Baada ya ukweli wa Erick Kabendera kubainika, wote walionituhumu kuhusika nimewasamehe kwani Mungu amewasamehe. Msirudie tena!

Baada ya ukweli wa Erick Kabendera kubainika, wote walionituhumu kuhusika nimewasamehe kwani Mungu amewasamehe. Msirudie tena!

Paskali safari hii hadi uathirike kisaikolojia - kama unaogopa hukumu za kidunia. Unaandika kwa nakshi kupita kiasi. Sisi Watanzania si wasomaji wazuri sana; unajua hilo. Sasa hizo mbwembwe zako na kuturundikia mabandiko yanayopandiana ili eti tufanye rejea ya masuala, zimeishia kukutwisha zigo la u-“snitch”.

Halafu ndio unaharibu zaidi kwa kutaka kujitakasa kwa mtindo uleule - au ni janja ya kuibua upya mjadala wa Kabendera kwa ‘namna’ ingine? Tuseme una wasiwasi kuwa wako wengi watakaoamini kuwa hii ishakuwa “case closed” baada ya “Roma locuta”? Sisi waelewa hatuna shida na wewe. I have no doubt of your innocence. Sijui unalenga kujisafisha kwa nani hasa?
 
Pascal Mayalla Kabendera amekiri makosa ya ML & tax evation. Wanaojaribu ku -spin hii story eti amelazimika kununua uhuru wake wanamchafulia jina kwa kumfanya mpiga dili za kukiuka mujibu wa sheria. Hamumsaidii kwa Hoja hizo za kitoto, bora mumuwache ajenge reputation yake afresh.Maana sasa huyu sio mshukiwa ni convict wa Kuhujumu Uchumi
Na sisi hilo tumeona halina uhalisia,tunaamini kabambikiziwa kesi na ni shinikizo la Mabeberu limempa uhuru mapema!
 
In this day and age ya information overload.., summarization ni muhimu sana.., bandiko lako lingeweza kujibu haya kwa sentensi tatu au mbili tu

a) Ulishutumiwa kwa yapi
b) Umesafishwa kwa lipi
c) Ukweli upi umejulikana
 
Eric Kabendera na Pascal Mayalla wakiwa jukwaa moja kujadili mustakabali wa uhuru wa habari na wa kujieleza bila kujikita kuchafuana ktk majukwaa ya Habari na Mawasiliano.



Source: JamiiForums
 
Lakini Mzee Pasko, Erick anaonekana kabisa hakuwa na jinsi. Na yote hao turejee tu kwenye ukamatwaji wake. Kama kawaida humo ndani ujumbe "haswa" uliotaka utufikie umeshatufikia.
 
Pasco katika utetezi wako huu ndio umeharibu. Mmoja wa watu walio sema kwa nguvu kuwa makala zako hazikuwa za kumharibia Kabendera ni mie, lakini wote tulijua kuwa kesi alizofunguliwa ni za kutunga hazina uhusiano na yeye maana watesi wake wamesimamia msimamo kuwa Kabendera amekuwa akiichafua nchi nje.

Kwa makala yako nikama unataka tuamini kuwa kilichomtesa sio kazi yake bali ni utakatishaji fedha ndio maana amelipa 100M na atalipa mamilioni mengine for six month.

Pasco, Kabendera kalipa 100M? Au ni mchezo unachezwa kuipa serikali advantage kuwa mashtaka yetu yalikuwa sahihi?

Wewe ni Investigative Journalist, hebu ingia chimbo utuambie hela hizo zilizolipwa kwa DPP zilikuwa zimehifadhiwa bank gani? Na zimepokelewa na kuingizwa account gani ya serikali? Fuatilia kwa wakili wake akupe risiti ( ERV) ya mapokezi ya fedha hizo. TUANZIE HAPO.

Hili shinikizo la wafadhili lingekwepeshwaje kama sio kutumia hadaa? Na Kabendera bado alikuwa anauhitaji Uhuru wake hivyo sio ajabu kukubali maelekezo ya mchezo ili akakae na mkewe!

Anyway, naweza kuwa wrong kiasi Fulani. Lakini kuachiwa kwake sio sababu ya kufuta tuhuma zako dhidi yake bali tuhuma zako juu ya yaliyompata Kabendera zilisha futika siku nyingi kwa ukweli uliouweka hadharani kwa kauli zako. Achana na vibaka waliokuwa wanaendelea kukushikia bango kwa ushabiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni mtu mzima, sio kijana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umemsamehe nani sasa? na Kwa kosa lipi? yanayofanyika gizazi kuna siku yatamulikwa na watu watajionea
 
Pascal Mayalla Kabendera amekiri makosa ya ML & tax evation. Wanaojaribu ku -spin hii story eti amelazimika kununua uhuru wake wanamchafulia jina kwa kumfanya mpiga dili za kukiuka mujibu wa sheria. Hamumsaidii kwa Hoja hizo za kitoto, bora mumuwache ajenge reputation yake afresh.Maana sasa huyu sio mshukiwa ni convict wa Kuhujumu Uchumi
Hivi Rais akihujumu uchumi anapelekwa mahakama ipi?
 
Back
Top Bottom