Wanabodi,
Kwa vile sisi binadamu tuna uwezo tofauti, na sio watu wengi wanajitambua uwezo wao katika kitu kinachitwa
"self realization", ikitokea unajitambua, na unapokasirika kwa kutotendewa haki, kwa kutwishwa misalaba ambayo sio yako, na ukiumia na kulaani watesi wako, na unajua nini kitawatokea pale Mungu anapoamua kukutua msalaba huo, then sauti ya Mungu inakuingia, na hapo hapo unakumbuka na kuwasamehe watesi wako, kabla karma haijaanza kuwafanyia kazi.
Baada ya mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera kukamatwa na polisi na kushikiliwa mahabusu kwa miezi 7, msalaba wa kukamatwa nilibebeshwa mimi. Eti ni mimi Pascal Mayalla ndiye niliyesababisha kukamatwa kwa Erick Kabendera, kwasababu ya zile makala zangu za uzalendo humu JF.
Hizi ni Baadhi ya Makala Zangu Kuhusu Uzalendo, wale wenye muda, pitieni halafu mnieleze wapi nimemponza mtu yoyote?
Japo nilijifanya mgumu na sijali, kwasababu kiukweli kabisa, makala zile wakati zinaandikwa hazikuwa na lengo la kumchomea mtu yoyote, popote, na wala sikuwahi kuwafahamu waandishi wa makala hizo. Na mpaka sasa ninapoandika leo, bado siwafahamu waandishi wowote wa makala hizo, lakini kwa upande mwingine, kwa vile kuna mwandishi wa habari, Erick Kabendera, amekamatwa katika mazingira ya kutatatisha. Baada ya askari waliotumwa kumkamata kukataa kujitambulisha, hivyo kudhaniwa ni wasiojulikana na Erick akawagomea kuwafungulia, ndipo wakamfanyia utekaji kwanza; kwa kutekwa na kufichwa kusikojulikana kwa muda siku mbili za mwanzo, huku serikali wakitupiana mpira, mara ni polisi, mara ni immigration, na kosa lake mara ni uraia ila full kujiuma uma!.
Ila baada ya kufikishwa mahakamani ndipo kukaibuka uhujumu, utakatishaji fedha na magenge ya uhalifu. No one was sure axactly what is it, hivyo any reasonable man lazima ujiulize, "what if ni kweli mwandishi ni yeye?", "what if ni kweli zile makala zangu ndizo zimeiamsha serikali na kuichochea kumtafuta anayeandika?", "what if ni kweli mwanzo alitumiwa wasiojulikana ili wampoteze kama Azory Gwanda na Ben Saanane lakini baada ya Erick kuunguza picha, ndipo ikashindikana, na kuamua kumtafutia mashitaka yoyote ya kumbambikia just to silence him? Then japo nilikuwa najikaza kisabuni, lakini automatically nilianza kujihisi, na kila siku Erick alipokuwa akifikishwa mahakamani naumia, "what if sababu ni mimi?".
Kila uzi wowote kumhusu Erick Kabendera ukipandishwa humu JF lazima humo ndani ya uzi, lazima nilikuwa natajwa as a
"snitch". Kila mateso aliyokuwa anakutana nayo Erick Kabendera, na mimi yalikuwa yananiumiza psychologically. Kwanza nikawa sichangii uzi wowote kuhusu jambo lolote kwa Erick Kabendera.
Mimi ni story teller, kwa wapenda nyuzi fupi, ishieni hapa, na kwenda kule kwenye hitimisho, wapenda mastory ya JF, tuendelee hapa
Sisi Wakristu wa kweli, tunaofuata mafundisho ya Mungu wa Kweli, na kufuata mafunzo ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Kweli, tumefundishwa kusameme hata saba mara sabini, hivyo mimi kwa upande wangu, niliisha kusamehe toka siku ile ya kwanza ulipopandisha bandiko hili kwa kulipuuza, kwasababu ulikuwa hujui utendalo. Pia nimewasamehe wale wote walionituhumu ni mimi kwa kuamini kuwa kweli ni mimi.
Hitimisho:
Hivyo kwa uzi huu, baada ya ukweli wa mashitaka ya Erick Kabendera kubainika, mimi nimewasamehe "Wale Wote walionituhumu mimi kuhusika na kukamatwa kwa Erick Kabendera, na kufuatia msamaha huo, pia "Mungu nae, amewasamehe" Hakuna tena adhabu ya karma kwenye kunisingizia mimi issue ya Kabendera, ila tafadhalini sana, msirudie tena kumtuhumu mtu mwingine yoyote kwa tuhuma ambazo hamna hakina nazo! Kauli huwa zinaumba, sisi wengine tunajijua kauli zetu na madhara yake, hivyo mkituudhi tusiposamehe.
Hivyo kwa upande wangu, uwe na amani kabisa, na wote mlionituhumu humu na kungine kote, muwe na amani, nimekusamahe na kuwasamehe wengine wote kwa roho safi na roho nyeupe, lakini ili karma isikushughulikie na wewe kwa upande wako, baada ya kuujua ukweli huu, do the right thing, hata kimoyo moyo tu, inatosha Mungu anasikia kila kitu hata usipozungumza, ile kuwaza tuu, is enough!
Ubarikiwe sana.
Paskali.
Ukweli gani umebainika??. Huo wa kulazimishwa ukubali makosa ili ulipe pesa kupitia michango ili waheshimiwa waonekane wanafanya kazi?. Hakika nchi hii imelaaniwa hatuwezi kuua mtu mzima anayetueleza wazi tena kwa kutuomba msameheni mwanangu nitakufa bila yeye, hadi bibi wa watu kafa. Sijui huyu Mungu kama yupo atatufanya nini kwa matendo yetu