Baada ya Ole Nasha kufariki ni wakati wa Mkataba wa bandari ya Bagamoyo kuwa wazi

Baada ya Ole Nasha kufariki ni wakati wa Mkataba wa bandari ya Bagamoyo kuwa wazi

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Waziri Ole Nasha ndiye aliyekuwa waziri ambaye kapewa majukumu ya ufuatiliaji wa mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo wenye makadirio ya thamani $10B. Watanzania wengi ni lazima tujiulize huyu waziri kijana kuondoka katika mazingira haya akiwa katikati ya mkataba mkubwa hivi.

Kwa kutoa Watanzania wasiwasi na kuzingatia tajari tulishaambiwa kuna madudu mengi sana kwenye huu mkataba. Lakini China nayo imekuwa ikisema kusuhu kuwa na base za kijeshi kwenye bandari zao ni lazima mkataba uwe wazi ili Watanzania wote tujue tunaingia kwenye mkataba wa namna gani. Wakina Samia na Kikwete hawatakuwepo pale China ikipewa bandari kwa miaka 99 na bandari kuwa kama balozi hivyo China kufanya wanalotaka.

Pamoja na mambo ambayo hatuyajui ni
1. Kuna umuhimu gani wa kuwa na bandari tatu karibu ya Tanga, Dar na hii ya Bagamoyo
2. Bandari ya Bagamoyo watarudisha vipi uwekezaji wa $10B bila kuchukuwa mizigo ya bandari ya Dar!. Je itawezekana vipi hizi bandari mbili kuongeza mizogo kwa zote!?. Na bandari ya Dar kuna mtu anafikiri watapata tena mizigo ya kutoka China?.
3 Tujue China ni kama inatawala shaba kule Zambia ndiyo mjenzi wa Tazara Je mizigo ya Zambia itaendelea kupitia bandari ya Dar au Bagamoyo?

Ukiangalia vizuri hii bandari ya bagamoyo ni mradi wa watu wachache. Hivyo viwanda wanavyosema watajenga sio viwanda ni magodauni ya kuweka mizigo huo ndiyo ukweli. Hakuna kiwanda eti kinasubiri bandari kwasababu Tanzania tuna bandari na maeneo ya ujenzi sasa hivi. Lakini kuna pesa ya mafuta na bomba linaenda Tanga ni kwanini tusikuzi pale ambapo tayari tuna uhakika wa soko kubwa na pesa? Tanga kuna umbali gani???! Na hii ingefanya bandari zote bado ziwe chini ya TPA. Hii bandari ya Bagamoyo haitakuwa ya TPA tujue hilo.

Msishangae mtoto wa Kikwete kualikwa China eti kwenye mafunzo na kuacha wabunge wengine wenye uzoefu. Hii yote ni mradi wa bandari na hawa Kikwetes tuwe nao makini sana. Vilevile tusiwaamini wapinzani kwenye hili China wanauwezo wa kuhonga mpaka upinzani. Kitu kimoja tu tunaomba ni uwazi mkataba wekeni hapa na sio kutudanganya kwa mambo ya kazi. Vilevile Ole Nasha kufariki ni kitu cha kujiuliza sana maana tunasikia alianza kupinga mambo mengine.

Niongezee haya maswali
1. Na hapa ndiyo tunapishana maana mkataba hauko wazi bandari itakuwa ya nani?
2. Je $10B ni mkopo au ni wezezaji kama Mo wa Simba?
3. Je tunawamilikisha wachina uendeshaji wa bandari Je uendeshaji ukiwa mbovu tutafanyaje? tunaweza kufukuza management na kuweka nyingine kama hao CEO wengine au?
4. Vitu gani ambavyo hatutaruhusu China wafanye? mfano meli ya kijeshi ya USA itaruhusiwa kupiga nanga kwenye bandari hii kama wamekuja kufanya shughuli za kijeshi na JWTZ?
5. Wanasema wanajenga viwanda tunaomba list ya viwanda ambavyo wanavijenga na ni kiasia gani cha $10B ni viwanda? au watakuwa wanauza viwanja kwa wawekezaji wengine . Hapa tusipokuwa makini patajegwa magodown tu!
6. Kwenye matumizi na uhakiki wa ujenzi ni kampuni gani ina hakiki gharama za ujenzi? Nani anaiteua hii kampuni Tanzania au China?
7. Je ni vifaa gani vya ujenzi kama chuma, cement ..... vitatoka Tanzania?
 
Hizi ndizo akili tunataka watanzania. Kwa nyongeza sharti ya hii bandari ni kufunga bandari zingine zote kwenye eneo fulani la umbali. Anayebisha aweke mkataba hapa tuuone.

Jk na ggenge lako tumekuchoka. Kwa ufupi hatukutaki. Kaa mbali na serikail yetu pendwa. Ulipewa miaka mitano ya kupita bila kuchujwa kwenye kamati ya maadili, bado ukavurunda, ukajiongezea mitano kwa ubabe ili ulinde kiburi na udanganyifu wako, ukaizika nchi. Sasa unarudi kwa hila ili ufanye nini na kwa mujibu wa katiba gani?

Tunaheshimu na kuthamini amani yetu, hivo usisuone watanzanai ni wapumbavu.
She is much more competent without your hands.
 
Sasa hivi mnaangaika sana mnazusha kila uongo ili muhalalishe mnachokizua hii haisaidii chochote zaidi ya kuchonganisha watu, halafu ebu weka angalau ile mikataba ya ununuzi wa ndege na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato uliyowahi kuoneshwa na yule bwana wenu mnayempiginia wacha mikataba mingine iliyoingiwa na huyo mnayemuabudu na kumuona ni Mungu mtu halafu ndio mdai hiyo mingine.
 
Mi napata wakati mgumu hasa nikijaribu kuchungulia ambao hawapo kwenye zile nafasi ambao walikataa ile proposal ya awali.

Kamati ya majadiliano ilikuwa chini ya Prof. Kabudi wakati wajumbe wakiwa

1. Engineer Mfugale
2. Dkt. Chamuriho
3. Engineer Kakoko
4. Dkt Kilangi (Alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali)

Ao wote hawapo leo kwenye zile nafasi na ukiangalia iyo list unaweza kuona kwanini ule mradi ulikataliwa sasa sijui wanasiasa watokaokuwa kwenye kamatu ya sasa ya mazungumzo.
 
Huna akili.

Yaani unasema kuwa bandari tulizo nazo zina tosha?

Ndiyo kwasababu upanuzi unaendelea mfano bandari ya Tanga kuna itakuwa inasafirisha mafuta ya Uganda sasa kwanini isikuzwe hii ? Bandari ta Dar imeanza kupanuliwa kuanzia wakati wa Magu . Mtwara inapanuliwa zaidi. Ingepeza kama utajibu maswali yangu
 
Ndiyo kwasababu upanuzi unaendelea mfano bandari ya Tanga kuna itakuwa inasafirisha mafuta ya Uganda sasa kwanini isikuzwe hii ? Bandari ta Dar imeanza kupanuliwa kuanzia wakati wa Magu . Mtwara inapanuliwa zaidi. Ingepeza kama utajibu maswali yangu
Mzee watu wanaangalia soko la kongo rwanda burundi etc.

Wewe unakomaa na soko la ndani?
Amka brother .
 
Back
Top Bottom