Baada ya teuzi mpya Makonda kapanda cheo au kashuka?

Baada ya teuzi mpya Makonda kapanda cheo au kashuka?

Kutoka kwenye Ukatibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi mpaka kuwa Mkuu wa Mkoa Arusha. Je cheo cha Paul Makonda hapo kimepanda au kimeshuka?
Iko 50/50

Kichama ameondolewa uwezo alokuwa nao wa kufanya shughuli zake (kitaifa) na kubakia kuwa mwanachama mwandamizi.

Kiserikali amepewa nafasi ya kuwa msimamizi mkuu wa shughuli za kiserikali katika mkoa wa Arusha ambalo ni eneo moja tu na si taifa zima, hivyo hapo napo amepunguziwa wigo wa majukumu yake.

Hivyo akiwa mwakilishi wa raisi mkoani Arusha akahakikisha wilaya zote mkoani humo zinafanya kazi zake kwa ufanisi unotakiwa.

Kwa kifupi ni kwamba atafanya yaleyale aloyafanya akiwa mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam enzi za wamu ya tano.

Kuna maeneo kama kodi, ushuru na uwajibikaji vyalegalega huko hivyo vyahitaji kusimamiwa kikamilifu.

Hiyo ndo strategia yake na CCM.
 
Kwa kashfa zinazomuandama, kuna kitu hakipo sawa, he is not supposed to be in public office at all . Ni ukaribu wake na mama sio wa kawaida

Mbona mtu mwenyewe sio hata smart kichwan. Tumekosa vijana wenye uwezo ?

Moja ya vijana walioaminiwa na kutuangusha ni huyu na Kigangwala

Nadhan sasa ni wakati wa polepole arudi kwenye NAFASI YAKE
 
Kwa upande wa Serikali amepanda maana alikuwa hana cheo chochote, ila kwa ulimbekeni wake, na ujinga wa watendaji wa Serikali alionekana yupo juu ya viongozi wa Serikali.

Kwa upande wa chama, amedondoka sana kwa sababu kwa sasa hana cheo chochote, yupo chini ya mwenyekiti wa tawi.
Anawajibika kwa mwenyekiti wa chama cha majizi ngazi ya mkoa
 
Back
Top Bottom