Tetesi: Baada ya Serikali kuanza mahojiano na Nyalandu kuhusu kashfa katika Wizara ya Maliasili na Utalii, atimkia CHADEMA

Hapo ni very simple case, Nyalandu atasema alipewa maelekezo na raisi wa nchi na hiyo inakua mwisho wa mchezo
Hiyo sio excuse hata mattaka alisema hivyo hivyo akaulizwa majukumu yake yanaishia wapi. Unakumbuka kesi ya zombe ameachiwa huru lkn alishiriki kutoa amri.
 
Kwamba chadema inatoa kinga dhidi ya mashitaka au wanaweza kuzuia!
 
kashfa ya uuzwaji wa nyumba za serikali na manunuzi ya kivuko kibovu mahojiano yanaanza lini.?
 
Ila duh karibu miaka 3 ivi ayupo kwenye uwazir na sikusikia haya kwa ccm kuna nn baada ya kwenda chadema imekua shidah kwake naona mahakama ya mafisadi iwe live tujue nini kinaendelea duniani
 
Umepata wapi hiyo story.
 
Mchuma janga huchumia wakwao
 
Africa bado ile ile na watu wake weusi (Wanyama weusi) Mungu sijui hili bara uliwahi kututamkia nini, sijawah kufahamu, bado natafuta maandiko ya kwenye biblia juu ya Africa na watawala wake. Kwanin hatuna uzalendo? Kwann kila akiingia ofisin anaiba na kukosa uaminifu?

The same case kwa Lazaro Nyalandu, umetumikia Singida kazkazin 4 terms ikiwemo hii ulojivua, umekuwa Naibu waziri hatimaye Waziri, ukavuliwa Uwazir kutokana na Misuse of Public offices, umeshindwa kusimamia rasilimali za watanzania, ukashindwa bhas hata kuchukua fesha hizo ulizogawana wakat unauza twiga ili singida kazkazn ionekane, umeishia kukimbia marekani na kwingineko huku ukihamishia makazi yako mkoani Arusha na kuhama kutoka Singida, Mungu anakuona na huko uendako atakufuata iwapo watanzania wanapata shida kwa kufuja mali zao walizozaliwa nazo.

Leo unakimbilia Chadema, watakupokea eti pia kwamba wewe ni msafi, wakat huo walikuwa wakikutukana ukiwa CCM, husikii aibu?
Bado nauliza kwa Mungu juu ya bara la wanyama weusi.
 
hoja zako zinafifilishwa na hulka yako Ya kutaja vyama, UMEWAHI KUJIULIZA : mraba, Yona, Dr mlingwa, kitilya, masaki, Siyoi walishitakiwa wakiwa chama gani? Aden Rage je?.

Acha kujificha nyuma Ya kivuli cha vyama ili uwe na mawazo huru
 
hoja isiyopendwa
 
Kwa yoyote akitoka huko lazima aundiwe kashfa kwa nini iwe baada ya kuhama. Mahakama zipo kwa nini hiyo tuhuma iwe sasa ebu kuwe na ustaarabu .
 
Samahani sana- Huyo Nyarandu ni nani??????? Mbona hueleweki?????? Kiswahili ndiyo hivyo jee ingekuwa kichina ??????
Tuheshimu majina yetu kwa kuyaandika yanavyostahili kuandikwa.
 
Yule so MTU wa simple lihivyo...hapo bwana yuuleee akijitahidi sana
 

Jamaa jina tu la anayemrushia madongo ameshindwa kuliandika kwa ufasaha....

"RAZALO NYARANDU"

Nilipoona tu makosa haya ya kisarufi, nikatambua mara moja kuwa hapa tunalishwa matango pori....!!
 

Aisee naona umeamua kutulisha matango pori mkubwa....

Spelling tu za jina la unayemtukana umeshindwa kuliandika kwa ufasaha, humo kichwani mwako utakuwa sawa kweli??

RAZALO NYARANDU *

LAZARO NYALANDU √
 
Inashangaza kidogo kwa pande mbili zinazotetea na zinazopinga Mbunge husika kujiondoa huko alikokuwa na kwenda huko anakojiunga.Kwa miaka miwili kama sio moja(naweza kusahihishwa)iliyopita/uliopita gazeti la Jamhuri lilidadavua kwa undani na vidhibiti visivyotia shaka kuhusu mambo yaliyokuwa yanafanyika wizara ya maliasili na sekta ya utalii kiujumla.Nami nikiri nilikuwa mmoja wa watu niyesoma nakala za kila gazeti kipindi wanafukunyua mikataba ya vutalu ili kupata undani kilichokuwa kinajiri Wizara ya mali asili na sekta ya utalii kiujumla.Kilichonifurahisha ni jinsi waandishi walivyo kuwa wanaangusha na ushahidi wa documents(niliwanyanyulia mikono).Hivi hawa waandishi si wapo hai au walihama nchi?Hebu tupieni nakala hizo za marejeo ili watu wengi waone kilichokuwa kinajadiliwa sekta ya maliasili na utalii ikihusisha mikataba badala ya baadhi yetu kudhani mijadala kuhusu maliasili na utalii sintofahamu zake imeanza juzi tarehe 30 Octoba,2017.Ninaposoma comments za wachangiaji kwa siku nne mfululizo mpaka sasa najiuliza hawakusoma au kuona yaliyokuwa yanajadiliwa na Gazeti la Jamhuri na vielelezo vyake?Halafu ile clip ya Mbunge wa Arumeru bungeni aliyekuwa anachangia kuhusu wizara ya maliasili na sekta ya utalii kuhusu dada moja ambaye hakuwa "Miss Tanzania"wala mtumishi wa wizara/serikali kwenda Marekani kutangaza utalii wakati ni "muigiza wa tamthilia ya kidedea"walahi nilicheka.Hebu tunapojadili masuala ya nchi yenye manufaa kwa Watanzania tuangaze kimapana na kiweledi tusiangalie mambo ya kisiasa siasa ingawa mtu kujiunga na chama anachoona kinafaa ni hiari yake pia ni demokrasia lakini haipendezi asilani kuwa na ajenda ya kufukia mabaya yaliyofanyika nyuma ili yasikumbukwe na kushughulikiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…