Baada ya Ole Nasha kufariki ni wakati wa Mkataba wa bandari ya Bagamoyo kuwa wazi

Baada ya Ole Nasha kufariki ni wakati wa Mkataba wa bandari ya Bagamoyo kuwa wazi

Sasa hivi mnaangaika sana mnazusha kila uongo ili muhalalishe mnachokizua hii haisaidii chochote zaidi ya kuchonganisha watu, halafu ebu weka angalau ile mikataba ya ununuzi wa ndege na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato uliyowahi kuoneshwa na yule bwana wenu mnayempiginia wacha mikataba mingine iliyoingiwa na huyo mnayemuabudu na kumuona ni Mungu mtu halafu ndio mdai hiyo mingine.

Tusisahau watanzania ni karibia mil 60. Tuache mambo ya kukopa au kuanzisha miradi ya kuneemesha watu wachache tu.
Hivi hatukomi kuanzisha kashfa zisizoisha?
 
Waziri Ole Nasha ndiye aliyekuwa waziri ambaye kapewa majukumu ya ufuatiliaji wa mkataba wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo wenye makadirio ya thamani $10B. Watanzania wengi ni lazima tujiulize huyu waziri kijana kuondoka katika mazingira haya akiwa katikati ya mkataba mkubwa hivi.

Kwa kutoa Watanzania wasiwasi na kuzingatia tajari tulisha ambiwa kuna madudu mengi sana kwenye huu mkataba. Lakini China nayo imekuwa ikisema kusuhu kuwa na base za kijeshi kwenye bandari zao ni lazima mkataba uwe wazi ili Watanzania wote tujue tunaingia kwenye mkataba wa namna gani. Wakina Samia na Kikwete hawatakuwepo pale China ikipewa bandari kwa miaka 99 na bandari kuwa kama balozi hivyo China kufanya wanalotaka.

Pamoja na mambo ambayo hatuyajui ni

1. Kuna umuhimu gani wa kuwa na bandari tatu karibu ya Tanga, Dar na hii ya Bagamoyo
2. Bandari ya Bagamoyo watarudisha vipi uwekezaji wa $10B bila kuchukuwa mizigo ya bandari ya Dar!. Je itawezekana vipi hizi bandari mbili kuongeza mizogo kwa zote!?. Na bandari ya Dar kuna mtu anafikiri watapata tena mizigo ya kutoka China?.
3 Tujue China ni kama inatawala shaba kule Zambia ndiyo mjenzi wa Tazara Je mizigo ya Zambia itaendelea kupitia bandari ya Dar au Bagamoyo?

Ukiangalia vizuri hii bandari ya bagamoyo ni mradi wa watu wachache. Hivyo viwanda wanavyosema watajenga sio viwanda ni magodauni ya kuweka mizigo huo ndiyo ukweli. Hakuna kiwanda eti kinasubiri bandari kwasababu Tanzania tuna bandari na maeneo ya ujenzi sasa hivi. Lakini kuna pesa ya mafuta na bomba linaenda Tanga ni kwanini tusikuzi pale ambapo tayari tuna uhakika wa soko kubwa na pesa? Tanga kuna umbali gani???! na hii ingefanya bandari zote bado ziwe chini ya TPA. Hii bandari ya Bagamoyo haitakuwa ya TPA tujue hilo.

Msishangae mtoto wa Kikwete kualikwa China eti kwenye mafunzo na kuacha wabunge wengine wenye uzoefu. Hii yote ni mradi wa bandari na hawa Kikwetes tuwe nao makini sana. Vilevile tusiwaamini wapinzani kwenye hili China wanauwezo wa kuhonga mpaka upinzani. Kitu kimoja tu tunaomba ni uwazi mkataba wekeni hapa na sio kutudanganya kwa mambo ya kazi. Vilevile Ole Nasha kufariki ni kitu cha kujiuliza sana maana tunasikia alianza kupinga mambo mengine.
Sukuma gang bana....
 
Tuache siasa ndugu....tuje kwenye hoja za msingi.....Tanzania ni yetu sote.......
Tuache ujinga wa kuwa na dhana mbaya na kubeza kila linalofanywa na utawala uliopo na kutaka kuaminisha watu tena kwa nguvu kwamba eti ni Magufuli tu ndiye aliyekuwa na nia njema na nchi hii na kwamba wengine wote ni wapigaji tu,huko ni kumkufuru na kumkosea mwenyezi Mungu kwani mwenyezi Mungu kama aliweza kumuumba huyo Magufuli atashindwaje kuumba wengine kama yeye?
Binafsi naamini utendaji kazi wa Rais Samia ni wa makini na ni wenye lengo la kuleta manufaa kwa taifa na wananchi wake kwa ujumla hivyo sikubaliani na upuuzi wowote unaeletwa na mtu yeyote kwa sababu ya chuki zake binafsi.
Najua hivi sasa kuna vita kubwa inayoendelea baina ya makundi fulani fulani kwa sababu ya utashi wao binafsi tu na wengine wamekuwa wakipinga utawala wa Rais Samia lakini huwezi kuwasikia wakizisema wazi sababu zao(halisi) bali wao wamebaki tu kujificha kwenye box la "uzalendo".
Watu hawa ndio wamekuwa vinara wa kuzua uongo kila kukicha ili tu watimize kile wanachokusudia,
Watu hawa ni sawa na chui waliojivika ngozi ya kondoo,
Watu hawa ukiwatizama usoni wanajionesha tofauti na walichokificha ndani ya mioyo yao.
Hawa watu ni wanafiki na ni wabinafsi na ni watu hatari sana.
 
Mimi sijwahi kuona Mkataba ulio wazi na wakauweka mahali nikausoma kama mwananchi
Nasubiri niuone mkataba huu kabla haujasainiwa
Au sijui watauweka live
Natania kukiwa na ukweli ndani yake
Hakuna mkataba wa wazi kwetu tusijidanganye never
 
Sasa hivi mnaangaika sana mnazusha kila uongo ili muhalalishe mnachokizua hii haisaidii chochote zaidi ya kuchonganisha watu, halafu ebu weka angalau ile mikataba ya ununuzi wa ndege na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato uliyowahi kuoneshwa na yule bwana wenu mnayempiginia wacha mikataba mingine iliyoingiwa na huyo mnayemuabudu na kumuona ni Mungu mtu halafu ndio mdai hiyo mingine.
Wanatia huruma sana chato gang😂😂😂

Naibu Waziri hata sio mjumbe wa Baraza la Mawaziri sasa mtu amuue kwa sababu gani?😂😂😂

Poleni sana chato gang uzandiki wenu unashtukiwa mapema
 
Wanatia huruma sana chato gang😂😂😂

Naibu Waziri hata sio mjumbe wa Baraza la Mawaziri sasa mtu amuue kwa sababu gani?😂😂😂

Poleni sana chato gang uzandiki wenu unashtukiwa mapema
Ni vita vya kimaslahi maana toka mtu wao afe wapo baadhi wamepoteza fursa za kujinufaisha kutokana na upendeleo waliokuwa wakiupata sasa wanateseka lakini wanajificha kwenye kichaka cha kujiita wazalendo kumbe uzalendo wenyewe ni yale maslahi yao binafsi.
 
Mi napata wakati mgumu hasa nikijaribu kuchungulia ambao hawapo kwenye zile nafasi ambao walikataa ile proposal ya awali.

Kamati ya majadiliano ilikuwa chini ya Prof. Kabudi wakati wajumbe wakiwa

1. Engineer Mfugale
2. Dkt. Chamuriho
3. Engineer Kakoko
4. Dkt Kilangi (Alikuwa mwanasheria mkuu wa serikali)

Ao wote hawapo leo kwenye zile nafasi na ukiangalia iyo list unaweza kuona kwanini ule mradi ulikataliwa sasa sijui wanasiasa watokaokuwa kwenye kamatu ya sasa ya mazungumzo.
Huenda familia ya Kikwete ndo wajumbe na wachumia tumbo kadhaa.
 
Tuache ujinga wa kuwa na dhana mbaya na kubeza kila linalofanywa na utawala uliopo na kutaka kuaminisha watu tena kwa nguvu kwamba eti ni Magufuli tu ndiye aliyekuwa na nia njema na nchi hii na kwamba wengine wote ni wapigaji tu,
Huko ni kumkufuru na kumkosea mwenyezi Mungu kwani mwenyezi Mungu kama aliweza kumuumba huyo Magufuli atashindwaje kuumba wengine kama yeye?
Binafsi naamini utendaji kazi wa Rais Samia ni wa makini na ni wenye lengo la kuleta manufaa kwa taifa na wananchi wake kwa ujumla hivyo sikubaliani na upuuzi wowote unaeletwa na mtu yeyote kwa sababu ya chuki zake binafsi ,najua sasa hivi kuna vita kubwa inayoendelea baina ya makundi fulani fulani kwa sababu tu utashi wao binafsi na wengine wamekuwa wakipinga utawala wa Rais Samia lakini huwezi kuwasikia wakizisema wazi sababu zao bali wao wamebaki tu kujificha kwenye box la "uzalendo".
Watu hawa ndio wamekuwa viongozi wa kuzua uongo kila kukicha ili tu watimize wanachokusudia hawa watu ni sawa na chui waliojivika ngozi ya kondoo ,watu hawa ukiwatizama usoni wanajionesha tofauti na walichokificha ndani ya mioyo yao.
Hawa watu ni wanafiki na ni wabinafsi na ni watu hatari sana.
Ungejaribu kujibu hoja badala ya kumshambulia mtoa hoja
 
Back
Top Bottom