sio kigezo cha kuwa na mtu ambaye tuna mashaka naye ya dhahiri, na mifano ya watu wa ccm kama yeye ipo wazi. Hiyo demokrasia unayosema nataka kulazimisha, ndio demokrasia hiyo hiyo hutaki mimi niitumie kumkataa mtu. Sina popote nimewashikia watu bunduki wamkatae Nyalandu, bali nashawishi na sababu naziweka wazi.
Wakuu hili suala la Lissu na Mwenyekiti kwa maono ya kawaida ni suala dogo sana lakini KISIASA na KIUTAWALA WA VYAMA sio suala jepesi hivyo.
KISIASA: Mashambulizi makali ya CCM kuelekeza Chadema yametokana na siasa ambazo Lissu amekuwa akiendesha kumwelekezea Mkulu na hata uhoi wa Chadema leo ni Mchango hasi wa Mh. Lissu kichama.
Tukitaka Chadema ipotee kwenye ramani ya siasa za uwakilishi ni turuhusu Mh Lissu agombee Urais na ashindwe. Kwa mfumo wa siasa zake ushiriki wake utaacha donda ambalo kama atashindwa CCM basi watahakikisha watafanya kila wawezalo wafute Siasa za uwakilishi za Chadema Tanzania.
Kwa hali ya Chama ilivyo leo tunatakiwa kukubaliana kuwa gonjwa zito limeipitia Chadema na lazima tujipe muda wa kutosha kuponya maumivu. Kwa upande huo Yeyote mwenye siasa za kupoa ili tuweze kuponya majeraha anaweza kuwa wa msaada sana kwetu.
KIUTAWALA WA VYAMA: Chama chochote kizuri huendeshwa kwa vikao, na vikao hutoa nafasi ya kila mjumbe atoe hoja na nyongo. Na katika vikao watu wa aina mbili huangaliwa sana.
1) Wajumbe ambao michango yao katika mijadala hubalisha mwelekeo na muono kichama.
2) Wajumbe ambao wanaushawishi mkubwa na huvutia wajumbe katika kupiga kura za maamuzi hata kama maamuzi hayo ni magumu kuyatekeleza.
Sasa kitu ambacho hatujui LISSU yuko kwenye upande gani kuhukumiwa, ila tusione maamuzi ya Chama ni mapesi ya ama kumuunga mkono Nyalandu, au LISSU kwa uchaguzi huu wa 2020. NAWAKILISHA
Kwani kinachoamua nani agombee urais ni wapiga kura (wajumbe) au wanachama?Mkuu hizo ni kura za awali, japo matamanio yako ni Lissu kutokurudi. Kwanza ufahamu Lissu harudi kwa ajili ya kugombea urais maana sio mkimbizi wa kisiasa, bali anarudi baada ya matibabu. Isitoshe mkutano wa mwisho bado, na hata cdm wakikosea wakampitisha Nyalandu, basi watakuwa wamejikaanga wenyewe. Sisi wapiga kura wengi wa upinzani hatuna imani na mwanaccm yoyote, bali tuna imani na Lissu.
Kwahiyo hao wajumbe wawe makini na maamuzi yao, maana sisi wapiga kura wa upinzani tunajitambua, na hatukoa tayari kurudia kosa la Lowassa.
Kumbe una jua kuwa upo, na selikali ime ukubali basi kuwa mpole, acha porojo jikite kwenye mada.Nyie wapinzani si mlikuwa mnaushangilia baada ya mabeberu kulalamika, mpaka mgombea wenu akasema sasa anauruhusu lasmi akichaguliwa,
Ni bora wa kujificha kuliko huo wa lasmi.
Unazungumzia elimu kwa maana ya kuelimika au elimu kwa muktadha wa vyeti!?
Sent using Jamii Forums mobile app