Baada ya teuzi mpya Makonda kapanda cheo au kashuka?

Baada ya teuzi mpya Makonda kapanda cheo au kashuka?

Kutoka kwenye Ukatibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi mpaka kuwa Mkuu wa Mkoa Arusha. Je cheo cha Paul Makonda hapo kimepanda au kimeshuka?

Kwa upande wa Serikali amepanda maana alikuwa hana cheo chochote, ila kwa ulimbekeni wake, na ujinga wa watendaji wa Serikali alionekana yupo juu ya viongozi wa Serikali.

Kwa upande wa chama, amedondoka sana kwa sababu kwa sasa hana cheo chochote, yupo chini ya mwenyekiti wa tawi.
 
Naona serikali na chama ni vyeo tofauti.

Cheo cha serikali anaenda kuwatumikia watanzania wote bila kujali itikadi zao.

Wakati kuwa Mwenezi alikuwa anakitumikia chama chake pekee.

Huyu kwa namna nyingine ni kama samaki aliyeondolewa kwenye bwawa, akaenda kupelekwa baharini au ziwani.
 
Amesogezwa karibu na yule Mzee wa watu Ole Sendeka hivi yule Babu atapata usingizi kweli?😆
 
Amepelekwa akasimamie mradi wake? Asisahau kupita kwa sabaya akamsabahi
 
Kwa upande wa Serikali amepanda maana alikuwa hana cheo chochote, ila kwa ulimbekeni wake, na ujinga wa watendaji wa Serikali alionekana yupo juu ya viongozi wa Serikali.

Kwa upande wa chama, amedondoka sana kwa sababu kwa sasa hana cheo chochote, yupo chini ya mwenyekiti wa tawi.
Ni mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa,na pia ni mlezi wa ccm mkoa.
 
Kama hamjui kwa sasa Mheshimiwa Makonda ni Mkuu wa Mikoa yote.
Ni Mkuu wa Wakuu wa Mikoa.
Subirini mtaona anaenda kumkagua Mkuu wa Mkoa wa Moshi, Manyara Tanga na kwingineko.
 
Back
Top Bottom