- Thread starter
- #21
Si mbaya nikikumbusha tena kuwa hakuna ninapolalamika bali ninasema.Kulalamika kila kukicha hakuongezi tija serikalini.
Mengi uliyoandika ni hisia tu, unao ushahidi kwamba wewe na mimi tusipolipa kodi bado serikali itashindwa kununua magari yanayotumiwa na viongozi wa serikali?.
Tatizo letu ni kujipatia haki mpaka kupitiliza, kwamba mimi na wewe tusipolipa kodi basi wale wabunge maisha yao hayataendelea kuwa kama yalivyo!. Naielewa concern yako kama mlipa kodi lakini maisha yanaendelea pasipo mimi na wewe kuwa sehemu ya walipa kodi.
Ufisadi upo tangu enzi za Yesu na Mohamed, sio jambo la kumalizika leo eti kwa mimi na wewe kuwa na uhuru wa kuhoji. Hasara za makampuni zipo dunia nzima, zipo kwenye mataifa yote.
Kodi hazikwepeki hata kama mimi na wewe tunaweza kuwa na mchango mdogo sana katika kuzilipa. Mataifa yote duniani hayawezi kujiendesha pasipo ukusanyaji wa kodi. Huo ndio ukweli na siku zote huwa unauma ukiutafakari kwa kina.
Kuna tofauti kubwa baina ya kulalamika na kusema.
Lipi la hisia baina ya haya?
Kuhitaji "fair share" ya kodi haiwezi kuwa ni hisia au kulalamika. Kuhitaji accountability hakuwezi kuwa ni hisia au kulalamika.
Kwenye hili kitaumana na huo ndiyo ukweli wenyewe.
Ufisadi kuwepo tangu enzi za Yesu hakuwezi kuhalalisha wewe kuiba au awaye yote kuendelea kuiba na hasa kutuibia.
Makampuni kupata hasara hali kadhalika hakuwezi kuhalalishwa kuwa ni dhidi yetu wala si dhidi yenu wala mwingine awaye yote.
Hayupo anayekataa kodi za halali. Hatutaki kodi na tozo dhalimu. Ndiyo maana tozo ya miamala sitakaa nilipe.