Baada ya vifo vya Said Oswayo na mkewe, Swalha Salum mali zinatakiwa kwenda katika Familia ya Mke au Mume?

Mleta mada, unakuja jamiiforum kutafuta ushauri!! Sio kwamba hawapo waislamu wanaozijua sheria za mirathi. Allah a'lam!

Ushauri wangu, mtafute sheikh aliesoma, anajua haya mas'ala ya urithi wa mali, na sio wadau wa sheria.

Tafuta sheikh, usifikiri hiki kitu rahisi rahisi tu kupata jibu. Hao wanasheria wanajua nini taratibu za kiislamu!!! Tusomeni dini ndugu zangu waislamu, haya ndio madhara yake mnaangukia kwa wadau wa sheria. Haijulikani ni dini gani hao watu.
 
Uwezekano wa kuwa kuna mali imepatikana ndani ya muda huo wa miezi 5 ya ndoa yao ni mdogo sana ingawa inawezekana.

Ndugu wa mke kuweni wapole mtoto wa marehem achukue mali za baba ake. Kama kuna chochote chenye jina la mke mtapewa
 
Hivi mfano ikitokea upande mmoja unataka sheria ya kiislam itumike kwenye mirathi na upande mwingine unataka sheria za kiserikali zitumike. Hapo inakuwaje?
 
Mi tangia mwanzo nilikuwa nawaza mashemeji kujazana nyumbani ndoa haina hata miezi sita, ndomana mimba haingii, itaingiaje mmejazana ndani ya nyumba ya wanandoa wapya [emoji1787]
Mimi wabongo mmenichosha[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hivi mfano ikitokea upande mmoja unataka sheria ya kiislam itumike kwenye mirathi na upande mwingine unataka sheria za kiserikali zitumike. Hapo inakuwaje?
Mwisho wa yote katiba na sheria za nchi ndo zitaamua.Hayo mambo ya dini yatapigwa chini kesi ikifika mahakamani.Kwenye dini Kuna ubaguzi ambao unavunja katiba na sheria za nchi.Mtoto wa nje ya ndoa kwenye dini anachukuliwa kuwa haramu lakini katiba inalinda usawa na sheria ya mtoto ya 2009 inatambua watoto wote kuwa sawa na sheria za urithi zinawapa watoto wote haki ya kurithi.Mahakama ilishaliweka wazi swala hili.
 
Umasikini mbaya Sana unaweza ukauza mwanao wa kike kisa njaa. Ama unafurahi mwanao akiiba
 
Hivi mfano ikitokea upande mmoja unataka sheria ya kiislam itumike kwenye mirathi na upande mwingine unataka sheria za kiserikali zitumike. Hapo inakuwaje?
Sheria za serikali huwa zimeakisi dini rules I think hazitofautiani sana
 
Hivi mfano ikitokea upande mmoja unataka sheria ya kiislam itumike kwenye mirathi na upande mwingine unataka sheria za kiserikali zitumike. Hapo inakuwaje?

Ndoa ilifungwa kiserikali au kidini? Kama ilifungwa Kwa dini ya kiislam basi ni wazi taratibu za sheria za kiislam zitafuatwa. Kama Walifunga Bomani basi sheria za nchi zitafuatwa
 
Mtu unafungua uzi kabisa kujadili mali za marehemu ambao hawakuhusu!
 
Umasikini mbaya Sana unaweza ukauza mwanao wa kike kisa njaa. Ama unafurahi mwanao akiiba

Sikiliza mkuu, waliofiwa familia zao ni waislamu, Sasa, kinachokuleta humu ni nini!! Halafu unaongea viyu havina mantiki yoyote!! Sheria za mirathi huzijui, acha wenyewe walishughulikie kupitia kwa masheikh.

Wadau wa sheria/serikali, mahakamani, polisi, hapa sio mahali pao.
 
Hivi mfano ikitokea upande mmoja unataka sheria ya kiislam itumike kwenye mirathi na upande mwingine unataka sheria za kiserikali zitumike. Hapo inakuwaje?

Mkuu wenger, mimi cna elimu, ndio maana nikashauri wamuone sheikh, waachane na hao wadau wa sheria/serikali.

Au wawasiliane na masheikh wa zanzibar, kuna sheikh mmoja amesoma sana anaitwa Shaaban Albattashi. Wengi watakua humu watakua wanamjua
 
Okay mkuu.
 
Kifupi walifunga ndoa ya Bakwata ambayo hamrithishi mwamamke mali. Hivo pointi ya msingi ni moja tu wosia na warangi lazima wafoji ndo maana hawataki kufungua nyumba.
 
NATAKA NISEME KIDOGO.
HAPA KUNA MASUALA MENGI YA KUZINGATIA.
1, YALITOKEA MAUAJI KWANZA
KATIKA QURAN SURATUL NISAA
'Na haiwi Muumini kumuuwa Muumini ila kwa kukosea. Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukosea basi amkomboe mtumwa aliye Muumini, na atoe diya kuwapa jamaa za maiti, isipo kuwa waache wenyewe kuwa ni sadaka. Na akiwa ni jamaa wa maadui zenu, hali yeye ni Muumini, basi ni kumkomboa mtumwa aliye Muumini. Na akiwa ni miongoni wa watu ambao pana ahadi baina yenu na wao basi wapewe diya watu wake na akombolewe mtumwa Muumini. Na asiye pata, basi afunge miezi miwili mfululizo, kuwa ni toba kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi na Mwenye hikima. (92) Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.'

KWA HIVYO SAID (ALIYEFARIKI),
MOJA KATIKA ALIYOTAKIWA KUFANYA NI , ALITAKIWA KULIPA FIDIA KWA FAMILIA YA MWANAMKE KAMA ALIMUUA SIO KWA KUSUDI, ILA IKIWA FAMILIA YA MWANAMKE IMESAMEHE HAMNA NENO.

2. SAID (ALIYEFARIKI) JEE WATOTO WALIOWAZAA ALIWAZAA NJE YA NDOA , AU ALIWAPATA WAKATI AMESHAOA? IKIWA ALIWAPATA BAADA AMESHAOA WANA FUNGU LAO, IKIWA ALIWAPATA KABLA YA KUOA HAWANA KITU HAPO.

3. IKIWA KUNA WATOTO WA NDOA, MKE ATAPATA CHAKE 1/8 AMBACHO KITAKWENDA KWA FAMILIA YAKE, LA IKIWA HAKUNA WATOTO WA NDOA MKE ATAPATA CHAKE 1/4.

4. MALI ZOTE AMBAZO SAID ( ALIEFARIKI) ALIMUANDIKIA MKEWE HIZO ZOTE HAZITOINGIA KWENYE MIRATHI.
MALI AMBAZO SAID AMEACHA WASIA APEWE MKEWE, HAITOWEZEKANA KUPEWA KWA SABABU KILA MWENYE KURITHIWA HAACHIWI URITHI.
KWENYE UISLAM SHERIA ZOTE ZIMEWEKWA HAZIFUATWI SHERIA ZA TWAAHUUTW.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…