Baada ya ukweli wa Erick Kabendera kubainika, wote walionituhumu kuhusika nimewasamehe kwani Mungu amewasamehe. Msirudie tena!

Kwa juhudi zako hizi za kuja JF kujitetea...
Nimekuelewa; lakini naomba niiache akili yangu ifanye maamuzi yake!!
 
Pascal Mayalla,
kuna "voluntary confession and a confession by inducement" A confession by inducement may result to the untrue admission of guilt" Ikiwa facts zipo wazi kwa nini upelelezi haukamiliki? Unahitaji Barua ya mtuhumiwa kama ilivyoelekezwa na mfalme au lengo ni kutaka ukweli ujulikane mbele ya ulimwengu kwa kutolewa ushahidi?

Tunajua the pre Bargaining yetu kuwa haiko transparent na ipo kwenye makosa yaliyo kwenye committal proceedings /hatua za awali na upelelezi usiokamilika,Hakuna anayependa uhuru wake upotee?Hivyo hata dukani mtu ataingia kununua uhuru kama amabavyo mkolooni alaivyotamani kutunyima uhuru nasi tulitamani kuwa huru.

Anayejua ukweli wa yote ni DPP tu maana yeye ndiye pilato mkuu wetu japo hanawi mikono kama pilato wa Kirumi. Hili Pandora la "detain" and "pre bargain" kuna siku walioanzisha watatamani mbingu zifunuke waingie moja kwa moja bila kufa.what comes around goes around.
 
Pascal Mayalla, Mayalla: Sept 2018, nikiwa naelekea Moshi kwa shuhuli ya Muhimu sana, nilikamatwa na trafic sehemu za Same kwa sababu ya walidai tyre zimechoka. Ukweli tyre Ilikuwa bado nzima kabisa. Baada ya majadiliano ya muda mrefu trafic walinipa option mbili.

Ya kwanza kulipa faini ya sh. 30,000, ya pili nisilipe nisilipe lakini wazuie gari na kesi iende mahakamani. Nili opt kulipa faini. Na tyre hizo mpaka leo nazitumia. Suala la Kabendera kulipa faini haina maana alikuwa na makosa hayo. Ndio maana serikali imesema hakuana ruhusa kukata rufaa. Kabendera ameamua kikiri, kulipa ili arudishiwe uhuru wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
I was undefined
Petro mtu huwezi kukiri makosa usiyoyafanya alafu ukubali kulipa mamilioni ya pesa acheni kudanganya umma. Kama kweli kaonewa basi wakili wake ni mzigo. Nikujulishe mimi nimesoma agreement yake. Mtani ukiisoma hasa page ya pili utabadilisha mawazo.

Nilikua namuonea huruma lakini sasa nikisikia karudishwa jela nitafurahi sana. Jamaa ni mav* kabisa. Subirini mtaona mengi huyoo kakubali kuwa snitch. Sababu hii doc ni nyeti ningeianika hadharani kusingetokea yeyote ws kumuonea huruma. Wote mnajiita rafiki zake subirini tu kugongewa hodi na mapolisi kama mlishirikiana naye katika maongezi yeyote

NAWAOMBEENI PITIENI KESI YA KUBAMBIKWA YA ISAACK WRIGHT JR aliyepewa hukumu ya kwenda jela maisha kwakesi ya kubambikiwa na serikali na kukaa jela miaka 7. Akiwa jela akasomea sheria na kujiwakilisha mwenyewe. Katika rufaa serikali ilikubali atoke baada ya hiyo miaka na yeye afute kesi. Jamaa alikataa na kusema bora afie jela kuliko kukubali makosa ambayo hakuyatenda. Mwishoni akashinda kesi na kufutiwa criminal record.

Petro wewe mwsnasheria tatizo lenu mnafanya biashara zaidi ya kusaidia watu baadhi yenu

[/URL]
 
Hii siyo mkataba kamili mkuu. Aliyekupatia kaweka nusunusu kasome ujurasa wa pili. Aliwekewa bunduki kuusaini? Wakili wake alikua wapi?
 
Pascal, wewe ndie ulienifanya mimi nikajiunga JF na nlikuwa nakuheshimu sana. Ila natangaza tena kama nlivyowahi kutangaza hapo kabla, sikuheshimu kamwe na nlidhani kweli wewe ni mtu Bora ila hufai kutokana na mengi uliyoyaandika humu.
Sema wewe mkuu wakati unamsubilia le mutuz, afikishe wachangiaji mia moja, unatililika na dogo pasikaliii, sijui kilichomsibu nini, sijui hizi teuzi za kujipendekeza ama vyuma ila jamaa nondo za maana zipo ila tu utawala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna watu humu wanataka watu waandike kile wanachokoamini au kukipenda lakini ikija hoja inayotofautiana na mtazamo wao badala ya kutoa hoja ya kuipinga wanakimbilia nkutoa matusi na kashifa kwa mtoa hoja hivi wao watajisikiaje siku wanabambikiziwa tuhuma ambazo hawakuzitenda? ila wakumbumbuke malipo huwa hapahapa duniani.
 
Ni ukweli upi tumeujua mzee? Ni mpuuzi na mpumbavu tu ndie atakaeamini mashtaka ya Eric. Ukweli unajulikana na hata watoto wadogo wanalijua hilo. Unahusika na tabu zote alizopitia Eric hata kama ni kwa asilimia 0.1

Sent using Jamii Forums mobile app
Tatizo unatetea mtu ambaye hata maisha yake ya kila huyajui. Unawezaje kumtetea mtu ukiwa hata hufahamiani naye naye pia hakufahamu, bedroom yake hamko pamoja!
 
Ukweli upi umebainika?Kwa ushahidi upi?Je imethibitishwa bila shaka yoyte kwamba kweli ana makosa au amelazimishwa kukiri ama asotee rumande?
 
Pascal, wewe ndie ulienifanya mimi nikajiunga JF na nlikuwa nakuheshimu sana. Ila natangaza tena kama nlivyowahi kutangaza hapo kabla, sikuheshimu kamwe na nlidhani kweli wewe ni mtu Bora ila hufai kutokana na mengi uliyoyaandika humu.
Hapo ndio unamfanya Pascal Mayalla aendelee kuwa bora zaidi na zaidi. Ili ukubalike sehemu yoyote, lazima wengine wakupende na wengine wakuchukie. Ndio unakuwa mkamilifu. Na uchangiaji wako unamfanya wasiomjua waanze kumjua vizuri. Nao wanaibuka wa kumpenda na wa kumchukia. Yeye tayari ana jina. Tengeneza la kwako tena uwe "verified user" kama yeye.
 
Ndugu Paskali pole sana, nakupongeza kwa kuwasamehe dhidi ya karma maana ile ya Dr.Slaa bado inawatandika. Nimalize kwa kusema pole sana kwa kuchafuliwa hadhi yako humu jamvini na vizabizabina.

aende zake uyo snitch wako, amekalia kujipendekeza tu kuusaka ukuu wa wilaya, watakupa tu hicho cheo ila huache kujipendekeza ata ukawaCOST wengine, au uliumia mwenzio kuupiga mpunga through magazeti ya wazungu, hacha hizo watu kama nyie wakati nasoma tuliwaita mandata pia wanafiki
 
Unacholeta mezani ni dhana. Kwamba kulikuwa na shinikizo lililopelea kuachiwa
Na kwa vile labda aliachiwa kwa shinikizo basi hizo hela hazikulipwa.
That's fine, kama hiyo ni dhana yako sawa tuambiwe kwa nini unaamini hivyo na ututhibitishie. Usimpe kazi tena pasco, eti yeye ndio akatafute ukweli sijui benki, mara risiti kuthibitisha dhana yako ambayo yeye haiamini na anayo ya kwake... Kaka huo ni ufala mkubwa.
Kwa kukusaidia kidogo
Kitendo cha Kabendera kukiri kuna madhara yafuatayo;
1. Hatokata rufaa milele
2. Anatambulika kitaifa na kimataifa kama mhalifu
3. Atapoteza haki za kuajiriwa kwenye utumishi wa umma, mwandishi wa serikali mkurugenzi etc.
4. Hawezi kuteuliwa nafasi yoyote ya umma kama ubalozi, Rc, msemaji wa Rais Zitto nk
5. Hawezi kugombea nafasi yoyote ya kisiasa kama ubunge urais au udiwani.
Kumbuka adhabu yake amepewa full kwa maana ya kulipa deni la kodi 170mls na fine ya 100mls sambamba na kifungo/au fine ya 250000.
Katika kutekeleza adhabu hiyo amelipa hela badala ya kifungo, amelipa 100mls na ameahidi kumalizia 170 ndani ya siku 180.
Katika uhalisia, hii ni 'maximum sentence' kwa mtu aliye fanya plea bargain.
Kama kungekuwa na shinikizo la hao mabeberu basi kungekuwa na UAHUENI ktk adhabu na wasingeruhusu achafuliwe na apoteze haki zake kiasi hiki achilia mbali mafedha aliyotoa ambayo hata hao Armnesty International wanasikitika.
Nakushauri, wajibu wa kuthibitisha kuwa Kabendera hajalipa ni wako wewe unayeamini hivo. Sio Pasco hasa ikizingatiwa mwenyewe amekiri kalipa.
Kwa vile yuko uraiani muulizeni hela alitoa wapi, muulizeni mkewe kweli walifungua kampuni, kweli walihamisha hela.
Serikali hoi ni wapumbavu sana maana hata mkewe alipaswa akamatwe kama mshiriki mwenza katika majimbo sambamba na lile genge lote.
 
Pascal, wewe ndie ulienifanya mimi nikajiunga JF na nlikuwa nakuheshimu sana. Ila natangaza tena kama nlivyowahi kutangaza hapo kabla, sikuheshimu kamwe na nlidhani kweli wewe ni mtu Bora ila hufai kutokana na mengi uliyoyaandika humu.
Akili kama zako ni za kipumbavu kabisa..
Hvi usipomheshimu ww unafikiri atapungukiwa nini? Ww umejiunga jf umemkuta na ubora wake na ndio maana ukashawishika naye kwahyo kutokumheshimu kwako ni kazi bure maana atabaki na ubora wake tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…