Baada ya siku 100: Tunapoachana kwenye Mataa na Rais Samia

Si mbaya nikikumbusha tena kuwa hakuna ninapolalamika bali ninasema.

Kuna tofauti kubwa baina ya kulalamika na kusema.

Lipi la hisia baina ya haya?



Kuhitaji "fair share" ya kodi haiwezi kuwa ni hisia au kulalamika. Kuhitaji accountability hakuwezi kuwa ni hisia au kulalamika.

Kwenye hili kitaumana na huo ndiyo ukweli wenyewe.

Ufisadi kuwepo tangu enzi za Yesu hakuwezi kuhalalisha wewe kuiba au awaye yote kuendelea kuiba na hasa kutuibia.

Makampuni kupata hasara hali kadhalika hakuwezi kuhalalishwa kuwa ni dhidi yetu wala si dhidi yenu wala mwingine awaye yote.

Hayupo anayekataa kodi za halali. Hatutaki kodi na tozo dhalimu. Ndiyo maana tozo ya miamala sitakaa nilipe.
 
MATAGA na Sukuma Gang wanakomeshwa
 

Mkuu ninadhani Mama alikuwa na nia njema na angali nayo. Ninaamini hapa ni kukaza kamba tu. Tatizo letu kubwa ni hao wanyoa viduku:



Humo kuna wahafidhina bila kuwasahau hawa hapa tameer Kitimoto Jumbe Brown na wenzao.

Ubinafsi wao uliopitiliza ndiyo unaowasumbua:


Ni wazi kuwa tunakokwenda kitaumana na wala si mbali.
 

Moyo kupumua haina maana ya kuwa nikubaliane tu hata na nisivyokubaliana navyo.

Bajeti si msahafu. Mpaka bajeti nyingine hiyo watajua wao. Hiyo sasa sisi haituhusu.

Tunajua ipo lugha wanayoielewa. Tulipo mbona tutaelewana tu?
 
Moyo kupumua haina maana ya kuwa sikubaliani tu na nisivyokubaliana navyo.

Bajeti si msahafu. Mpaka bajeti nyingine hiyo watajua wao.

Tunajua ipo lugha wanayoielewa. Tulipo tutaelewana tu.
Kodi zitalipwa mpaka siku ambayo zitabadilishwa, haya mengine ni maongezi ya kufurahishana.
 
Your browser is not able to display this video.
 
Wasisubiri msemo ule wa kizaramo ukafanya kazi,"mwana kulitafuta mwana kulipata"

Wanampango mkakati wa kulitafuta. Mbona wana watalipata.

Kwa mwendo huu kitaumana si muda mrefu.
 
Sasa kurudia njia mbaya tuliyokuwa tukiifuata na kutambua kuwa ilikuwa njia mbaya,je kwa hiyari tutairejea?

Kukaa na kudumu kwenye njia inayopaswa kwa hakuwezi kuwa hisani au utashi wa mtu binafsi.

Tunayo kazi takatifu mbele yetu ya kulifanyia taifa hili katika namna ambayo historia itatukumbuka.
 
Uzuri mmoja ni kuwa nchi hii ina msingi wa maelewano tofauti na baadhi ya mataifa ya afrika.

Mtanzania ni muelewa siku zote hata akilalamika siku au wiki nzima.

Naamini awamu ya sita haina nia mbaya.

Tate Mkuu palikuwa na uzi hapa:


Wanatuchukulia poa. Waache waendelee hivyo hivyo.
 
Unayo yasema yana mantiki. Ni kweli kwamba ikiwa huwezi kutatua jambo, ishi nalo...wanasema "let go" na hivyo unajipunguzia chance ya kupata magonjwa...nk. Ati hakuna maendeleo yasiyo na gharama...nk. Maneno hayo ni mema yanapozungumzwa na mtu mwenye hekima na busara ambaye ni mwenye moyo safi anayependa kwa dhati kuwaona wanaoitwa wanyonge wanaishi kama binadamu wenye heshima na raha ya aina fulani pale wanapoishi.
Huenda ingependeza zaidi ikiwa yangesemwa bila chumvi wala ushabiki wowote ambao kuwepo kwake kunamfanya mtu huyo mnafiki. Anakuwa mnafiki ikiwa anajua anayoyasema ni uongo.
Yako maendeleo ya vitu na yako ya watu...nk na tofauti zinajulikana. Sasa, hizo gharama ni za vitu au watu? Unapopandisha kodi ili uongeze ndege au umjengee kiongozi hekalu wakati unampokonya mnyonge kuku au chochote kwa kushindwa kuchangia mabweni na huku mwanasiasa anaruhusiwa kutolipia baadhi ya anasa zake, utakuwa unazungumzia maendeleo ya yupi?
Unazijua shule zilizoko vijijini zikoje? Vituo vya afya vina hali gani? Barabara zikoje? Shule je?
Kwa sasa hivi, kwa kiasi kikubwa upinzani umedhibitiwa, nani atoe mawazo mbadala?
Huenda sasa umefika wakati waTz wakaweka ushabiki pembeni. Bei ya mafuta inapopandishwa kwa kiasi hicho, nani asiyeona kwamba itasababisha mfumuko wa bei ambao utawatesa waitwao wanyonge? Ati "wajifunze kukubaliana na hali halisi" - wakipata maumivu wasilie?!
Wanasema "if you live in a glass house, don't throw stones". Unapoishi katika nyumba ya vioo, usirushie watu mawe hovyo.
Wako wanaojengewa mahekalu bure, wanoingiza magari ya kifahari bila kodi, mamishahara yao makubwa...nk. Ikiwa wenye kuyapitisha hayo ni kwa ajili yao wenyewe wakilipiwa na wanyonge bila ridhaa yao, unapendekeza watu wakae kimya? Nafikiri, mojawapo ya sababu ya kupinga Katiba ya Warioba, sasa inajitokeza hadharani
Watu waachwe watoe ya moyoni kwa kuwa hawana mwingine wa kuwasemea.
Mungu awe nasi
 

Anasema serikali yake ni Sikivu lakini yasikia nusu nusu:

 
Hii imekaa vizuri.
 
Siyo hisia kaandika ukweli mtupu! Labda wewe ni mbunge ndiyo maana unaona hayakuhusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…