TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 25,225
- 25,488
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Petro mtu huwezi kukiri makosa usiyoyafanya alafu ukubali kulipa mamilioni ya pesa acheni kudanganya umma. Kama kweli kaonewa basi wakili wake ni mzigo. Nikujulishe mimi nimesoma agreement yake. Mtani ukiisoma hasa page ya pili utabadilisha mawazo.I was undefined
Wanajishuku, wanajisafidha, ila hakuna siri duniani.Kaka Pascal Mayalla wakati mwingine kukaa kimya huepusha na kuponya. Ingekuwa vyema kama ungebaki kimya. Sasa kwenye suala lile kuna ukweli gani uliothibitika? Wewe umetajwa wapi katika kusafishwa? Pole na chukua mkondo wa kubaki kimya.
Hii siyo mkataba kamili mkuu. Aliyekupatia kaweka nusunusu kasome ujurasa wa pili. Aliwekewa bunduki kuusaini? Wakili wake alikua wapi?Halafu huo mkataba wa kukiri umekaa kikandamizaji sana:
Hii ni sheria ya ajabu sana.
- Ukishakiri kosa unapoteza haki ya kukata rufaa, isipokuwa tu kama rufaa hiyo ni dhidi ya adhabu
- Mkurugenzi wa Mashitaka bado ana haki ya kukata rufaa
- Kwa kukiri makosa unafutiwa pia mashitaka mengine yaliyoshitakiwa pamoja na hayo uliyokiri, lakini ukikiuka makubaliano makosa hayo yote yatafufuliwa (yaani hii iko kimafia kabisa, mfano kama Eric alivyokiri kosa la kutakatisha fedha amefutiwa pia shitaka la kuratibu kundi la kihalifu, lakini akikiuka makubaliano shitaka hili litafufuliwa, maana yake msoto wa jela na kauli za 'upelelezi haujakamilika' zitaendelea indefinitely)
Sema wewe mkuu wakati unamsubilia le mutuz, afikishe wachangiaji mia moja, unatililika na dogo pasikaliii, sijui kilichomsibu nini, sijui hizi teuzi za kujipendekeza ama vyuma ila jamaa nondo za maana zipo ila tu utawala.Pascal, wewe ndie ulienifanya mimi nikajiunga JF na nlikuwa nakuheshimu sana. Ila natangaza tena kama nlivyowahi kutangaza hapo kabla, sikuheshimu kamwe na nlidhani kweli wewe ni mtu Bora ila hufai kutokana na mengi uliyoyaandika humu.
Tatizo unatetea mtu ambaye hata maisha yake ya kila huyajui. Unawezaje kumtetea mtu ukiwa hata hufahamiani naye naye pia hakufahamu, bedroom yake hamko pamoja!Ni ukweli upi tumeujua mzee? Ni mpuuzi na mpumbavu tu ndie atakaeamini mashtaka ya Eric. Ukweli unajulikana na hata watoto wadogo wanalijua hilo. Unahusika na tabu zote alizopitia Eric hata kama ni kwa asilimia 0.1
Sent using Jamii Forums mobile app
Ukweli upi umebainika?Kwa ushahidi upi?Je imethibitishwa bila shaka yoyte kwamba kweli ana makosa au amelazimishwa kukiri ama asotee rumande?Wanabodi,
Kwa vile sisi binadamu tuna uwezo tofauti, na sio watu wengi wanajitambua uwezo wao katika kitu kinachitwa "self realization", ikitokea unajitambua, na unapokasirika kwa kutotendewa haki, kwa kutwishwa misalaba ambayo sio yako, na ukiumia na kulaani watesi wako, na unajua nini kitawatokea pale Mungu anapoamua kukutua msalaba huo, then sauti ya Mungu inakuingia, na hapo hapo unakumbuka na kuwasamehe watesi wako, kabla karma haijaanza kuwafanyia kazi.
Naomba nitoe pole sana kwa mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera kwa anayopitia, na hayuko peke yake katika hayo, kuna wengi wengine pia wanapita katika mapito kama hayo japo ni kwa njia tofauti tofauti, yote haya ni mapito tuu na kuna siku yatafika mwisho na yatapita.
Toka kukamatwa kwake na polisi na kushikiliwa mahabusu kwa miezi 7, msalaba wa kukamatwa huko nilibebeshwa mimi. Eti ni mimi Pascal Mayalla ndiye niliyesababisha kukamatwa kwa Erick Kabendera, kwasababu ya zile makala zangu za uzalendo humu JF.
Hizi ni Baadhi ya Makala Zangu Kuhusu Uzalendo, wale wenye muda, pitieni halafu mnieleze wapi nimemponza mtu yoyote?
Japo nilijifanya mgumu na sijali, kwasababu kiukweli kabisa, makala zile wakati zinaandikwa hazikuwa na lengo la kumchomea mtu yoyote, popote, na wala sikuwahi kuwafahamu waandishi wa makala hizo. Na mpaka sasa ninapoandika leo, bado siwafahamu waandishi wowote wa makala hizo, lakini kwa upande mwingine, kwa vile kuna mwandishi wa habari, Erick Kabendera, amekamatwa katika mazingira ya kutatatisha. Baada ya askari waliotumwa kumkamata kukataa kujitambulisha, hivyo kudhaniwa ni wasiojulikana na Erick akawagomea kuwafungulia, ndipo wakamfanyia utekaji kwanza; kwa kutekwa na kufichwa kusikojulikana kwa muda siku mbili za mwanzo, huku serikali wakitupiana mpira, mara ni polisi, mara ni immigration, na kosa lake mara ni uraia ila full kujiuma uma!.
Ila baada ya kufikishwa mahakamani ndipo kukaibuka uhujumu, utakatishaji fedha na magenge ya uhalifu. No one was sure axactly what is it, hivyo any reasonable man lazima ujiulize, "what if ni kweli mwandishi ni yeye?", "what if ni kweli zile makala zangu ndizo zimeiamsha serikali na kuichochea kumtafuta anayeandika?", "what if ni kweli mwanzo alitumiwa wasiojulikana ili wampoteze kama Azory Gwanda na Ben Saanane lakini baada ya Erick kuunguza picha, ndipo ikashindikana, na kuamua kumtafutia mashitaka yoyote ya kumbambikia just to silence him? Then japo nilikuwa najikaza kisabuni, lakini automatically nilianza kujihisi, na kila siku Erick alipokuwa akifikishwa mahakamani naumia, "what if sababu ni mimi?".
Kila uzi wowote kumhusu Erick Kabendera ukipandishwa humu JF lazima humo ndani ya uzi, lazima nilikuwa natajwa as a "snitch". Kila mateso aliyokuwa anakutana nayo Erick Kabendera, na mimi yalikuwa yananiumiza psychologically. Kwanza nikawa sichangii uzi wowote kuhusu jambo lolote kwa Erick Kabendera.
Mimi ni story teller, kwa wapenda nyuzi fupi, ishieni hapa, na kwenda kule kwenye hitimisho, wapenda mastory ya JF, tuendelee hapa
Sisi Wakristu wa kweli, tunaofuata mafundisho ya Mungu wa Kweli, na kufuata mafunzo ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Kweli, tumefundishwa kusamehe hata saba mara sabini, hivyo mimi kwa upande wangu, niliisha kusamehe toka siku ile ya kwanza ulipopandisha bandiko hili kwa kulipuuza, kwasababu ulikuwa hujui utendalo. Pia nimewasamehe wale wote walionituhumu ni mimi kwa kuamini kuwa kweli ni mimi.
Hitimisho:
Hivyo kwa uzi huu, baada ya ukweli wa mashitaka ya Erick Kabendera kubainika, mimi nimewasamehe "Wale Wote walionituhumu mimi kuhusika na kukamatwa kwa Erick Kabendera, na kufuatia msamaha huo, pia "Mungu nae, amewasamehe" Hakuna tena adhabu ya karma kwenye kunisingizia mimi issue ya Kabendera, ila tafadhalini sana, msirudie tena kumtuhumu mtu mwingine yoyote kwa tuhuma ambazo hamna hakina nazo! Kauli huwa zinaumba, sisi wengine tunajijua kauli zetu na madhara yake, hivyo mkituudhi tusiposamehe.
Hivyo kwa upande wangu, uwe na amani kabisa, na wote mlionituhumu humu na kungine kote, muwe na amani, nimekusamahe na kuwasamehe wengine wote kwa roho safi na roho nyeupe, lakini ili karma isikushughulikie na wewe kwa upande wako, baada ya kuujua ukweli huu, do the right thing, hata kimoyo moyo tu, inatosha Mungu anasikia kila kitu hata usipozungumza, ile kuwaza tuu, is enough!
Ubarikiwe sana.
Paskali.
Hapo ndio unamfanya Pascal Mayalla aendelee kuwa bora zaidi na zaidi. Ili ukubalike sehemu yoyote, lazima wengine wakupende na wengine wakuchukie. Ndio unakuwa mkamilifu. Na uchangiaji wako unamfanya wasiomjua waanze kumjua vizuri. Nao wanaibuka wa kumpenda na wa kumchukia. Yeye tayari ana jina. Tengeneza la kwako tena uwe "verified user" kama yeye.Pascal, wewe ndie ulienifanya mimi nikajiunga JF na nlikuwa nakuheshimu sana. Ila natangaza tena kama nlivyowahi kutangaza hapo kabla, sikuheshimu kamwe na nlidhani kweli wewe ni mtu Bora ila hufai kutokana na mengi uliyoyaandika humu.
Ndugu Paskali pole sana, nakupongeza kwa kuwasamehe dhidi ya karma maana ile ya Dr.Slaa bado inawatandika. Nimalize kwa kusema pole sana kwa kuchafuliwa hadhi yako humu jamvini na vizabizabina.
Unacholeta mezani ni dhana. Kwamba kulikuwa na shinikizo lililopelea kuachiwaPasco katika utetezi wako huu ndio umeharibu. Mmoja wa watu walio sema kwa nguvu kuwa makala zako hazikuwa za kumharibia Kabendera ni mie, lakini wote tulijua kuwa kesi alizofunguliwa ni za kutunga hazina uhusiano na yeye maana watesi wake wamesimamia msimamo kuwa Kabendera amekuwa akiichafua nchi nje.
Kwa makala yako nikama unataka tuamini kuwa kilichomtesa sio kazi yake bali ni utakatishaji fedha ndio maana amelipa 100M na atalipa mamilioni mengine for six month.
Pasco, Kabendera kalipa 100M? Au ni mchezo unachezwa kuipa serikali advantage kuwa mashtaka yetu yalikuwa sahihi?
Wewe ni Investigative Journalist, hebu ingia chimbo utuambie hela hizo zilizolipwa kwa DPP zilikuwa zimehifadhiwa bank gani? Na zimepokelewa na kuingizwa account gani ya serikali? Fuatilia kwa wakili wake akupe risiti ( ERV) ya mapokezi ya fedha hizo. TUANZIE HAPO.
Hili shinikizo la wafadhili lingekwepeshwaje kama sio kutumia hadaa? Na Kabendera bado alikuwa anauhitaji Uhuru wake hivyo sio ajabu kukubali maelekezo ya mchezo ili akakae na mkewe!
Anyway, naweza kuwa wrong kiasi Fulani. Lakini kuachiwa kwake sio sababu ya kufuta tuhuma zako dhidi yake bali tuhuma zako juu ya yaliyompata Kabendera zilisha futika siku nyingi kwa ukweli uliouweka hadharani kwa kauli zako. Achana na vibaka waliokuwa wanaendelea kukushikia bango kwa ushabiki.
Sent using Jamii Forums mobile app
Akili kama zako ni za kipumbavu kabisa..Pascal, wewe ndie ulienifanya mimi nikajiunga JF na nlikuwa nakuheshimu sana. Ila natangaza tena kama nlivyowahi kutangaza hapo kabla, sikuheshimu kamwe na nlidhani kweli wewe ni mtu Bora ila hufai kutokana na mengi uliyoyaandika humu.