Baada ya ukweli wa Erick Kabendera kubainika, wote walionituhumu kuhusika nimewasamehe kwani Mungu amewasamehe. Msirudie tena!

Baada ya ukweli wa Erick Kabendera kubainika, wote walionituhumu kuhusika nimewasamehe kwani Mungu amewasamehe. Msirudie tena!

Bandiko la kipuuzi kabisaa! Maelezo mengiiii..,lkn yote yanathibitisha tu jinsi hiyo dhambi uliyotenda inavyokutesa! Bora hata ungekaa kimyaa tu,unazidi kujidharaulisha tu.

Kiukweli ww ni mtu wa kuogopwa sana hapa TANZANIA..Yaani unaonekana kufurahia kabisa hukumu ya EK kwamba imekusafisha!? Natamani kukutukana ila acha tu nivumilie.
 
Ni ukweli upi tumeujua mzee? Ni mpuuzi na mpumbavu tu ndie atakaeamini mashtaka ya Eric. Ukweli unajulikana na hata watoto wadogo wanalijua hilo. Unahusika na tabu zote alizopitia Eric hata kama ni kwa asilimia 0.1

Sent using Jamii Forums mobile app
Watanzania mna vichwa vibovu Sana , Una ushahidi gan anahusika....?? Ifikie hatua kila mmoja apambane na Hali yake na sio kujibanza kwa mtu
 
Wachafu siku zote katika maisha yao huvaa nguo SAFI, siku yaja roho zenu zitatamani ziombe msamaha kwa ubaya wenu lakini mtakuwq mmechelewa.
 
Ukweli upi umejulikana. Hakuna kilichojulikana. Kabendera anaweza kuwa ameingia "plea deal" ili mradi tu awe huru lakini ukweli ukabaki kuwa haujulikani kwa sisi watazamaji. Serikali kubadilishabadilisha mashtaka dhidi ya Kabendera mpaka wanakuja kumtoa inaibua maswali zaidi, haionyeshi ukweli wowote hapo.
 
Ndugu Mayala narudia tena niliokuambia nyuma. Wewe ni mmoja ya watu tunaodhania ni kama mfano humu JF. Lakini ndugu yangu wakati mwengie unaandika maneno ambayo kwa kwetu sisi tunahisi unajidhalisha mwenyewe na upande wa pili unadhalilisha fani yako ya Uandishi wa habari.

Hivi kama ni wewe mwenyewe umetiwa ndani miezi 7, mama yako Mzazi amekufa yuko ndani, ngelisemaje? Unafikiri MO Dewji baada ya kuachiwa aliyoyazungumza yote ni ya kweli?. Usifikiri watanzania wa Leo ni wale wa miaka ya 70 utawambia jambo hawatafikiria. Unajidhalilisha ndugu yangu bora ungelikaa kimya tu
 
Back
Top Bottom