Baada ya ukweli wa Erick Kabendera kubainika, wote walionituhumu kuhusika nimewasamehe kwani Mungu amewasamehe. Msirudie tena!

kabendera kukiri na kuamua kuilipa serikali si ushahidi kwamba kweli alitenda makosa hayo! tumia akili kidogo paskali!

kwa bandiko lako hili unazidi kuitangazia dunia kwamba Erick alikua mhujumu uchumi na anamiliki genge la kivita.

badala ya kumsafisha mwandishi mwenzako et ww unajisafisha na kumkandia mwenzako,kwamba serikali makosa waliyomkamata nayo hayana uhusiano na uandishi wake wa habari.

sijui unakwama wap brother! mbona uko miongoni mwa wanaotumia ubongo wao? kwanini kuna wakati unaweka akili pembeni?

plz inapobidi kaa kimya usichokonoe vidonda vya watu
 
Pole Pascal, though nilikupa pole tangu siku ya kwanza. Tumekuwa wepesi sana kutuhumu.
 
Pole sana mayalla binafsi mpaka leo sioni kosa lako hata kama zile Makala zilikuwa za Kabendera japo haijathibitika kama zile ni makala zake.

Ulichofanya ni ku share zile makala kama makala zingine zozote zile hapa JF..

Wengi humu Jf walikuwa wanakupinga pale ulipokuwa unazipinga zile makala kuwa ni za uongo na zinamkosea heshima Rais. Watu walikuwa wanasema kilichoandikwa kwenye zile makala ndio hali halisi.

Lakini ilipokuja kuhisiwa kuwa mwandishi ni kabendera wale wale walikugeuka kuwa umemchomekea Kabendera.

Watanzania tumejaa unafiki ni vigeugeu na hatuna msimamo..

Ndio maana leo mtu huyohuyo akiwa chama tawala ataitwa kila majina mabaya ya ufisadi lakini siku akihamia upinzini ataitwa shujaa...

Leo tunashuhudia wanasiasa wakihamia chama tawala kwa kasi, huku wakitaja maendeleo chini ya Maguli. Lakini kiuhalisia wanawaza nafasi zao matumbo yao na famili a zao.

Kifupi usimwamini Mtanzania mara nyingi yeye anafuata upepo unakovumia..

Wakati mwingine naunga mkono Magufuli bora atuburuze tu mapaka tupate akili,maana hatujui tunataka nini.
 
Mkuu P umeeleweka... Nadhani hata nawe ulitegemea upinzani dhidi ya hili bandiko kutoka kwa watu waliokutuhumu...Ila binafsi nimekuelewa....Uwongo hauwezi simama mbele ya ukweli daima.
 
Ni sakata la Ndugu Erick Kabendera,

Kila mtu ana lake...Wengine watatunga ili kufurahisha nafsi zao na watu wao. Tafadhali ukipata habari yoyote kuhusu hii ishu ni vema ukaihakiki kabla ya kuiweka humu... Na wewe uliyeikuta humu ihakiki pia kabla ya kuisambaza kwa wengine.

Nimeandika sababu nimeshazishuhudia habar kadhaa za hivyo mpaka sasa na pia ni kutokana na kasumba ya baadhi ya wanajf hasa kwa matukio yanayotrend nchini.

Ni hayo tu.
 
Shukurani ndugu kwa somo hili. Hapo juu kwa kina Mazegenuka nimekuelewa sana. Duh! Ama kweli nchi hii imetoka mbali.
 
Fake kivipi sasa?

Hajaachiliwa toka jela?

Hajalipa ama kutakiwa kulipa Tshs. 273M ili kununua Uhuru wake?

Mama yake hajafa?

Hajabambikiziwa kesi?

Pls, explain tujiepushe na feke news kuhusu lipi au nini juu ya huyu mtu Erick Kabendera....
 
POMPEO BABA LAO.
 
Maumivu aliyoyapitia Kabendera hayaelezeki,pascal umekimbilia kujisafisha kwanza pasipo kuwa na UTU , huna uchungu kabisa nilitegemea ungeenda kwa kabendera kumtia moyo kwa kufiwa na mama yake pili kwa adha iliyompata ya kukaa mahabusu kwa kubambikiwa kesi...PASCAL UMEACHA FANI YAKO SASA UMEKIMBILIA SIASA, ,ITAKUMALIZA!

hivi Kabendera kama angefungwa, ungekuja tena kujisafisha???
 
Fake kivipi sasa?

Hajaachiliwa toka jela?

Hajalipa ama kutakiwa kulipa Tshs. 273M ili kununua Uhuru wake?

Mama yake hajafa?

Hajabambikiziwa kesi?

Pls, explain tujiepushe na feke news kuhusu lipi au nini juu ya huyu mtu Erick Kabendera....
Nadhani hatujaelewana boss
 
Pole sana! Nakushauri uendelee kuusema ukweli hata kama utapingwa na watu wote, ilmradi ujue kuwa Mungu atakuwa upande wako.

Kumbuka kuwa ni aheri kuwa peke yako na Mungu kuliko kuungwa mkono na umati wa watu - wanafiki, vigeugeu na waovu!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…