Baada ya tamko la TEC, tunasubiri tamko la BAKWATA

Ninakazia nilikuita kujadili hoja yangu iliyokuwa uzi kamili kupitia hiyo comment aliyoitwa FF.
Sina tatizo na hili.
Mbona masheikh na waislam hawa ni ndugu wa wote?
Hili halina utata ila kwanini wengine, pamoja na kuwa ni ndugu wa wote, wanawadharau na kuwakebehi?
Haipo vita ya kibaguzi kwenye mkataba wa Bandari. Hapa pana suala la kisheria siyo kidini.

Tusiondolewe kwenye reli kirahisi namna hii.
Ukizungumza inapaswa ionekane hivyo kivitendo. Nami nikapendekeza huyu aelimishwe. Sijaliona hilo.
 
Sina tatizo na hili.

Jambo jema tuko sote hapa.

Hili halina utata ila kwanini wengine, pamoja na kuwa ni ndugu wa wote, wanawadharau na kuwakebehi?

Usisahau kuwa penye wengi pana mengi. Humo ma CCM, wasiojulikana na hata wasiotutakia mema nao wapo. Tukiwaita, wenye kuukaanga mbuyu na kuwaachia wenye meno watafune.

Ukizungumza inapaswa ionekane hivyo kivitendo. Nami nikapendekeza huyu aelimishwe. Sijaliona hilo.

Mkuu tunafanya sana Hilo. Hapa chini ni mfano wake:

Tuwatambue wanaohaha kutusambaratisha kama Taifa

Angalia pia hata comments mbali mbali kwenye uzi huu zikiitisha staha na kujikita kwenye hoja.

CHADEMA msipoyakabili/kuyakemea haya magazeti yatawayumbisha wafuasi wenu na kuleta mgawanyiko, yakemeeni

Humu JF watu hula ban labda kama ungependekeza vitendo kwa maana ya bakora kama za MUM Morogoro?
 
Hii issue wakipinga TEC ndio imeshaisha hiyo, tec they are powerful
 
Kumbuka moja ya ahadi za DPW nikujenga misikiti Sasa bakwata watasemaje?
Siamini kama Bakwata wanaweza kukubali kuuza Uhuru wao na rasilimali za kizazi cha sasa na vijavyo kwa sababu tu ya kujengewa misikiti.
 
Du! Hawa mashehe kwa kweli wanatisha sana aisee. Yaani waraka umetolewa na TEC kupinga uuzaji wa rasimali za umma wao wanaona umewalenga waislamu? Sijui hawa mashehe huwa wanawaza nini aisee!
 
Wewe umesema unasubiri tamko la BAKWATA, sasa endelea kusubiri kile watasema usiwapangie kuunga mkono tamko la mtu yeyote ama kukataa la mtu. Wao wanautashi wao na kama kutoa tamko watatoa kwa kadri watakavyoona wao. Na pia wanauhuru wa kutosema chochote, sio lazima maoni yatolewe na viongozi wa dini ndio yasikilizwe. Coz wapo viongozi wa dini pia mafisadi vile vile na wanamaslahi binafsi kwenye miradi ikiwepo bandarini kupitisha mizigo yao bila kodi
 
Wao wanautashi wao na kama kutoa tamko watatoa kwa kadri watakavyoona wao
Mkuu ukisoma vizuri munaksaha wangu hata mimi nimesema hivyo na wala sijawalazimisha kutoa tamko. Wana uhuru wao binafsi, sijawaingilia mkuu.
 
Unataka BAKWATA watoe tamko,kwan ANGLICAN wao wametoa tayar,WASABATO JE? na Dini nyenginezo ambazo zipo tz zimetoa matamko.
MUFTI YUPO KIMYAA NA WALA HATOTOA TAMKO
TEC WAO WAENDELEE KUUSOMA HUO WALAKA MAKANISANI MWAO NA WALA HAWAFANYI UDINI NA PIA HAO MASHEKH NAO WALA HAWAFANYI UDINI
ILA MWISHONI TUNAOMBA UWE MWISHO WA AMANI KWA NCHI YANGU
 
Hata hao nao wakitoa tamko hakuna shida yoyote kwa kuwa nao ni raia na wana uhuru wa kutoa maoni kama raia wengine. Kwanini unataka kuwabagua?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…