Sijaona hii taarifa kwenye mtandao wa CAF. na pia CAF wanafanya 5 year ranking baada ya mashindano kumalizika na wala sio timu zikiingia makundi tu. Kwa kila hatua timu inayofikia kunakuwa na point zake. Tanzania inashika nafasi ya 13 mpaka sasa kwa kutumia 5 year ranking ya msimu wa
(2016 -2020) na waliopo juu yetu wote timu zao zimefuzu kwenda hatua ya makundi kasoro inch ya Nigeria, Libya na Zambia ambazo timu zao zimeshindwa kwenda hatua ya makundi hivyo kuangukia kwenye play off ya shirikisho. Hivyo hizo nchi zinaweza kutetea nafasi zao endapo zitafuzu kwenye group stage kombe la shirikisho wataiongezea point inchi zao.
Na wakifika mbali zaidi ya hatua hiyo basi na point pia zitakuwa zinaongezeka. Hivyo Caf hawawezi kutoa award points kabla ya mashindano kumalizika. Kikubwa kuiombea Namungo wafuzu ili kazi ya kuiongezea taifa point iwe nyepesi kwa kuwa na timu mbili, na la pili ni kuniziombea timu zetu zote mbili zifike mbali zaidi. Na Cha tatu ni kuziombea zile inchi 12 zilizo juu yetu basi inchi moja wapo timu yakw ishindwe kwenda hatua za juu zaidi ili wasiongeze point.
N.b
Caf wanaruhusu inchi 12 tu ndizo ziinazoingiza timu nne kwenye michuano ya kimataifa kwa kuzingatia record ya performance ya timu zao ndani ya misimu mitano kwenye ngazi ya champions league na confederation cup