Baada ya OYA kumtesa mwanangu, Mungu amejibu dua na sala zangu. OYA wamevuna walichokipanda

Ndio maana hii biashara ya kukopesha hela siitaki kabisa,watanzania wengi sio walipaji,kumkopesha mswahili bila ya dhamana ya kueleweka utaishia jela usipoangalia...
Ni kweli kabisa Tena mtanzania mkopaji anakuwa mkali kuliko anaedai Yani ukienda kumdai mtu asipoelewa anaweza kuhus wew ndo unadaiwa japo Hao OYA ni kiboko
 
Kwa Yeyote aliyesoma Kitabu Cha The Charismatic Charlie Wade atakuwa amesoma matukio kama Ya OYA kwa microcredit za Huko China.

Kwa mujibu wa kitabu kile ukikopeshwa ukashindwa kulipa wanakujeruhi na hata kukuua.

Endapo OYA wana mkono wa mchina.
 
Mimi siungi mkono vitu vinavyofanywa na wakopeshaji katika kampuni au taasisi binafsi ila tatizo pia lipo kwa nyie mnaetaka mikopo maana huwa mnachukua mikopo kwa kufata mkumbo mkishachukua haukuna mnachofanya zaidi ya kufanya anasa na vitu vya hovyo kabisa ivi unachukuaje pesa na kwenda kumtunza mwenzio au kuandaa visherehe visivyo na msingi kipindi hiki unakuta wamama na hawa dada zetu inapofika siku ya jumanne,alhamisi ya kila wiki anatweza utubwake kwa kuuza mwili tena hapo hana mkopo mmoja ni zaid na hana chanzo cha kumuingizia pesa zaidi ya mwili wake, jaman ukiona ndugu yako au mke anachukua mikopo hvyo mshaur na asipoelewa kaa nae mbali kabisa muda wowote anakuletea majanga kama sio kufa basi kufilisiwa vitu vya thaman mana wengine hadi wanakimbia nyumba kwa ajili ya vitu vya kipuuzi na familia zao zinalizika afu baadae wanatafuta huruma za watu pembeni,wakopaji msipokua makini mtakwisha sana mana mmekosa hata sura za haibu huko mitaani kwenu watu wanapishana mlangoni kwa kukudai ww kila siku unakopa hapa ukalipe pale kwa ajili ya ujinga tu
 
Watu wa mikopo wajifunze kudai.
Njia ya vitisho haisaidii
 
Watanzania
Watanzania sio waaminifu kwenye mikopo
 
Du! hiyo OYA inamilikiwa kwa ubia na Mafwele na Muliro ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…