Baada ya Rais Samia kumaliza teuzi katika vyombo vya dola, Sasa macho yote Mahakamani. Nani kuwa Jaji Mkuu?

Baada ya Rais Samia kumaliza teuzi katika vyombo vya dola, Sasa macho yote Mahakamani. Nani kuwa Jaji Mkuu?

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Naona Mh. Rais SSH kamaliza kupanga safi ya viongozi wa vyombo vya dola. Macho yetu yote ni kwa Mahakama. Je, nani atakalia kiti Cha Jaji Mkuu?
Screenshot_20220720-063640.jpg
 
Kwanini wateuliwe?

Nchi zinazojielewa kuna platform kabisa watu hutuma maombi na kuna mchujo wa wazi kabisa.

Sio habari za kulipa hisani za ukaka,udada ,ushemeji n.k
 
Kwanini wateuliwe?

Nchi zinazojielewa kuna platform kabisa watu hutuma maombi na kuna mchujo wa wazi kabisa.

Sio habari za kulipa hisani za ukaka,udada ,ushemeji n.k
Huo ni utaratibu tu, hata Tanzania inajielewa na huo ndo utaratibu wake kwa mujibu wa Katiba
 
Kwanini wateuliwe?

Nchi zinazojielewa kuna platform kabisa watu hutuma maombi na kuna mchujo wa wazi kabisa.

Sio habari za kulipa hisani za ukaka,udada ,ushemeji n.k
Safi sana kwa hoja nzuri hii, wateule wote hawa kuanzia IGP mpaka kwa CJ ilibidi waombe na kufanyiwa interview, tukiambiwa tunaishi in a pithole country tunachukia wakati ndio ukweli wenyewe
 
Huo ni utaratibu tu, hata Tanzania inajielewa na huo ndo utaratibu wake kwa mujibu wa Katiba
Real?,tuna katiba nchi hii!mbona bado tunajificha kwenye hizi ID fake?,bila JF hakuna platform yeyote ya kuongea kwa uhuru huu, nchi zenye katiba watu hawajifichi kwenye ID fake, wake up mkuu
 
Katiba mpya kama sheria mama itasimamia vema mhimili wa mahakama kutoingiliwa na aliyeshika hatamu!

Itahakikisha mteule judge hafanyi hukumu KWA rimoti kutoka Ikulu kama ilivyo Sasa!!

Ndio maaana wenye hekima wa zama hizi Wanaimba KWA pamoja wimbo huu hapa:-

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"
 
Back
Top Bottom