Baada ya tamko la TEC, tunasubiri tamko la BAKWATA

Baada ya tamko la TEC, tunasubiri tamko la BAKWATA

Hivi sasa mbivu na mbichi zimejulikana wazi kuwa TEC hawaungi mkono bandari kukabidhiwa mwarabu kiholela!
Hapo awali wadau mbalimbali walikuwa wakihoji kulikoni TEC wako kimya juu ya mkataba, kumbe walikuwa wakifanya zao tafiti na hatimae wameleta majibu ya tafiti hiyo!
Hivyo basi ni vyema nao CCT pamoja na BAKWATA wakaweka nao wazi msimamo wao juu ya uwekezaji wa bandari!
Hawa CCT pamoja na BAKWATA bila shaka watakuwa nao wamefanya utafiti wao, hivyo kwa nia ya dhati kwa manufaa ya taifa letu waeleze nao msimamo wao!!
Wanaogopa kuonekana wamewaiga TEC
 
Hivi sasa mbivu na mbichi zimejulikana wazi kuwa TEC hawaungi mkono bandari kukabidhiwa mwarabu kiholela!
Hapo awali wadau mbalimbali walikuwa wakihoji kulikoni TEC wako kimya juu ya mkataba, kumbe walikuwa wakifanya zao tafiti na hatimae wameleta majibu ya tafiti hiyo!
Hivyo basi ni vyema nao CCT pamoja na BAKWATA wakaweka nao wazi msimamo wao juu ya uwekezaji wa bandari!
Hawa CCT pamoja na BAKWATA bila shaka watakuwa nao wamefanya utafiti wao, hivyo kwa nia ya dhati kwa manufaa ya taifa letu waeleze nao msimamo wao!!
Aahaaaa
 
Acha uchonganishi wa kidini mpumbavu
Acha ujinga mkuu. ushakuwa mtu mzima sasa. Unawezaje kusapoti wizi wa rasimali za taifa unaofanywa na mafisi wa CCM au nawe ni mmoja wao?
 
Acha ujinga mkuu. ushakuwa mtu mzima sasa. Unawezaje kusapoti wizi wa rasimali za taifa unaofanywa na mafisi wa CCM au nawe ni mmoja wao?
Sisapoti wizi wa rasilimali za taifa letu ila unayoyasema ni kuleta uchonganishi wa kidini unalazimisha bakwata waingilie kati sakata la bandari ili waonekane wana unga mkono huo ni uchochezi wa kidini ni heri ukakaa kimya kuliko kulazimisha mambo yasiyofaa
 
Bakwata huwa wanaendeshwa na Serikali. Sasa wakitoa tamko la kiudini; zile hoja zao za kusema kuwa Samia anachukiwa kisa anavaa hijab au kisa ni Muislam, tujue hatuna serikali jamani. Tujue kuwa hii serikali inaendelea kukandamizia hoja za udini wakidhani wanakwepesha issue ya bandari kumbe inaleta moto mkubwa wa vita ya udini.

Na serikali ikijibu kitu kupitia hawa Bakwata, basi ni wamejipanga kuendelea na mkataba huo regardless wananchi wanataka nini. Ila mwisho wa siku wajue kuwa wananchi hawabakigi wajinga siku zote. Sio kila chaguzi watafanikiwa kuiba kura. Wananchi huwa wanafikia hatua ya mwisho ya kuchoka na kutaka mabadiliko ya kweli.
 
Sisapoti wizi wa rasilimali za taifa letu ila unayoyasema ni kuleta uchonganishi wa kidini unalazimisha bakwata waingilie kati sakata la bandari ili waonekane wana unga mkono huo ni uchochezi wa kidini ni heri ukakaa kimya kuliko kulazimisha mambo yasiyofaa
Mkuu leo KKKT wametoa tamko lao na wamepita mulemule walimopita wakatoliki wa TEC. Wewe huoni kuwa kuna haja ya BAKWATA nao kuja na tamko lao ili tujue msimamo wao?
 
TUKUMBUKE MWAKA 1992

Mwaka 1992, Serikali iliingia Mkataba na Makanisa kupitia Taasisi zao za TEC na CCT. Chini ya Makubaliano yale, hospitali za Makanisa zitatumika kwa wananchi wote pale ambapo Serikali haina hospitali.

Kwa kufanya hivyo, Serikali itakuwa na wajibu wa kuyapa Makanisa fedha za kuendesha hospitali hizo ingawa umiliki wa hospitali utabaki kuwa wa Makanisa.

Ifahamike kuwa fedha hizo zinatokana na kodI za Watanzania wote; Waislamu, Wakristo, Mabaniani, Magoha, Makadiani, na hata wale wasio na dini.

Nini athari za Mkataba huu ? Mkataba huu wa kibaguzi una athari nyingi. Kwanza:

Serikali inatumia kodi za wananchi kuyapa Makanisa kuendesha shughuli zake za kuimarisha Ukristo.

Tunasema hivyo kwa sababu utaratibu unaotumika ni kuwa Serikali inatoa fedha kwa Makanisa ambayo wao ndio wanapanga matumizi ya fedha zile na sio Serikali.

Pili, kwenye Jamii, Makanisa yanaonekana ndio yanatoa huduma za Jamii na hivyo kujenga saikolojia kwa wananchi kuwa Ukristo ndio unajali wananchi.

Athari ya tatu ni kuwa Makanisa yananyonya wananchi kwa sababu pamoja ya kuwa hospitali zile zinapata fedha kutoka Serikalini, bado wananchi wanalipia huduma.

Nne, Mkataba hauna ukomo, yaani ni wa milele. (Wakristo wataendelea kupewa hayo mabilioni na Waislamu watanyimwa milele).

Kwa tafsiri nyingine ni kuwa Serikali imejivua kwenye wajibu wa kutoa huduma za Jamii na kuchagua Makanisa kuwa ndio wakala wake.

Tunapenda kuwakumbusha Watanzania kuwa wakati Mkataba huo unasainiwa aliyesaini Mkataba ni Bwana Edward Lowassa aliyekuwa Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu. Huyu ni Mkristo

Kwa utaratibu wa Serikali, Lowassa alikuwa Waziri wa Nchi, hivyo basi Waziri mwenye dhamana ni yule mwenye ofisi yake kwa maana ni Waziri Mkuu.

Wakati unatiwa saini Mkataba, huo Waziri Mkuu alikuwa John Samwel Malecela ambaye ni Mkristo.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndie aliyeishauri Serikali isaini Mkataba ule ambao kwanza hauna ukomo (mkataba wa maisha) na pili unatumia kodi za wananchi kuimarisha Ukristo alikuwa Damian Lubuva ambaye ni Mkristo.

Kwa upande wa Kanisa mwanasheria wao alikuwa Prof Balozi Costa Mahalu, Mkristo.
Kwa maana hiyo, upande wa Serikali, Mkataba ule umeasisiwa na kusimamimwa na Wakristo watupu. Waziri wa Nchi Mkristo, Waziri Mkuu Mkristo, Mwanasheria Mkuu Mkristo.

Ni Wakristo! Wakristo! Wakristo!

Kama kwenye hoja ya makubaliano ya Bandari ni Wazanzibari wawili (ambao ni Waislamu) wamesaini makubaliano ya kuiuza Tanganyika, Mbona Waislamu hawakulalamika pale Wakristo 3 wazito Serikalini walipobuni mbinu za kutumia kodi za wananchi kuimarisha dini yao Ukristo Tanzania?

Kama hoja ni ukomo wa mkataba, mbona Mkataba huu wa Serikali na Makanisa hauna ukomo? Ni mkataba wa milele na ndio maana mpaka leo (miaka 30 sasa) bado unaendelea kutumika.

Bado Serikali inaendelea kutekeleza Mkataba wa kibaguzi ambapo inatumia kodi za wananchi wote kuimarisha shughuli za Kanisa.

USHAHIDI

Tarehe 23 Januari 2019, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa dini zote IKULU. Kwenye Mkutano ule Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga Bwana Maimo Mndolwa alilalamika kwa Rais Magufuli kuwa Serikali inavunja Mkataba kwa kujenga hospitali kwenye maeneo ambayo Kanisa imeachiwa kuwa na hosptali ambazo zinapewa fedha na Serikali.
Amelalamika hivyo kwa sababu Mkataba wa Makanisa na Serikali hauna ukomo. Kila penye hospitali ya Kanisa, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali yake. Badala yake, Serikali inatakiwa kuendelea kutoa fedha za kodi kuwapa Makanisa ili ziendeshe hospitali zao na kuimarisha Ukristo kwa kutumia jasho la Watanzania.

Katika kusisitiza madai yake, Askofu Mkuu alitoa ushahidi wa hospitali zilizojengwa na Serikali katika Wilaya ya Ifakara, Ngara na Muheza ambazo kwa mujibu wa Mkataba wa 1993, Serikali haikutakiwa kujenga hospitali hizo za Wilaya.

Kitendo cha Serikali kujenga hospitali hizo kinatafsiriwa na Kanisa kuwa Serikali imevunja Mkataba kwa sababu sasa inatoa huduma hiyo muhumu kwa wananchi.

Askofu Mkuu alifafanua kua matatizo haya yapo kwenye ngazi ya Wilaya kwa sababu kwenye ngazi za juu, hakuna tatizo kwa kuwa kuna Msimamizi anaesimamia Mkataba huo.

Hapa Askofu Mkuu alikuwa ana maana kuwa hospitali za KCMC ya Moshi, Bugando ya Mwanza na CCBRT ya Dar es Salaam ambazo zote ni mali ya Kanisa bado zinaendelea kupata fedha za kodi huku zikiendelea kuwalipisha wananchi kwa huduma wanazopewa kwenye hospitali hizo.

Rais Samia Suluhu Hassan alifanya Mkutano na Baraza la Maaskofu la Kanisa Katoliki Tanzania uliofanyika Kurasini tarehe 25 Juni 2021. Katika risala yao, Baraza la Maaskofu limeilaumu Serikali kwa kujenga hospitali zake kinyume cha Mkataba wa 1992, na Makanisa.

Kwenye risala hiyo, Baraza la Maaskofu limeshangaa kuona Serikali inajenga hospitali kwenye Wilaya ambazo Makanisa tayari yana hospitali zao. Wamehoji kwa nini kuwepo na ushindani wa kutoa huduma hizo?

Kwa maana nyepesi, kwa nini Makanisa yasiachiwe kuendesha hospitali maisha (milele) na kuendelea kupewa ruzuku zinazotokana na kodi za wananchi?

Risala hiyo ni ya chombo cha juu kabisa katika Kanisa Katoliki ambao leo viongozi hao hao wanaohoji na kulalamika kuhusu makubaliano ya Serikali na DP World kuwa hayana ukomo!

Kanisa hilo hilo ambalo linapiga kelele kuhusu mkataba wa Serikali na DP World, ndilo ambalo kiongozi wake Askofu Method Kilaini alipewa shs. 80.9 milioni, Askofu Eusebius Nzigirwa alipewa shs. 40.4 milioni na Mchungaji Alphonce Twimanye Simon alipewa shs 40.4 milioni fedha za Rushwa zilizotokana na kashfa ya akaunti ya Tegeta ESCROW.

Hadi leo Kanisa halijatangaza hadharani hatua za kinidhamu iliyowachukulia viongozi hao. Ukimya huu tuutafsiri vipi? Kwa ukimya huu, Kanisa linapata wapi “moral authority” ya kupinga mkataba wa DP World.
Kumbuka moja ya ahadi za DPW nikujenga misikiti Sasa bakwata watasemaje?

 
Sisapoti wizi wa rasilimali za taifa letu ila unayoyasema ni kuleta uchonganishi wa kidini unalazimisha bakwata waingilie kati sakata la bandari ili waonekane wana unga mkono huo ni uchochezi wa kidini ni heri ukakaa kimya kuliko kulazimisha mambo yasiyofaa
Kwani BAKWATA wakiunga mkono DPW kuna shida mkuu? Mbona serikali na CCM wanaunga?
 
Ajabu na kweli. Huu Mbona wala si u Simba wala u Yanga; u Arsenal wala u Man U?

F4DQnPZWwAAZcRr.jpeg


Waraka wa TEC ulikuwa kwa wa waumini dhidi ya mpango wa serikali kuhusiana na mkataba wa bandari.

Waraka wa TEC ulikuwa kwa manufaa ya watanzania wote yaani wakristi, waislam na hata wasio waumini.

Sasa wa hawa ndugu utakuwa ni wa nani dhidi ya nani? Kwamba utakuwa wa maslahi kwa nani?

Hata hivyo, kwa kuanzia hadi mtu unajiuliza

"Hivi waraka huo ambao nao wangependa kuwasomea waumini wao, wenyewe wanao?"
 
Tumuulize kikongwe ff maaana ndiye walau aliyemaliza form four kwenye Imani yao
 
HAWAJUI KUSOMA HAO HATA MTUME SAW HAKUJUA KUSOMA WALA KUANDIKA.

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ

[ AL - JUMUA' - 2 ]
Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.
 
HAWAJUI KUSOMA HAO HATA MTUME SAW HAKUJUA KUSOMA WALA KUANDIKA.

هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ

[ AL - JUMUA' - 2 ]
Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa katika upotofu ulio dhaahiri.
Inauma lakini mustahamili tu mutazoea Bandari ndio hiyo imeenda poleni sana
 
Baada ya TEC kuukataa mkataba wa DPW hadharani bila kumumunya maneno, sasa tunasubiri tamko la BAKWATA nao tusikie watasema nini. Ni matumaini yangu kwamba BAKWATA watafuata nyanyo za TEC kwa kuukataa mkataba wa DPW bila kupepesa macho.

Aidha, inawezekana BAKWATA wakaukubali mkataba na endapo watafanya hivyo basi watakuwa na sababu za msingi. Au wanaweza kuukubali na kutoa maoni kuhusu kuboreshwa vipengele vyenye utata, hasa vile vinavyohusu muda wa mkataba na vinavyobagaza mamlaka ya nchi (sovereignty).

Kimsingi ni vigumu kubashiri nini BAKWATA watasema lakini kwa kuwa bado hawajatoa tamko hadharani, ngoja tusubiri tuone watakuja na tamko zito au jepesi kiasi gani. Waswahili wanasema 'usiusemee moyo' au 'usiandikie mate wakati wino upo'. Kwa maana hiyo, hebu tuvute subira kidogo tusubiri kusikia BAKWATA watakuja na tamko la aina gani. Wakati ukifika wataanika kila kitu hadharani. Subra yavuta kheri.
Acha masihara mkuu

BAKWATA inayoshindwa kusimamia waislamu itawezaje kusimamia mambo ya nchi


BAKWATA ni CCM B


Nawashangaa waislamu wanaowasikiliza BAKWATA.
 
Back
Top Bottom