Baada ya Oktoba 25, Mbowe atang'olewa uenyekiti wa CHADEMA?

Baada ya Oktoba 25, Mbowe atang'olewa uenyekiti wa CHADEMA?

Huyu jamaa ni ccm leo anaongelea chadema! Ama kweli kutumika kama -ndomu ni shida.

Kwa taarifa,Mh.Mbowe atakuwa waziri mkuu wakati huo so itabidi amkabidhi mwingine kijiti cha uenyekuti.
 
makamanda wa ukweli hawarushi ngumi gizani...bila shaka wewe ni nyumbu. makamanda wa kweli wanajibu hoja kwa hoja sio kuhorojoka na matusi.

Hapo kuna hoja gani ya kujibu wee msee...wewe ccm cdm inakuhusu nn!
 
Huyu jamaa ni ccm leo anaongelea chadema! Ama kweli kutumika kama -ndomu ni shida.

Kwa taarifa,Mh.Mbowe atakuwa waziri mkuu wakati huo so itabidi amkabidhi mwingine kijiti cha uenyekuti.

Jitahidi kusoma kilichoandikwa na kukielewa kabla ya kuja kujibu thread.
 
Chakaza wewe ni mkongwe humu sitegemei ujibu kirahisirahisi namna hii.

Haya ndiyo yanayowakumba Chadema na Ukawa kwa sasa.Yalishatabiriwa!

Kwa sababu unani shangaza, hivi tuwe wakweli kabisa, kwa misimamo ya Mbowe jee sio mwiba kwa utawala wa ccm? Kwa hiyo jambo la kuondolewa madarakani lingekuwa heri sana kwao na nina hakika hayo ndio matamanio yao, na wewe umeleta story hii kwa matamaniyo hayo na sii uhalisia. Mbona wafuatiliaji wa ndani wa chama chenyewe hawalijui hilo uliloamka nalo?
 
Last edited by a moderator:
Hilo linajulikana ila hafai tena

Vipi unashaurije! Akiondolewa Mbowe tumrudishe Zitto? Na jee atakuja na ACT yake? (Maana ile ni personal property yake ndio maana nasikia hata picha ya mgombea haiwekwi inawekwa ya CEO)
 
Hangaika na nani atakuwa mwenyekiti Wa Ccm baada ya uchaguzi, Kama ccm itakuwepo Tena kwenye duru za siasa hapa Tanzania au itakua ahera! Freeman Mbowe, kamanda Wa anga, Ardhi na Baharini; atatunukiwa nishani ya "Mwanasiasa kijana JASIRI Wa karne" na kupewa heshima ya Mwenyekiti Wa maisha hâta Kama huko tuendako atakabidhi kijiti kwa kamanda mwingine.



Baada ya Oktoba 25 wanachama wa chadema asili wanajipanga kukirudisha chama chao kutoka mikono ya familia ya Mtei na kukifanya kuwa taasisi ya umma kwa kuwa inatumia ruzuku za serikali.


Ni wazi Mbowe anaonekana kujutia uamuzi wake wa kubadili gear angani,uamuzi ambao umeigharimu chadema kwa kumpoteza shujaa wa ujenzi wa upinzani wa kweli Tanzania ndugu Dr Slaa.

Ni ukweli usiojificha kwa wanachama wa chadema asili wametaharuki na kushangaa chama chao kutekwa na wahuni au makapi yaliyoisumbua ccm hadi Kikatio cha Mangula kilipotumika.

Wanachama wa chadema asilia wamelazimika kuirudisha ccm madarakani kwa kosa kubwa la kiitifaki lililoamuliwa na familia moja tu ndani ya chama.

Wanachama wa chadema asilia ni wazi wanatafakari hasa baada ya ushindi wa kishindo wa Magufuli ni kwa vipi wanaweza kukinusuru chama chao kisiporomoke kama NCCR,CUF na TLP.

Wanachadema asilia wanatafuta mwenyekiti kwani haiwezekani Wangwe,Arfi,Zitto,Kitila,Mwigamba na Slaa wakawa na matatizo...tatizo ni mwenyekiti na akiendelea kuchekewa chama kitafutika kwenye ramani ya kisiasa.

Wanachadema asilia wanatambua wanayo haki ya kisheria ya kukiondoa chama mikononi mwa familia ya mtei.

Wanachadema asilia wanataka kuona mfumo wa uteuzi wa wagombea ndani ya chama unakuwa wazi na kufuata taratibu za chama.

Wanachadema asilia wanataka kuona mgao wa ruzuku unakuwa fairly distributed na sio kuwafikia baadhi ya wanaojidai makamanda kutoka kaskazini.

Ni katibu aliyeondolewa na Mbowe ndio aliyetuelekeza kwenda mitaani na vijijini ili kukikuza chama na aliahidi kutupima kwa hilo.leo hii Mbowe amemfanya katibu ni mvivu.

Wanachadema asilia hawajapewa fursa rasmi ya kumpitisha lowassa kuwa mgombea urais kupitia chadema.hili limefanyika kiujanjaujanja kwa kuwa Mwenyekiti anajua wanachama wangelipinga kwani mgombea huyu hana sifa za kikamanda wala hajui misingi ya kuwa kamanda wa wananchi wanyonge.

Wanachadema asilia hawakupewa fursa ya kuamua au kujua jinsi gani mchakato wa kuachiana majimbo utakavyokuwa.sana sana mchakato ulisikika kwenye vyombo vya habari tu.

Wanachadema asilia walijitoa kwa hali,mali na uhai wao kwa kutarajia Tanzania mpya inazaliwa ikiwa haina ufisadi,uongo,udini,ukanda,ufamilia,ukabaila na usaliti badala yake Mwenyekiti na timu ya wachache imetuletea mamluki wanaokichafua chama na kukiacha kikiwa vipande vipande.

Kwa heshima ya Wangwe,Zitto,Slaa,Arfi,Kitila,Kafulila na wengine ni lazima Mwenyekiti uondolewe kwani wewe ndio tatizo.Mwenyekiti umebebwa sana na think tanks ndani ya Chadema na malipo yao yamekuwa ni kuwafukuza tu.

Mwisho wa Mbowe kuwa mwenyekiti Chadema ni oktoba 25.


SENT AS RECEIVED!
 
Back
Top Bottom