SAUTI YAKO
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 2,953
- 2,044
Naona WATOTO wadogo wengi wakiwa wamekusanyika pamoja wakiendelea na michezo yao tena kwa furaha kubwa na mama zao wakiwa nao wamekaa kwenye vikundi hapa mtaani story za hapa na pale zikiendelea.
WATOTO waliorudishwa majumbani na serekali kwa nia nzuri tu ya kuwakinga na maambukizi haya ya Covid-19 ili Kila mmoja atulie nyumbani kwao mambo hayako hivo; labda kwa WATOTO wa Saint Marry, tena wanaoishi huko Upanga, Mbezi Beach, Masaki, O'bay, Seaview a.k.a kina Junior hao ndio wazazi wao wana upeo wa kuelewa nia ya serikali kuwarudisha wanafunzi nyumbani.
Kwetu huku Manzese, Kigogo, Buguruni, Kwa Mtogole, Rangi Tatu, Kiwalani na Vingunguti Mambo ni tofauti gololi zinaendelea kuchezwa kwa pamoja; kukimbizana na kupikapika mpaka najiuliza maswali kulikuwa na haja gani ya kuzifunga hizi Saint Kayumba?
Mwisho nakuja kugundua kuwa elimu elimu juu ya janga hili bado inahitajika sana huku mitaani kwetu. Mungu azidi kuwalinda na kuwapigania watoto wetu.
Enyi wakuu mlio humu naomba tuendelee kuwahamasisha wazazi wenzetu wa uswahilini wajue umuhimu wa kuwatuliza watoto wetu huko uswazi sio kuwaachia kucheza hadi saa tano usiku hasa kipindi cha janga hili la Corona. Mungu ibariki Tanzania na watu wake!